Fafanua nafasi/mchango wa vyombo vya habari katika jamii ya Sagamoyo ya tamdhilia ya Kigogo.

      

Fafanua nafasi/mchango wa vyombo vya habari katika jamii ya Sagamoyo ya tamdhilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
Vyombo vya habari vilivyorejelewa katika tamthilia ni redio, runinga, gazeti na mitandao ya kijamii.
? Vyombo vya habari ni muhimu katika kupasha watu habari. Mjumbe (uk. 4-5) anawapasha kina Sudi habari kuhusu sherehe za uhuru.
? Kadhalika huburudisha wafanyakazi wakiendelea kuchapa kazi, pengine zikachukua nafasi ya nyimbo za hodiya. Sudi anasikiliza wimbo wa taarabu kwa redio yake ya simu, ambayo pia ndiyo inawapasha habari kuhusu sherehe za uhuru.
? Vyombo vya habari vilevile hutumiwa kufanyia utafiti. Sudi anamweleza Kenga aingie mtandaoni atafiti kuhusu shujaa anayemchonga. (Tunu)
? Kadhalika, gazeti linaangazia harakati za kuupinga utawala wa Majoka, kwa mfano maandamano. Linafahamisha kuwa Tunu aliwahutubia waandishi wa habari na kuwaeleza masaibu ya Wanasagamoyo.
? Vyombo vya habari pia hutumiwa kuonyesha umaarufu wa viongozi. Gazeti lina habari kuwa asilimia sitini ya Wanasagamoyo iko tayari kumpigia Tunu kura akiwania uongozi, jambo linalowashangaza Kenga na Majoka. (uk. 33)
? Pia huifanya jumuiya ya kimataifa kujua mambo yanayoendelea katika maeneo mbalimbali.
? Maendeleo ya teknolojia yamewawezesha wengi kupata habari kupitia mitandao ya kijamii. Kupitia kwayo, Kenga anapata habari ambazo zinapeperushwa na Runinga ya Mzalendo na kumfahamisha Majoka. Tunapata kujua kuwa vyombo vinavyoeneza ukweli kuhusu utawala wa kidhalimu huwa mashakani. Majoka anasema Runinga ya Mzalendo itafungwa, ibaki tu Sauti ya Mashujaa.
? Baadhi ya vyombo hutumika kueneza propaganda na sera za utawala dhalimu. Mjumbe (uk 4-5 na 86-87) anatumiwa kupigia debe maslahi ya Majoka huku akipuuza jitihada za wanaompinga Majoka akiwaita ‘wachache waliojazwa kasumba za kikoloni’. (uk. 5) Ni wazi kuwa vyombo vya habari vyaweza kutumiwa kunufaisha jamii na wakati huo huo kuidhulumu na kuipotosha.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:46


Next: Utawala wa Majoka ni wa kidhalimu. Thibitisha ukweli huu katika tamdhilia ya Kigogo.
Previous: Eleza jinsi methali zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions