Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“... mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi Masharti ya Kisasa.

      

“... mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi Masharti ya Kisasa.

  

Answers


Francis
? Dadi ndiye mchuma riziki - yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kuilisha jamaa yake. Pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya mpya na mapambo.
? Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.
? Kidawa hakubali kuwa mwanamume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya kazi za ndani ni hisani tu.
? Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui.
? Dadi anaosha nyumba, kufagia, kufua na hata kupiga nguo pasi.
? Wanandoa kujiwekea masharti ya uzazi. Wanahiari kumzaa mtoto mmoja tu kutokana na athari za usasa.
? Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja. Kila mara mkewe anapofanya hivyo, anaumia sana. Anaiona hiyo kama fursa ya mkewe kuhusiana na wanaume wengine.
? Dadi anaona ugumu wa masharti ya mkewe katika maisha ya ndoa lakini anashindwa kumweleza.
? Licha ya kuwa Dadi aliona ugumu wa kuzingatia masharti aliyowekewa na mkewe, asingeyavunja. Angefanya hivyo ndoa yao ingevunjika na huko kungekuwa ni kumvunja yeye pia.
? Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu. Hali hiyo inampa wasiwasi sana hata anashindwa kula.
? Kila mara Dadi alitarajiwa kuwa baada ya kula angeviondoa vyombo mezani na hata kuvisafisha.
? Dadi anapoamua kuzua mpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu, anafumaniwa na watu akiwa amepanda paipu na anaanguka na kuumia vibaya sana jambo linalomshutua sana mkewe pamoja na mwalimu mkuu anayelazimika kumwitia ambulensi impeleke hospitalini.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:16


Next: Kwa mujibu wa hadithi Mame Bakari, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka.
Previous: ‘Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharau biu hubiuka.’ (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa maneno haya. (b) Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika muktadha huu. (c) Eleza wasifu...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions