“Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua mbinu tatu za...

      

“Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine)
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza madhila kumi yaliyompata ‘kabwela’.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
? Haya ni mawazo ya Dennis.
? Anamrejelea Shakila.
? Mahali - katika afisi ya Shirika la kuchapisha magazeti.
? Tukio - ni baada ya kumwona mamake Shakila (pandikizi la mama) akipita huku akisubiri kufanya mahojiano.

(b) Fafanua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
? Chuku - akanyagapo chini, ardhi inatetemeka.
? Taswira - picha ya ardhi ikitetemeka
? Nahau - kujitia hamnazo

(c) Eleza madhila kumi yaliyompata ‘kabwela’.
? Anakosa kazi katika shirika la magazeti
? Kuachwa na Penina
? Kukejeliwa na Daktari Mabonga
? Hapewi pesa za masurufu na wazazi
? Kushindwa kujibu maswali wakati wa mahojiano – anaaibika
? Njaa – anaamua kupika uji
? Hana nguo za kisasa/ simu/tarakilishi n.k.
? Anasumbuka kiakili kwa sababu ya hali /asili/umaskini
? Kufukuzwa na Penina
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:25


Next: “... mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi Masharti ya Kisasa.
Previous: Kwa kurejelea hadithi za Mapenzi ya Kifaurongo na Shogake Dada ana Ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana. (a) Mapenzi ya Kifaurongo (b) Shogake Dada ana Ndevu

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions