Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (a) Mapenzi ya Kifaurongo (b) Masharti ya Kisasa (c) Mtihani wa Maisha (d) Ndoto ya Mashaka

      

Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza.
(a) Mapenzi ya Kifaurongo
(b) Masharti ya Kisasa
(c) Mtihani wa Maisha
(d) Ndoto ya Mashaka

  

Answers


Francis
(a) Mapenzi ya Kifaurongo
? Ndoa iliyotarajiwa ya Dennis na Penina ilitawaliwa na unafiki. Penina anamjia Dennis na wazo la kuwa wapenzi bila kuzingatia hali duni ya familia yake. Dennis anapokosa ajira Penina anamfukuza.
? Inatawaliwa na kuhimiliana.
? Imetawaliwa na kukata tamaa - Penina anakata tamaa baada ya Dennis kukosa kazi.
? Imezingirwa na utabaka wa kiasili.
? Mapenzi hukua, huugua na hufa.

(b) Masharti ya Kisasa
Ndoa ya Dadi na Kidawa
? Ndoa inayodhibitiwa na masharti
? Ndoa ya kugawana majukumu
? Ndoa ya kupanga uzazi
? Ndoa inayoruhusu mwanamke kufanya kazi. Kidawa anafanya kazi ya umetroni usiku na kuuza bidhaa mtaani.
? Baadhi ya watu huingilia ndoa za wenzao kama njia ya kuona mapenzi yamevunjika baina ya wanandoa husika.

(c) Mtihani wa Maisha
? Wazazi wa Samueli ni wenye mapenzi - wanaonyesha mapenzi kwa mtoto huyu wao kwa kumpeleka shuleni akajipatie elimu.
? Samueli anaonyesha mapenzi kwa Nina. Kwa muda amekuwa mpenziwe.
? Nina anaamini kuwa mwanaume huyu ni bingwa kutokana na kudanganywa alikodanganywa na Samueli.
? Mamake Samueli ana mapenzi ya dhati kwake, baada ya Samueli kujaribu kujitoa uhai mamake anamsihi waende nyumbani.

(d) Ndoto ya Mashaka
? Tatizo la kwanza ni ndoa ya kulazimishwa. Mashaka na Waridi walitoka kwenye matabaka mawili tofauti. Waridi - tabaka la kitajiri naye Mashaka - tabaka la maskini.
? Kuna kutohusisha wanawake katika ndoa. Mamake Waridi hakuhusishwa katika harusi.
? Ndoa inakumbwa na tatizo la malezi bora - upendo, kujikubali, taasubi ya kiume.
? Kuna changamoto zinazojitokeza baada ya kifo cha mmoja. Mashaka anaachwa yatima.
? Kuna utengano katika ndoa. Waridi anatengana na mumewe kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 10:15


Next: Kwa kurejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza.
Previous: Kwa mujibu wa hadithi Mame Bakari, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions