Kwa kurejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza.

      

Kwa kurejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza.

  

Answers


Francis
? Mzee Mambo hafanyi kazi wizarani ilhali analipwa mshahara mkubwa kuliko Sasa na Mbura wanaofanya kazi wizarani.
? Mambo anatumia runinga ya taifa inayofaa kuufahamisha umma masuala ya taifa lao kwa maslahi yake. Anaitumia kupeperusha sherehe nyumbani kwake.
? Mambo anaifilisi serikali kwa kutumia pesa za serikali kugharamia sherehe zake binafsi. DJ na wenzake wanalipwa pesa za serikali kwa kusimamia sherehe hii.
? DJ anaipunja serikali kwa kutumia mtaji wa bohari kuu ya dawa za serikali kufungua duka lake la dawa.
? DJ anaifilisi serikali kwa kupokea huduma za maji, umeme na matibabu bure ilhali wananchi maskini wanazilipia.
? Wafanyakazi wa umma wanaibia serikali saa za kazi. Sasa na Mbura wanahudhuria sherehe zilizofanyika kwa Mambo siku nzima ilhali walipaswa kuwa kazini.
? Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa mfano, anayatumia kusomba maji, chakula, kuwaleta jamaa wa Mambo shereheni na mapambo.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 09:59


Next: Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa.
Previous: Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (a) Mapenzi ya Kifaurongo (b) Masharti ya Kisasa (c) Mtihani wa Maisha (d) Ndoto ya Mashaka

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions