Eleza jinsi umaskini unavyoathiri wenyeji wa Sagamoyo katika tamthilia ya Kigogo.

      

Eleza jinsi umaskini unavyoathiri wenyeji wa Sagamoyo katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
Umaskini katika eneo la Sagamoyo unatokana na uongozi wa Majoka usiojali masilahi ya wananchi. Uongozi huu umejikita katika udhalimu na ufisadi hivi kwamba ni wachache ndio wanaonufaika nao huku wengi wakibebeshwa mzigo mzito wa kulipa kodi.
? Uongozi wa Majoka unaendeleza umaskini kwa kutolewa sera madhubuti za kukuza uchumi na nafasi za wafadhili zinazotumiwa kufadhili miradi isiyokuwa na faida kwa wananchi. Kenga anamwambia Sudi kuwa mradi wa kuchonga kinyago cha Ngao umefadhiliwa kutoka nje. Kwa kweli kinyago hiki hakina faida kwa wananchi ambao wanasalia katika umaskini. (uk. 11)
? Sagamoyo ina madeni makubwa na jukumu la kulipa madeni hayo limeachiwa wananchi. Mradi wa kuchonga kinyago umefadhiliwa kwa mkopo ambao unafaa kulipwa kwa muda wa miaka mia moja. Hii ina maana kuwa Wanasagamoyo watasalia katika ufukara huku wakikazana kulipa deni la fedha ambazo hazikuwafaa kitu.
? Kutokana na umaskini, Wanasagamoyo wengi wanalazimika kufanya kazi ya uchuuzi katika soko la Chapakazi ili kujipatia riziki. Biashara yao haiendi vyema kwa kuwa kodi iko juu na wafanyabiashara wanahangaishwa sana. (uk. 2) Chai ya mkandaa ni ishara kuwa chakula cha Wanasagamoyo ni duni. Kadhalika watoto wao Ashua na Sudi wanatafunwa na njaa kwa kukosa chakula. Kwa Majoka kuna chai ya maziwa (uk. 31) na anaagiza mkewe aambiwe ampikie chapati kwa kuku. (uk. 30)
? Umaskini Sagamoyo unaosababishwa na utepetevu wa Majoka umewafanya wananchi kuwa wategemezi. Majoka amefungulia biashara ya ukataji miti. Hali hii inaweza kusababisha ukosefu wa mvua na hivyo yaelekea Wanasagamoyo watatumia maji yatokayo ng’ambo. (uk. 53) Kilimo pia kimeathiriwa na hamna chakula cha kutosha kama anavyodokeza Hashima.
? Kufungwa kwa soko la Chapakazi kumewaingiza Wanasagamoyo katika umaskini mkubwa. Watu wengi wanalitegemea soko hilo kukidhi mahitaji yao. Kufungwa kwa soko hilo kwa mujibu wa Ashua (uk. 25) ni sawa na kuzika matumaini yao. Ndiyo sababu Hashima anapepeta “kichele” huku akishangaa watakula nini wakingoja soko kufunguliwa. (uk. 52)
? Umaskini huweza kusababisha mtafaruku katika ndoa. Ashua akiwa kizuizini anatishia kumwacha Sudi, anasema amechoka kupendwa kimaskini. Sudi anamhimiza asimwache kwani ugumu huo wa maisha ni wa msimu tu, utapita.
? Umaskini ndio unaosababisha wafanyakazi katika eneo la Sagamoyo kugoma. Licha ya kuwepo kwa maandamano yanayoongozwa na Tunu kupinga kufungwa kwa soko la Chapakazi, wauguzi na walimu pia wanagoma. Wanagoma ili kushinikiza nyongeza ya mishahara. Wamekataa kuvumilia kuishi kimaskini. Hata hivyo Majoka anataja kuwa atawaongezea asilimia kidogo ya mshahara kisha kodi ipandishwe. (uk. 36)
? Mwandishi anaonyesha kuwa jamii ya Sagamoyo ina watu wengi ambao ni maskini. Anaulaumu uongozi uliopo kwa kutorekebisha sera za kiuchumi zinazoendeleza umaskini. Kuwepo kwa deni kubwa, utegemezi na migomo ni ishara ya umaskini kuwepo kwa kiwango kikubwa. Hivyo basi ili kukabiliana na umaskini uliopo Sagamoyo, wahusika Tunu na Sudi wanajaribu kwa kila hali kuondoa uongozi wa Majoka.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 08:24


Next: Fafanua jinsi mbinu ya sadfa inavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo.
Previous: Eleza sifa na umuhimu wa Husda katika tamthilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions