Kwa mujibu wa hadithi Mame Bakari, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.

      

Kwa mujibu wa hadithi Mame Bakari, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.

  

Answers


Francis
? Tukio la Sara kubakwa linampotezea fahamu na anaaibika sana anapozinduka.
? Mwanamke kujeruhiwa – baada ya Sara kubakwa na janadume lile, anaharibiwa na kuvuja damu.
? Mwanamke kuvunjiwa ujanajike na utu wake.
? Maisha ya mwanamke kuingiliwa na kuharibiwa.
? Masomo yake yanakatizwa – mwalimu mkuu alimkabidhi Sara barua ya kumfukuza shuleni.
? Mwalimu mkuu hamsikilizi wala kumhurumia – badala yake aliongoza kumkejeli na kumweleza ile haikuwa shule ya wazazi bali wa wasichana. Anasema hawafundishi wanawake hapo.
? Mwanamke anateseka kiakili/kisaikolojia – Sara anaingiwa na mawazo mengi jinsi atakavyoukabili ule ujauzito. Anafikiria hata kuitoa ile mimba, kuhama kwao na hata kujiua.
? Mwanamke katika umri mdogo anabebeshwa mimba jinsi Sara alivyofanysihwa. Mzigo huo ungekuwa na changamoto nyingi kutokana na umri wake mdogo.
? Kuogopa kutoa taarifa ya kubakwa kwa wazazi kwa sababu wazazi hawangemwamini.
? Kila mara mwanamke anapobakwa, anayelaumiwa ni mwanamke na hata huonwa kama shetani.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:14


Next: Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (a) Mapenzi ya Kifaurongo (b) Masharti ya Kisasa (c) Mtihani wa Maisha (d) Ndoto ya Mashaka
Previous: “... mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi Masharti ya Kisasa.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions