Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

‘Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharau biu hubiuka.’ (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza muktadha wa maneno haya. (b) Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika muktadha huu. (c) Eleza wasifu...

      

‘Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharau biu hubiuka.’ (Shibe Inatumaliza)
(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
(b) Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika muktadha huu.
(c) Eleza wasifu wa mzungumzaji wa maneno haya.
(d) Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi hii.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa maneno haya.
? Haya ni maneno ya Samueli Matandiko
? Anajizungumzia
? Yuko ofisini mwa mwalimu mkuu
? Amekuja kuchukua matokeo ya mtihani

(b) Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika muktadha huu.
? Uzungumzi nafsi - Samueli anajizungumzia
? Kinaya - Samueli ndiye aliyeaibika wala si mwalimu
? Methali - mdharau biu hubiuka

(c) Eleza wasifu wa mzungumzaji wa maneno haya.
? Ni mwongo - alimdanganya Nina kuwa ni mwerevu shuleni.
? Hana matumaini - anataka kujiua.
? Hana bidii - anashindwa na masomo.

(d) Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi hii.
? Babake Samueli anauza mali yake ili asomeshe watoto.
? Babake Samueli anathamini elimu ya Samueli kuliko dada zake Mwajuma na Bilha.
? Samueli anatembea umbali wa kilomita sita ili kutafuta elimu.
? Samueli anaogopa kuzungumza na babake kuhusu matokeo yake.
? Mwalimu mkuu alimdharau Samueli kwa kumrushia matokeo yake.
? Samueli hakutaka kuonyesha matokeo yake kwa wenzake alipoanguka.
? Samueli hakutia bidii masomoni mwake kwani hata majibu yake si sahihi.
? Samueli alipoanguka mtihani wake alikosa matumaini na kutaka kujiua.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:18


Next: “... mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi Masharti ya Kisasa.
Previous: ‘Kusema kweli lakini hata mimi sikuwa na nadhari katika kumpenda msichana huyu ... Nilimpenda kufa! Lakini! Kwao bure tu!’ (Shibe Inatumaliza) (a) Eleza dondoo. (b) Taja mtindo...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions