Eleza sifa na umuhimu wa Ngurumo katika tamthilia ya Kigogo.

      

Eleza sifa na umuhimu wa Ngurumo katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


Francis
Ngurumo ni kijana mpenda anasa. Anajulikana sana Sagamoyo kwa uraibu wake wa vileo. Ni mfuasi sugu wa Majoka.
? Ni mpenda anasa. Mlevi ambaye hunywa pombe kwa Asiya. Kwa mujibu wa Boza, Asiya alipata mradi wa keki kwa kumpa Ngurumo uroda. (uk. 64)
? Ni mkware. Anahusiana kimapenzi na mke wa mtu. Hata hafichi. Anasema Asiya ni wao wawili; yeye na Boza. (uk. 64)
? Ni mwenye kejeli. Anatumia kejeli anapowazungumzia Sudi na Tunu. Anakejeli uhusiano wa Tunu na Sudi.
? Ni mwenye mtazamo finyu kuhusu maisha. Haoni faida ya kufunguliwa kwa soko la Chapakazi. Anaona uzuri wa kuhudhuria sherehe za uhuru.
? Ni katili. Alishiriki kumuumiza Tunu na hata anamkumbusha.
? Hata baada ya kuwa mfuasi sugu wa Majoka, Ngurumo anakufa baada ya kunyongwa na chatu. Vyombo anavyotumia Majoka kuwaangamiza wasiomuunga mkono vinampata Ngurumo na kumwangamiza.
? Ngurumo anaishi maisha ya kujidanganya kuwa yu salama. Majoka anayempigia debe na kumsifu ndiye anayemwangamiza.
? Kwa namna moja Ngurumo anawakilisha vijana wanaotumiwa na viongozi kufanikisha malengo yao ya kisiasa lakini pindi wanapoonekana hawafai, wanaangamizwa. Mwandishi amemtumia kuwaonya wanaounga mkono watawala dhalimu ambao hawawathamini hata chembe.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 08:48


Next: Eleza sifa na umuhimu wa Asiya katika tamthilia ya Kigogo.
Previous: Huku ukirejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, fafanua namna ubadhirifu wa mali ya umma unavyoendelezwa.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions