Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa.

      

Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa.

  

Answers


Francis
? Mwanaume humposa mwanamke. Dadi alienda nyumbani kwa Kidawa kumposa.
? Mwanamke ndiye huamua wakati wa kuolewa na nani wa kumwoa. Kidawa alimchagua Dadi baada ya muda mrefu.
? Ndoa huandamana na masharti. Dadi alipewa masharti na Kidawa ili akubali kuolewa naye.
? Wanandoa hufanya kazi pamoja ili kukidhi mahitaji ya nyumbani. Dadi anachuuza samaki na Kidawa ni metroni.
? Wanaume hawafurahi wake wao wanapotangamana na wanaume wengine. Kidawa anaposimama kuongea na wanaume, Dadi anaudhika sana.
? Wanandoa husaidiana kazi za nyumbani, Dadi anasaidia kidawa kazi za nyumbani kama vile kuosha vyombo na kufagia.
? Wanandoa wanapanga uzazi, Dadi na Kidawa wanapanga kuwa na mtoto mmoja pekee.
? Ndoa imekosa uaminifu. Dadi anashuku kuwa Kidawa ana mapenzi na mwalimu mkuu.
? Kiwango cha elimu si kikwazo katika ndoa. Kidawa anaolewa na Dadi licha ya kuwa ana kisomo cha juu kuliko Dadi.
? Mwanamke amekengeuka. Kidawa anapenda fasheni.
? Kuna makubaliano ya kufanya mambo kwa pamoja.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:58


Next: “Ningeondoka ... mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.” (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa maneno haya. (b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza katika dondoo. (c)...
Previous: Kwa kurejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions