Fafanua jinsi mbinu ya sadfa inavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo.

      

Fafanua jinsi mbinu ya sadfa inavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
? Ashua akiwa na Majoka ofisini, Husda anaingia bila kutarajiwa, Ashua anamaka na kubakia kinywa wazi.
? Majoka anaposoma gazeti anaona maoni kuwa Tunu awanie uongozi Sagamoyo, hakutarajia kuyaona maoni hayo gazetini.
? Chopi wanapozungumza na Majoka Mwango anafika na habari kuwa Majoka ana wageni, Tunu na Sudi ambao hakutarajia.
? Majoka anapongojea Husda katika hoteli ya kifahari Sagamoyo, Kenga anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga, kuwa Tunu bado yupo, hakuvunjwa miguu, Majoka hatarajii Tunu kuwa mzima.
? Ni sadfa kwa kifo cha Ngao Junior kutokea sawia na kifo cha Ngurumo.
? Majoka anazirai siku kabla ya sherehe ya uhuru, anapopata habari kuhusu kifo cha Ngao Junior.
? Inasadifu kuwa siku ya sherehe ndio waandamanaji wanakuwa na mkutano katika soko la Chapakazi wakati ambapo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:59


Next: Fafanua sifa na umuhimu wa Kenga katika tamthilia ya Kigogo.
Previous: Eleza jinsi umaskini unavyoathiri wenyeji wa Sagamoyo katika tamthilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions