Kwa kurejelea hadithi za Mapenzi ya Kifaurongo na Shogake Dada ana Ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana. (a) Mapenzi ya Kifaurongo (b) Shogake Dada ana Ndevu

      

Kwa kurejelea hadithi za Mapenzi ya Kifaurongo na Shogake Dada ana Ndevu fafanua changamoto zinazowakumba vijana.
(a) Mapenzi ya Kifaurongo
(b) Shogake Dada ana Ndevu

  

Answers


Francis
(a) Mapenzi ya Kifaurongo
? Dennis na wanafunzi wengine wanakaliwa na ugumu wa masomo katika chuo kikuu.
? Umaskini unatatiza masomo na mapenzi ya Dennis Machora.
? Utabaka baina ya wanafunzi chuoni.
? Ukosefu wa ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu k.m Dennis na Penina.
? Mapuuza ya wahadhiri k.m Dkt. Mabonga.
? Migogoro ya mapenzi - rafiki wa kwanza wa Penina wanatengana na pia tunamwona Penina wakitengana na Dennis.
? Kutamauka - masomo chuoni yanakuwa magumu kiasi kwamba wanafunzi wanaamua kufanya kazi za matatu na kukusanya kodi.
? Kuna mapenzi ya kiholela miongoni mwa wanafunzi wa chuo kikuu, walitembea wakishikana mabega.
? Shinikizo la rika – Dennis alitamani kuvaa kama wenzake na vile vile kuwa na vifaa vya kielektroniki kama vya wenzake.

(b) Shogake Dada ana Ndevu
? Mapenzi miongoni mwa wanafunzi yanaathiri masomo yao.
? Mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi k.m Safia.
? Kuna uavyaji wa mimba k.m Safia.
? Mauti- kifo cha Safia.
? Unafiki wa kidini k.m Safia na Kimwana.
? Mapuuza ya wazazi yanapelekea watoto wao kupotoka kimaadili.
? Kuna udanganyifu wa vijana kwa wazazi wao k.m Safia kumdanganya mamake.
? Kuna utovu wa maadili miongoni mwa vijana k.m inadaiwa Mkadi alikuwa na vitendo viovu.
? Vijana wanapata changamoto katika maandalizi ya mtihani wa mwisho ndiposa Safia na Kimwana wanaungana kudurusu pamoja.
? Kutokuwepo kwa mawasiliano baina ya wazazi na watoto wao kunawakosesha maelekezi mema.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 11:31


Next: “Akanyangapo chini ardhi inatetemeka...Amejitia hamnazo. Kabwela kama mimi nina faida gani? (Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua mbinu tatu za...
Previous: “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza.” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii katika Hadithi za Tumbo Lisiloshiba.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions