Bainisha matatizo ambayo Wanasagamoyo wanakumbana nayo katika upiganiaji wa haki katika eneo la Sagamoyo katika tamdhilia ya Sagamoyo.

      

Bainisha matatizo ambayo Wanasagamoyo wanakumbana nayo katika upiganiaji wa haki katika eneo la Sagamoyo katika tamdhilia ya Sagamoyo.

  

Answers


Francis
? Mchakato wa kupigania haki katika eneo la Sagamoyo unakumbwa na changamoto kwa sababu wananchi wanaoongoza harakati hizo wanakumbwa na matatizo mbalimbali. Uongozi wa Majoka unaowadhulumu wananchi unajaribu kila njia kufisha upinzani.
? Kuwepo kwa mazingira machafu katika soko la Chapakazi. Eneo wanalofanyia biashara limeachwa likiwa chafu. Hali hii inasababisha ukosefu wa riziki na vilevile maisha kuwa magumu.
? Tunu anapigwa na wahuni kutokana na msimamo wake dhidi ya utawala wa Majoka. Anaumizwa miguu na kuachwa na maumivu. Walikuwa wameagizwa kumuua.
? Sudi na Tunu wanasingiziwa kuwa ni wapenzi. Tuhuma hizi zinalenga kuwalegeza katika juhudi zao za kupigania haki. Tuhuma hizi zinamkasirisha Ashua na kumwagiza Sudi ampe talaka yake.
? Baadhi ya waandamanaji wanauawa. Wachuuzi waliokuwa wanaandana kufungwa kwa soko la Chapakazi wanaumizwa na vijana katika kampuni ya Majoka and Majoka kuuawa.
? Kuna juhudi za kumshawishi Sudi kuchonga kinyago cha Ngao. Mradi huu umefadhiliwa na wafadhili kutoka nje. Sudi anakataa licha ya kuahidiwa kuwa mradi huo ungeyabadilisha maisha yake.
? Wananchi wenyewe wanasalitiana. Kombe na Boza hawamuungi Sudi mkono katika harakati za kupigania haki ya Wanasagamoyo. Boza anapinga kila kauli na hatua ya Sudi. Kombe anajiunga na walevi kunywa pombe kwa Asiya. Anapowaona anatoweka badala ya kusaidiana na Sudi na Tunu kuwashawishi Wanasagamoyo kuandamana kupinga kufungwa kwa soko la Chapakazi.
? Ashua anachochewa na Majoka kumwacha Sudi kwa sababu ya umaskini wake na tuhuma kuwa upo uhusiano baina yake na Tunu. Uchochezi huu unalenga kumwondoa Sudi katika harakati za kupinga uongozi wa Majoka.
? Sudi anashindwa na jukumu la kuikimu familia yake. Wanawe, Pili na Pendo wanalia kwa sababu ya njaa. Inamlazimu kuanza kulegeza shinikizo lake la kupigania haki. Tunu anamshajiisha kisha anawachukua Pendo na Pili kuwapeleka kwa mama yake, Hashima, ili awatunze vyema.
? Kuwepo kwa vibaraka wanaomuunga Majoka katika uongozi wake. Vibaraka hawa ni kama vile Kenga na Ngurumo. Ngurumo anawapuuzilia mbali Tunu na Sudi kwa madai kuwa wametamauka. Anadai kuwa Sagamoyo ni pahali pazuri sana. Hali hii inawapa wapiganiaji haki changamoto.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:28


Next: “Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo) (a) Eleza muktadha wa nukuu. (b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu. (c) Eleza sifa tatu za mnenewa. (d) Kwa kifupi, fafanua...
Previous: Utawala wa Majoka ni wa kidhalimu. Thibitisha ukweli huu katika tamdhilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions