(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
? Haya ni maneno ya Jairo.
? Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu.
? Sherehe hii inafanyika shuleni.
? Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kumpatia matumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii.
(b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo.
? Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa matumaini maishani badala ya kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana lazima aibe na aue.
(c) Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu. Thibitisha.
? Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
? Ni kinaya pia kwa mwalimu Mosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosoa badala ya kumsifu.
? Ni kinaya kwa Jairo kuona elimu haina manufaa yoyote ilhali wenzake walifaidi kutoka kwa elimu ya mwalimu wao.
? Ni kinaya kwa Jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili mkewe kama zawadi.
? Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa pombe ni kiliwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masaibu ya maisha na kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
? Ni kinaya kwa mkewe jairo kukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
? Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa ufuska ndio raha ya maisha na kuwa uadilifu haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
? Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi, Sera kukubali na kumkaribisha mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake.
(d) Nini umuhimu wa msemaji katika hadithi?
? Ni kielelezo cha utovu wa nidhamu miongoni wa wanafunzi. Anakunywa pombe na hata kujihusisha katika ufuska.
? Kupitia kwake uwajibikaji wa mwalimu Mosi unajitokeza. Kama mwalimu, alimkanya kunywa pombe na hata ufuska.
? Anaendeleza maudhui ya umaskini katika hadithi.
? Anakuza sifa za wahusika wengine kama vile Mwalimu Mosi.
? Ametumiwa kudhihirisha ukweli wa methali “asante ya punda ni mateke.”
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:34
- Huku ukirejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, fafanua namna ubadhirifu wa mali ya umma unavyoendelezwa.(Solved)
Huku ukirejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, fafanua namna ubadhirifu wa mali ya umma unavyoendelezwa.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza sifa na umuhimu wa Ngurumo katika tamthilia ya Kigogo.(Solved)
Eleza sifa na umuhimu wa Ngurumo katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza sifa na umuhimu wa Asiya katika tamthilia ya Kigogo.(Solved)
Eleza sifa na umuhimu wa Asiya katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza sifa na umuhimu wa Husda katika tamthilia ya Kigogo.(Solved)
Eleza sifa na umuhimu wa Husda katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza jinsi umaskini unavyoathiri wenyeji wa Sagamoyo katika tamthilia ya Kigogo.(Solved)
Eleza jinsi umaskini unavyoathiri wenyeji wa Sagamoyo katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua jinsi mbinu ya sadfa inavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo.(Solved)
Fafanua jinsi mbinu ya sadfa inavyojitokeza katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua sifa na umuhimu wa Kenga katika tamthilia ya Kigogo.(Solved)
Fafanua sifa na umuhimu wa Kenga katika tamthilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza jinsi methali zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.(Solved)
Eleza jinsi methali zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua nafasi/mchango wa vyombo vya habari katika jamii ya Sagamoyo ya tamdhilia ya Kigogo.(Solved)
Fafanua nafasi/mchango wa vyombo vya habari katika jamii ya Sagamoyo ya tamdhilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Utawala wa Majoka ni wa kidhalimu. Thibitisha ukweli huu katika tamdhilia ya Kigogo.(Solved)
Utawala wa Majoka ni wa kidhalimu. Thibitisha ukweli huu katika tamdhilia ya Kigogo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Bainisha matatizo ambayo Wanasagamoyo wanakumbana nayo katika upiganiaji wa haki katika eneo la Sagamoyo katika tamdhilia ya Sagamoyo.(Solved)
Bainisha matatizo ambayo Wanasagamoyo wanakumbana nayo katika upiganiaji wa haki katika eneo la Sagamoyo katika tamdhilia ya Sagamoyo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo)
(a) Eleza muktadha wa nukuu.
(b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu.
(c) Eleza sifa tatu za mnenewa.
(d) Kwa kifupi, fafanua...(Solved)
“Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo)
(a) Eleza muktadha wa nukuu.
(b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu.
(c) Eleza sifa tatu za mnenewa.
(d) Kwa kifupi, fafanua maudhui mawili yaliyodokezwa katika dondoo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
(b) Dondoo...(Solved)
“Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
(b) Dondoo hili linadokeza sifa gani ya mnenaji?
(c) Toa mifano miwili ya mbinu za lugha zilizotumika kifunguni.
(d) Linganisha mnenaji na mnenewa.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.(Solved)
Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)