Huku ukirejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, fafanua namna ubadhirifu wa mali ya umma unavyoendelezwa.

      

Huku ukirejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, fafanua namna ubadhirifu wa mali ya umma unavyoendelezwa.

  

Answers


Francis
? Mzee Mambo analipwa mshahara mnono kama mkuu wa wizara zote ilhali kila wizara ina waziri wake.
? Sherehe kubwa za viongozi wa serikali zinatumia mali ya umma. Hivyo basi kuchangia ubadhirifu wa mali katika jamii.
? Viongozi huendeleza ubadhirifu kwa kutumia mali ya umma kwa manufaa yao wenyewe. Magari ya serikali yanatumika katika sherehe na kazi za nyumbani kama vile kuleta maji katika sherehe.
? Vyakula katika sherehe vinanunuliwa kwa pesa za umma. Pesa hizi zingetumika kuendeleza asasi za kijamii.
? Ubadhirifu unadhihirishwa pale DJ anapolipwa kuwatumbuiza wageni katika sherehe.
? Ubadhirifu unadhihirishwa na viongozi wa serikali wanaowachukua watu wao wa karibu na kuona kuwa wamefaidika kutokana na raslimali za wanajamii bila kuzitolea jasho.
? Viongozi wa serikali kama vile Sasa na Mbura wanaamua kujipakulia chakula kupita kiasi katika sherehe za Mzee Mambo na jamii yake. Ubadhirifu wa mali ya umma unaonekana ambapo mali ya umma inatumika kuwaajiri mawaziri wawili wenye majukumu sawa katika wizara moja. Kazi hii ingefanywa na waziri mmoja na mshahara wa waziri wa pili ungechangia katika kuinua sekta nyingine.
? Upeperushaji wa matangazo ya sherehe ya kiongozi binafsi katika vyombo vya habari vya kitaifa kwa siku nzima ni ubadhirifu wa mali ya umma. Pesa zilizotumika zingechangia pakubwa katika kuinua uchumi wa taifa.
? Uuzaji wa dawa zilizotolewa katika bohari la kitaifa katika duka la DJ ambayo ni biashara ya mtu binafsi ni ubadhirifu wa mali ya umma.
? DJ kupewa kazi ya mipango na mipangilio katika sherehe ilhali kuna mawaziri wawili wanaolipwa mshahara kwa kazi hiyo ni ubadhirifu wa mali ya umma.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 08:51


Next: Eleza sifa na umuhimu wa Ngurumo katika tamthilia ya Kigogo.
Previous: “Ningeondoka ... mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa maneno haya. (b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo. (c)...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions