Fafanua sifa na umuhimu wa Kenga katika tamthilia ya Kigogo.

      

Fafanua sifa na umuhimu wa Kenga katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
? Kenga ni mshauri mbaya. Anamshauri na kuunga mkono hatua ya Majoka kwenda kumuua Tunu. Anashauri amfungie Ashua kizuizini kwa tuhuma ya kuzua vurugu katika afisi ya serikali.
? Ni kibaraka wa Majoka. Anaunga mkono maamuzi anayofanya hata yakiwa mabaya. Anaunga mkono hatua ya kufunga soko na kujenga hoteli.
? Ni barakala. Anajipendekeza kwake Majoka na kumshauri na kumuunga mkono. Anatarajia kupata manufaa kama vile ardhi na hata uongozi wa jimbo hili.
? Ni katili. Ni ukatili mkubwa kumfunga mtu kwa kosa ambalo hakulitenda. Kenga anamshauri Majoka kumtia Ashua ndani ili waweze kumshurutisha Sudi akubali kutekeleza mradi wa kuchonga kinyago cha Ngao. Anadai polisi wanafanya kazi yao vizuri kwa kukabiliana na waandamanaji. (uk. 31)
? Kenga ni msaliti. Anapoona utawala wa Majoka umeporomoka anamgeuka na kushindwa kumsaidia. Anamwambia Majoka kuwa mbio za sakafuni zimefika ukingoni, na ikiwa Majoka amekataa kushindwa, yeye anaungama kushindwa. (uk. 91)
? Ni mpyaro. Anamwita Tunu ‘hawara’. (uk. 12)
? Ni mwenye ujuzi wa kupanga mikakati ingawa mikakati anayoipanga inachangia wizi na unyanyasaji. Anapanga mikakati ya ubomoaji wa soko la Chapakazi na ujenzi wa hoteli katika eneo la soko. Ndiye anayemwongoza Majoka kumfungia Ashua korokoroni kwa kisingizio cha kuzua vurugu katika afisi ya serikali.
? Kenga ametumiwa na mwandishi kuonyesha jinsi ushauri mbaya unavyopotosha na kuleta maangamizi. Majoka anapokaribia kuangamia, Kenga anamsaliti. Yeye ni kielelezo cha marafiki ambao hufaidika kutoka kwa mtu akiwa hana tatizo. Tatizo linalopotokea wanatoroka.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:57


Next: Eleza jinsi methali zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.
Previous: Fafanua jinsi mbinu ya sadfa inavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions