Eleza sifa na umuhimu wa Asiya katika tamthilia ya Kigogo.

      

Eleza sifa na umuhimu wa Asiya katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
Asiya anajulikana kama Mamapima. Jina hili ni la kimajazi linaloashiria kazi anayoifanya ya kuwapimia wateja wake pombe. Asiya ni mke wa Boza.
? Ni mpenda anasa. Licha ya kuwa na mumewe Boza, anashiriki mapenzi na Ngurumo ili apate mradi wa kuoka keki ya sherehe za uhuru. Vilevile anashiriki ulevi wa pombe.
? Ana tamaa. Kushiriki kwake katika kula uroda ili kupata kandarasi kunaashiria tamaa yake. Pia kunaashiria kuwa yeye ni fisadi, hataki kufuata hatua halali za kutafuta kandarasi. Vilevile kibali cha kuuza pombe haramu alipata kwa njia isiyokuwa halali.
? Ni mcheshi. Anawakaribisha wateja wake kwa furaha. Anakimbia mbio kuwakaribisha wageni wake. Anawaambia Tunu na Sudi kuwa kwake utaipata furaha. (uk. 60)
? Ni katili anayejali mapato yake tu. Kwa sababu ya ubinafsi huo, anahiari kuuza pombe inayowapofusha na kuwaua wale wanaoibugia.
? Mwingi wa vitisho kwa vile anawapa kina Tunu muda wa dakika moja kuondoka kwake mangweni lau sivyo watajua kwa nini anaitwa Mamapima. (uk. 62)
? Mwenye majuto. Mwishoni mwa tamthilia, Asiya anatambua kuwa alikuwa anawapunja na kuwapotosha Wanasagamoyo kwa hivyo anawaomba kina Tunu msamaha na kuomba wamlinde. (uk. 92)
? Ni tapeli. Anawatapeli Wanasagamoyo kwa kuwauzia pombe haramu iliyopigwa marufuku. Anajua madhara ya pombe hiyo ila anaiuza tu.
? Asiya ni kielelezo cha watu wanaotumia uhusiano wao na viongozi ili wanufaike wao. Mwandishi anamtumia kuonyesha thamani ya msamaha katika ujenzi wa jamii mpya. Tunu anamsamehe anapokuja kuomba msamaha. (uk. 92)
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 08:46


Next: Eleza sifa na umuhimu wa Husda katika tamthilia ya Kigogo.
Previous: Eleza sifa na umuhimu wa Ngurumo katika tamthilia ya Kigogo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions