Eleza sifa na umuhimu wa Husda katika tamthilia ya Kigogo.

      

Eleza sifa na umuhimu wa Husda katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
Husda ni mke wa Majoka; ni mama yake Ngao Junior. Asiya ni mkoi wake.
? Ni mwingi wa hasira. Anapoingia afisini mwa Majoka, anashangaa kumpata Ashua. Anapandwa na hasira. Anatishia kumuua Ashua. (uk. 26)
? Ni mwenye dharau na kejeli. Anamdharau Ashua kwa kisomo chake. Anamwambia kuwa ikiwa ameshindwa kufuga kuku, atawezaje kumfuga kanga?
? Mwenye vitisho. Si kwa Ashua tu, bali pia mumewe. Majoka anamwambia achunge ulimi wake, anamjibu: Wa kujichunga ni wewe pwagu. Mtanitambua leo na huyu hawa... (uk. 27).
? Mwepesi wa kutuhumu maanake mara anapompata Ashua ofisini, anadai yeye ndiye anamfanya Majoka kutoonekana kwake. Anasema kuwa Ashua daima anachana vichochoro kuwinda wanaume. (uk. 27)
? Ni mpenda raha. Anaenda na mumewe katika hoteli ya Majoka and Majoka Modern Resort kupunga unyunyu.
? Ni mdanganyifu. Hana mapenzi ya dhati kwa mumewe, kama Majoka anavyoweka wazi akiwa ndotoni. Anachotaka ni mali ya Majoka na yuko tayari kuilinda kwa jino na ukucha. Anapigana na Ashua kwa kutuhumu kuwa anacheza na mumewe. Anaingiwa na wasiwasi wakati Majoka anazirai na kupoteza fahamu.
? Mwenye uchu. Anamwangalia Chopi kwa jicho la uchu na kutembea kwa madaha ili kumvutia. (uk. 70)
? Licha ya tabia zake mbaya, Husda ni mtambuzi kwa vile anaelewa baadhi ya mambo yanayofanya ndoa kuingia doa. Anasema wanaume wanapaswa kujidadisi na waseme na wake zao kwa henezi huku wakiwaheshimu. (uk. 77)
? Husda ni mhusika anayewakilisha wanajamii wanaoishi na viongozi dhalimu ila hawawezi kuwashauri. Hawajajitokeza kupigania mabadiliko katika jamii. Wanafikiri hali ni salama. Kwa mfano Husda anaenda kustarehe katika hoteli ya kifahari na mumewe huku Wanasagamoyo wanaendeleza harakati za ukombozi.
? Ametumiwa kuendeleza maudhui ya ndoa na mapenzi. Mwandishi anaonyesha baadhi ya wanandoa wamo katika asasi hii ili kunufaika kwa mali lakini hawana mapenzi kwa wenzi wao.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 08:28


Next: Eleza jinsi umaskini unavyoathiri wenyeji wa Sagamoyo katika tamthilia ya Kigogo.
Previous: Eleza sifa na umuhimu wa Asiya katika tamthilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions