Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili jazanda za anwani katika hadithi zifuatazo. a) Shibe Inatumaliza b) Mtihani wa Maisha c) Mkubwa

      

Jadili jazanda za anwani katika hadithi zifuatazo.
a) Shibe Inatumaliza
b) Mtihani wa Maisha
c) Mkubwa

  

Answers


Francis
a) Shibe Inatumaliza
? Sasa na Mbura wanamalizwa na shibe pale wanapokuwa wakiburudika katika sherehe ya mwanawe Mzee Mambo. Mbura anapigiwa simu na rafikiye kumjuza wanaonekana kwenye kioo cha taifa; gazeti na fesibuku – Mbura kawapa watu makavu.
? Kwa mujibu wa Mbura, kula sana kunaleta magonjwa hatari kama vile presha, sukari, saratani na madonda ya tumbo.
? Vilevile, watu wanauana kwa mabomu, risasi, kunyongana kutokana na kula tu.
? Mbura anamfahamisha Sasa kuwa hawawezi kumaliza kula kwani kila siku wanakula vitu wasivyojua vitokako, vyao na vya wenzao. Hii ni jazanda ya viongozi kutumia raslimali za nchi kwa kutojali, ikipigiwa chuku wanakula na wanafisidi haki ya watakaozaliwa miaka hamsini ijayo na ya waliowatangulia.
? Ni tashtiti ya viongozi kama vile Mzee Mambo wasio na maarifa lakini wana pupa ya mali ili wapate mali. Wananyakua vyeo bila kujali wengine. Yeye ni waziri kivuli wa wizara zote.
? Tashtiti ya namna kazi inavyoendeshwa katika serikali. Mzee Mambo haogopi serikali yao, kile kinachoangaziwa zaidi ni kwenda kazini wala si kufanya kazi. Vyeo kazini vinampa fursa ya kupata mshahara si haba.
? Vilevile hadithi inakejeli ufisadi unaotekelezwa serikalini. Viongozi kama vile Mzee Mambo anafadhili sherehe duni kutumia raslimali za umma. Magari yanayotoa huduma, chakula kinacholiwa kinagharimiwa na serikali. DJ na wenziwe hawajali lawama - kwani wangejali hawangechota mabilioni ya serikali katika sherehe ya Mzee Mambo. DJ anamiliki duka kubwa la dawa ambalo mtaji wake ni bohari kuu ya dawa za serikali.
? Anwani inadhihaki kitendo cha ubaguzi kwa wananchi kwani wananyimwa huduma kama vile umeme, matibabu, maji na huduma za kimsingi ikiwalazimu walipe huku wasiojali lawama kama DJ wakipata bure. Almradi tu viongozi washibe kwa kujitosheleza kwa mahitaji yao, hawakumbuki haki zake mwananchi.
? Tashtiti inakuzwa na Sasa na Mbura kuwa chakula walacho si halali bali viplastiki au unga uliosarifiwa ama vifunza vilivyokaushwa ambao ni hatari kwa afya.
? Sasa na Mbura wanakula kupita kiasi, wanajaza sahani, kuzitafuna, kuunga foleni, kujaza tena bila kujali aina ya chakula walacho. Mwishowe, ndipo baada ya shibe wanatambua aina moja ya basmati - mchele duni wa viplastiki vifunza na mwingine ni mbeya.


b) Mtihani wa Maisha
? Samueli analemewa na mtihani wa maisha. Anapofeli mtihani anachukua jukumu la kujirusha kwenye kidimbwi cha maji badala ya kupambana na maisha. Anamwogopa babake mzazi.
? Babake Samueli anakosa kutambua usamehevu wa mzazi. Anakata tamaa ya penzi lake kwa Samueli baada ya kufeli, anamwambia hana faida maishani ajirushe majini afe.
? Mamake Samueli ana penzi la mzazi. Ana elimu ya maisha kwani, anamuomba mwanawe asijitose majini. Vilevile anamuarifu akishindwa na mtihani wa shuleni hawezi akashindwa na wa maisha. Mungu hamkoseshi mja wake yote. Mwishowe anasalimu amri na kumfuata mama.
? Dada zake Samueli wametambua umuhimu wa bidii na kuwajibikia elimu. Wao walipita vizuri wakajiunga na vyuo kama vile Chuo Kikuu cha Kenyatta na Chuo cha Ualimu cha Eregi.
? Wazazi wana matumaini makubwa kwa wanao. Hili linawafanya watie bidii kuwapa kile watakacho ili wasome. Mfano familia nzima inategemea mafanikio ya Samueli mtoto wa pekee wa kiume. Hili linambidi babake auze ng’ombe ili Samueli asome.
? Mwanafunzi anapoanguka mtihani wa mwisho shuleni anakata tamaa ya maisha. Samueli anaondoka nyumbani kuelekea kwenye bwawa lililo karibu na kwao kujitosa majini. Anaogopa ukali wa babake aliyemdanganya hakupata matokeo kutokana na salio la karo.
? Elimu ya shuleni inatoa matokeo ya mtihani wa mwisho unachagua mkondo wa maisha. Wengine wamenywewa kama kuku walioroa maji ya mvua kuashiria kufeli.


c) Mkubwa
? Ni mamlaka aliyo nayo kiongozi ya kumiliki stakabadhi muhimu kama vile paspoti ya kidiplomasia kama vile Mkubwa.
? Ni uwezo wa kiongozi kutumia paspoti ya kidiplomasia inayomilikiwa na viongozi pekee kupitia uwanja wa ndege au bandarini bila kukaguliwa na yeyote.
? Ni uwezo wa kimamlaka alionao kiongozi wa kufanya biashara ya unga bila kujali sheria kwani hakaguliwi na walinzi wanaolinda uwanja au bandarini. Mfano biashara haramu ya unga ya viongozi.
? Ni kigogo aliye na uwezo wa kuhonga ili mzigo wake ulioshikwa uachiliwe. Mkubwa anamwendea Ngwengwe usiku wa manane ili aweze kurejeshewa mzigo wake kwa namna yoyote ile.
? Ni kiongozi wa ulinzi Ngwengwe wa Njagu anayetambuana na vigogo wengine katika uongozi. Anafanya mkutano na Mkubwa usiku wa manane ili kufanya mambo yao yawe sawa.
? Kuwa mkubwa kwa kubadilishwa na biashara ya unga mfano, Mkubwa anabadilika kuwa tajiri wa majumba, maduka na magari ya bei mbaya.
? Aidha, inaonyesha tamaa ya Mkubwa ya kuwa tajiri. Anauza ardhi milioni kumi ili afanye siasa ya kuwa kiongozi ili aweze kuuza unga. Ana tamaa ya kuwa mkubwa – katika uongozi na kubadilisha hali yake ya maisha.
? Wakubwa katika magereza wanafisidi vyakula vya wafungwa na haki nyinginezo kuhiniwa. Nyumbani wanatiliwa mlima wa chakula lakini mahabusu wanafikiwa na bapa. Aidha, wafungwa wana maisha duni ya malezi na usafi.
? Mkubwa ni kiongozi anayeishi maisha ya hali ya juu. Mkubwa alibadilisha nyumba yake rangi na taili mara kwa mara.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 08:57


Next: Huku ukirejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, fafanua namna ubadhirifu wa mali ya umma unavyoendelezwa.
Previous: “Kutazamia shule za vijijini kumwibua bingwa katika mtihani wa kitaifa ni kama kutarajia kupata maziwa kutoka kwa kuku.” (Shibe Inatumaliza) a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b)...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions