Eleza jinsi methali zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.

      

Eleza jinsi methali zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.

  

Answers


Francis
? Fuata nyuki ule asali (ukitaka kula asali kaa na nyuki) Methali hii imetumika kuonyesha kuwa ukitaka kupata kitu, kaa na walionacho. Asiya na Ngurumo walimwandama Bi. Husda hadi wakapata kandarasi ya kuoka keki.
? Chelewa chelewa utapata mwana si wako. Boza, Kombe na, Sudi wasichelewe kuchonga vinyago ili wafaidi, na majina yao yajulikane nje.
? Mbio za sakafuni, huishia ukingoni. Kenga anatumia methali hii kurejelea kuwa harakati za Tunu kuleta mabadiliko Sagamoyo hayatafanikiwa. Kauli hii ni kinaya.
? Udongo haubishani na mfinyanzi. Wenye nguvu hawabishani na wanyonge. Boza anatumia methali hii kumwonya Sudi asibishane na Majoka anapodai kuwa keki wanayoletewa ni makombo.
? Aketiye na cha upele, haishi kujikuna. Sudi anatumia methali hii kurejelea Kombe anapomuunga mkono na kusema mambo yamekwenda kombo Sagamoyo.
? Simba hageuki paka kwa kukatwa makucha. Kuwa Majoka alikosa fursa ya kumwoa Ashua haimanishi hana uwezo wa kumfanyia lolote.
? Kuvuja kwa pakacha ni nafuu kwa mchukuzi. Kuvunjika kwa ndoa ya Ashua au Ashua kutalikiwa itakuwa heri kwa Majoka ili ampate Ashua
? Heri kufuga mbuzi, binadamu wana maudhi. Majoka anatumia methali hii Ashua anapokataa ombi lake. (uk. 26)
? Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake. Kenga anarejelea wafadhili wa gazeti kuwa walimtetea Tunu na habari kumhusu zimetiwa chuvi. Waandishi wa gazeti ni wafadhili wa Tunu. (uk. 33)
? Dalili ya mvua ni mawingu. Tunu huenda akaongoza Sagamoyo.
? Ukitaka kuwafurusha ndege, kata mti. Kenga anamrejelea Jabali, kuwa ukitaka kuwaangamiza maadui au kiongozi wao. Jabali alikufa na wafuasi wake kumfuata ahera. (uk. 35)
? Udongo uwahi ungali mbichi. Wangemkomesha Tunu kabla ya kupata umaarufu.
? Asante ya punda ni mateke. Majoka anamrejelea Tunu kwa kumpinga baada ya kugharamia masomo yake baada ya kifo cha babake.
? Maji ukiyavulia nguo yakoge. Majoka amekubali kuhukumiwa na kujibu mashtaka kwa kutowajibika kwake na kusaliti nchi yake. (uk. 79)
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:48


Next: Fafanua nafasi/mchango wa vyombo vya habari katika jamii ya Sagamoyo ya tamdhilia ya Kigogo.
Previous: Fafanua sifa na umuhimu wa Kenga katika tamthilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions