Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Hebu kwanza kanawe hilo dongo jekundu miguuni.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua sifa za wandani wa msemaji. (c) Jadili jinsi hadithi hii inavyoafiki...

      

“Hebu kwanza kanawe hilo dongo jekundu miguuni.” (Shibe Inatumaliza)
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua sifa za wandani wa msemaji.
(c) Jadili jinsi hadithi hii inavyoafiki mataifa ya kiafrika.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
? Msemaji ni kijana mbwia unga akiwa kichochoroni.
? Alikuwa akimwambia Mkubwa.
? Alikuwa amekasirishwa na Mkubwa kwa kumsumbua akiwa katika usingizi wake wa ndoto tamu. Mkubwa alikuwa akielekea pwani kununua pweza wa biashara yake.

(b) Fafanua sifa za wandani wa msemaji.
? Wenye vitisho - mmoja wao alitisha kumshambulia Mkubwa. Ilibidi atoroke.
? Wenye matusi/wapyaro - mmoja wao anamtusi Mkubwa mshamba, mavi ya bata, juha we!
? Wezi - Wanawapora wapita njia mali yao. “...ukisinzia washaondoka na kitu.”
? Wasi haya - kwa ajili ya kutojijua hufanya vitendo vya aibu kadamnasi. Ndotoni Mkubwa aliwaona vijana wachafu “wakifanyiana vitendo vichafu vya kaumu kama wanyama.”
? Wavivu- hawafanyi kazi ila kuwapora wapita njia wapate hela za unga. Wanapobwia unga hulala tu na kuota mchana.
? Wepesi wa kushawishika- wanashawishika haraka na wanakuwa watumiaji wa dawa za kulevya.
? Katili – mmoja wao alitishia kumtoa mtu change.

(c) Jadili jinsi hadithi hii inavyoafiki mataifa ya kiafrika.
? Matumizi mabaya ya mamlaka k.m paspoti ya kidiplomasia.
? Uozo wa idara ya magereza – ina mapendeleo mf: Mkumbukwa
? Ufisadi
? Ulanguzi wa dawa za kulevya km. viongozi kama Mkubwa
? Umaskini
? Ujinga km. wakati wa uchaguzi
? Matumizi ya dawa za kulevya
? Ukosefu wa ajira
? Wizi
? Athari za dawa za kulevya
? Athari za maamuzi mabaya katika uchaguzi
? Tamaa k.m Mkubwa
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:09


Next: Jadili suala la mikosi maishani ukirejelea hadithi zifuatazo: i) Nizikeni Papa Hapa ii) Ndoto ya Mashaka
Previous: “Ningeondoka ... mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa maneno haya. (b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo. (c)...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions