Utawala wa Majoka ni wa kidhalimu. Thibitisha ukweli huu katika tamdhilia ya Kigogo.

      

Utawala wa Majoka ni wa kidhalimu. Thibitisha ukweli huu katika tamdhilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
? Mzee Majoka amepuuza utunzaji wa mazingira. Amefungulia ukataji wa miti. Hali hii imesababisha upungufu wa mvua.
? Wakazi wa Sagamoyo wana haki ya kupata huduma bora kulingana na kodi wanayolipa. Hata hivyo, utawala wa Majoka unawatoza kodi Wanasagamoyo wafanyiao biashara zao kwenye soko la Chapakazi ilhali soko lenyewe halisafishwi.
? Wakazi wa Sagamoyo wanawajibika katika kulipa kodi wakiamini kuwa hiyo ni njia ya nchi kujitegemea. Utawala wa Majoka hauoni juhudi hizi. Ashua anasema kuwa uvundo na kuhangaishwa na wenye nguvu ndiyo hewa wanayoipumua. Wanatozwa kodi zaidi au hata kuchukuwa kila kitu.
? Wananchi wana haki ya kufanya biashara ili kujipatia riziki; haki ambayo inakiukwa wakati soko la Chapakazi linafungwa na Wanasagamoyo wanakosa mahali pa kufanyia biashara zao. Kwa njia hii wanakosa njia ya kujipatia riziki.
? Wanasagamoyo wananyimwa haki ya kuandamana ili kudai haki yao namna wanavyoandamana kudai kufunguliwa kwa soko la Chapakazi. Askari wanawaua vijana watano na kuwaumiza wachuuzi wengine waliokuwa wakishiriki maandamano hayo. (uk. 16) Si mara ya kwanza hili kutendeka kama anavyodokeza Majoka. (uk. 31)
? Utawala wa Majoka unatumia vitisho ili kusalia mamlakani. Majoka anamfungia Ashua ili Sudi atishike na aende kwa Majoka. Sudi amekataa kuchonga kinyago cha Ngao, na badala yake kuchonga kinyago cha Tunu. Tunadokezewa kuwa Sudi pia amewahi kufungwa na utawala huu. (uk. 46)
? Dhuluma inadhihirika wakati Majoka anamtumia Chopi wakiwa na Ngurumo katika njama ya kumwua Tunu. Hata hivyo, Chopi anakosa kufaulu kumwua Tunu na badala yake wanamuumiza tu.
? Dhuluma katika jamii ya Sagamoyo itakoma iwapo uongozi dhalimu wa Majoka utaondolewa na kuwekwe mamlakani utawala unaojali haki ya raia. Kufikia mwisho wa tamthilia, matumaini ya kukomeshwa kwa uongozi huo yanaonekana wakati Tunu, Sudi na wengine wanamwondoa Majoka mamlakani.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:31


Next: Bainisha matatizo ambayo Wanasagamoyo wanakumbana nayo katika upiganiaji wa haki katika eneo la Sagamoyo katika tamdhilia ya Sagamoyo.
Previous: Fafanua nafasi/mchango wa vyombo vya habari katika jamii ya Sagamoyo ya tamdhilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions