- Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
WASAKATONGE
1. Wasakatonge na juakali
Wabeba zege ya maroshani,
Ni msukuma mikokoteni,
Pia makuli bandarini,
Ni wachimbaji wa migodini,
Lakini...(Solved)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
WASAKATONGE
1. Wasakatonge na juakali
Wabeba zege ya maroshani,
Ni msukuma mikokoteni,
Pia makuli bandarini,
Ni wachimbaji wa migodini,
Lakini maisha yao chini
2. Juakali na wasakatonge
Wao ni manamba mashambani,
Ni wachapa kazi viwandani,
Mayaya na madobi wa nyumbani,
Ni matopasi wa majaani,
Lakini bado ni masikini.
3. Wasakatonge na juakali
Wao huweka serikalini,
Wanasiasa madarakani,
Dola ikawa mikononi,
Wachaguliwa na ikuluni,
Lakini wachaguaji duni
4. Juakali na wasakatonge
Wao ni wengi ulimwenguni,
Tabaka lisilo ahueni.
Siku zote wako matesoni,
Ziada ya pato hawaoni,
Lakini watakomboka lini?
(Mohammed Seif Khatib)
(a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua rai hii kwa kutoa mifano minne.
(b) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na uonyeshe mifano miwili ya jinsi iiivyotumika.
(c) Eleza umbo la shairi hili.
(d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari.
(e) Onyesha mifano miwili ya maadiii yanayojitokeza katika shairi hili.
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Manamba
(ii) Tabaka lisilo ahueni
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:
Kila Mchimba Kisima
Musa Mzenga
1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,
Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia,
Kalmia yenye upendo, kufurahisha...(Solved)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:
Kila Mchimba Kisima
Musa Mzenga
1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima,
Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia,
Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama,
Ya kukupa kila tija, na ushindi wa daima,
Upate njema daraja, duniani na kiyama,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
3. Utendapo la miuja, tendo ni yako nakama
Ya kukutia harija, hasara kukuandama,
Usione afuwaja, mwanza ajue heshima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe
4. Nakwambia uelewe, pulika ninayosema,
Si ari ya mwenginewe, kumuonya kwa lazima,
Mtu hufunza mwanawe, Kwanza ajue heshima,
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
5. Nisipokwambia wewe, kukufunza kila jema,
Kusudi nikuongowe, uepukwe na tujuma,
Matusi ndimi nipawe, ila na kila lawama,
Kila mchimba kisima, bundi hungia mwenyewe
6. Hii si heri ujuwe, matusi kuigandama,
Hadhi usiniuzuwe, hamithilishwa na nyama,
Fikiri moyo utuwe, nikupapo taaluma
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
7. shika tena utambuwe, wasia huu ni mwema
Matendo usipunguwe, mazuri kutenda hima,
Yatende ubarikiwe, upawe na taadhima
Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe.
8. Yakupasa uchunguwe, kila jambo kulipima
Upime ufafanuwe, mambo yote kwa alama
La kuwaka ulijuwe, pia lipi la kuzima,
Kila mchimba kisima hungia mwenyewe.
a) Eleza maudhui ya shairi hili.
b) Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na utoe mifano.
c) Eleza umuhimu wa kipokeo kinachotumiwa katika shairi hili
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa...(Solved)
Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!
Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa
Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.
Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotoshelezaIsipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
Viulize: Ni nani huyo ni nani!
Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
Viulize: Ni nani huyo nani1
Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”
a) Eleza dhamira ya shairi hili.
b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi
c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya kimuundo mshairi
d) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu vibarua.
e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari
f) Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Dhamiri yangu
Dhamiri imenifunga shingoni.
Nami kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
Na nimekwishachora duara.
Majani niwezayo kufikia yote nimekula.
Ninaona...(Solved)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.
Dhamiri yangu
Dhamiri imenifunga shingoni.
Nami kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
Na nimekwishachora duara.
Majani niwezayo kufikia yote nimekula.
Ninaona majani mengi mbele yangu
Lakini siwezi kuyafikia: kamba, kamba.
Oh! Nimefungwa kama mbwa.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Kuifikia na hapa nilipofungwa
Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.
Kamba isiyoonekana haikatiki.
Nami sasa sitaki ikatike, maana,
Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba
Aliharibu na mbwa aliuma watu.
Ninamshukuru aliyenifunga hapa
Lakini lazima nitamke kwa nguvu
“Hapa nilipo sina uhuru!”
(E. Kezilahabi)
(a) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia.
(b) Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru?
(c) Eleza rnaana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. “Kamba isiyoonekana haikatiki.”
(d) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hili.
(e) Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza katika shairi hili.
(f) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- HAKI
1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,
Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu,
Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu,
Tutokwe na utu!
2. Hatutakufanya, mwana kwa...(Solved)
HAKI
1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu,
Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu,
Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu,
Tutokwe na utu!
2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele; aliyemzaa,
Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
Haki twashangaa!
3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu,
Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu,
Usifanyekatu!
4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza,
Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza,
Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,
Kambi yatuviza!
5. Haki buna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,
Tukiifatia, hatufiki mbali, wengi tunaganda,
Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,
Haki yatuponza!
6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika,
Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika,
Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika,
Kwetu nimashaka!
7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa,
Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,
Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,
Nandio ya sasa!
8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,
Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,
Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,
Haki wauliwa!
9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,
Hatuna ashiki,kuvutalahaja,haki ituvae,
Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,
Haki tamati!
(Suleiman A. Ali) Malenga Wapya
(a) Eleza dhamira ya shairi hili.
(b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili.
(c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili.
(d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi katika shairi hili.
(e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari.
(f) Mshairi ana maana gani kwa kusema:
(i) Kambi yatuviza
(ii) Kuweza tukisi.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
-
(a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani?
(b) Shairi hili ni la aina gani? Toa...(Solved)
(a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani?
(b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja.
(c) Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili kujitegemea.
(d) Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake.
(e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari.
(f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi:
(i) Ghaibu
(ii) Tukamshabihi.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
1. Huno wakati mufti, vijana nawausia,
Msije juta laity, mkamba sikuwambia,
Si hayatti si mamati, vijana hino dunia,
Uonapo vyang’aria,...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
1. Huno wakati mufti, vijana nawausia,
Msije juta laity, mkamba sikuwambia,
Si hayatti si mamati, vijana hino dunia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
2. Japo aula kushufu, na machoni vyavutia,
Dunia wana dhaifu, waugua nisikia,
Vijana nawasarifu, falau mkisikia,
Ukiona vyang’aria, tahadhari vitakula.
3. Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria,
Msije andama baa, makaa kujipalia,
Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
4. Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia,
Wajimwaie uturin na mapoda kumichia,
Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
5. Wawapi leo madume, anasa walopapia?
Wamepita ja umeme, leo yao sitoria,
Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
6. Nambie faida gani, nambie ipi fidi?
Upatayo hatimani, waja wakikufukia,
Ilakufa kama nyani, kasoroyako mkia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
7. Kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia,
Ujifanye kama kwamba, u jiwe huna hisia,
Wakwambe watalokwamba, kwa lolote vumilia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
8. Vyatiririka tiriri, vina vyanikubalia,
Alo bora mshairi,pa tamu humalizia,
Nahitimisha shairi, dua ninawapigia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
9. Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia,
Wakinge wanarika, na anasa za dunia,
Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
(Mwalaa M.Nyanje)
(a) Eleza ujumbe wa shairi hili.
(b) Fafanua kwa kutoa mifano, mbinu nne alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili.
(c) Nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili inasema na pande mbili. Zieleze pande hizo.
(d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
(e) Bainisha toni ya shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana,
Kiwa ni riziki yangu,...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana,
Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona,
Ni wakati utanena.
Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipazao nao,
Wapitao wakiimba, eti mimi, ningapenda hali zao,
Haupandiki mgomba, wana nyemi, fisadi wa hadhi zao,
Eti ni kwa raha zao.
Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa,
Ni mtu kuwa hawara, wa vitimbi, ama alozawa tasa?
Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa,
Waama sina makosa
Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo,
Muwaite watribu, kina Siti, watuzwa ilimu hiyo,
Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo,
Kwalo sichafuki moyo
Hidhuru yote ni bure, sio kitu, kudhiki asodhikika,
Siwi nikaona ghere, lailatu, nyota njema itafika,
Kwa shangwe na njerejere, kila mtu, mdomo utafumuka,
Akiri amejibika.
(Mwalaa M. Nyanje)
(a) Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa.
(b) Fafanua mambo matano ambayo mzungumzaji (nafsineni) anapinga katika shairi hili.
(c) Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili.
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(e) Eleza muundo wa shairi hili.
(f) Bainisha matumizi mawili ya tafsida katika shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Watafuta Riziki
1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula washakiki, visipungue vinyuani.
2. Watafuta riziki, wahaingaikao...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Watafuta Riziki
1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula washakiki, visipungue vinyuani.
2. Watafuta riziki, wahaingaikao mijini
Kutwa kile na hiki, kama watanga na mipini
Japo hawasikii, hawakosi kujiamini
3. Watafuta riziki, wazalendo wa nchi hii
Kamwe hawajidhiki, tama za moyo kutii
Bali huafiki, kupingana na ulaghai
4. Watafuta riziki, pato ambalo la halali
Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali
Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali
(a) Fafanua sifa tano za watu wanaozungumziwa katika shairi hili.
(b) Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili.
(c) Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi.
(d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
(i) idadi ya mishororo katika beti.
(ii) mpangilio wa vina
(iii) mpangilio wa maneno
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza
1 Ngakua na mato, ya kuonea
Ngalisana kito,cha kuchezea
Kilicho kizito, cha kuelea
Kikamuenea,...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza
1 Ngakua na mato, ya kuonea
Ngalisana kito,cha kuchezea
Kilicho kizito, cha kuelea
Kikamuenea, akivae.
2 Makusudi yangu,ngaliandaa
Ngafinyanga chungu, cha mduwaa
Ngatia vitangu,vinavong’aa
Ili ziwe taa, kwa apikae.
3 Mkungu wa tano, wa mduwara
Ulo bora mno, kisha imara
Ulo na maono, kuwa ni dira
Kwenye barabara, itindiae.
4 Ngaomba Baraka, kwake Rabana
Punje za nafaka, kila aina
Chunguni kuweka, kwa kulingana
Hajaangu suna, yule alae.
5 Ngafanya bidii, kwenda mwituni
Sio kutalii, kukata kuni
Ya miti mitii, huko jikoni
Isio na kani,ni iwakae.
6 Kwa yangu mabega, nikathubutu
Ngabeba mafiga, yalo matatu
Bila hata woga, kwenye misitu
Simba tembo chatu, sinitishie.
7 Miti yenye pindi,na jema umbo
Ngajenga ulindi, mwema wimbombo
Fundi aso fundi, penye kiwambo
Moyo wenye tambo, apekechae.
8 Singaajiri, ngachimba mimi
Kisima kizuri, cha chemchemi
Maji ya fahari, ya uzizimi
Jua la ukami, siyaishae
9 Tamati nafunga, kwa kuishia
Mato ndo malenga, kanikimbia
Nahofu kutunga, mabeti mia
Asije chukia, ayasomae.
(a) Eleza ujumbe wa shairi hili.
(b) Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi aliotumia mshairi.
(c) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Fafanua aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili.
(f) Bainisha nafsi neni katika shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.
Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.
Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.
Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.
a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
c) Eleza toni ya shairi hili.
d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili?
e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande.
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi za maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa,kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha …
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
(T. Arege)
Maswali
a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.
c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.
d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:
i. tashhisi
ii. kinaya
iii. tashbihi
f) Eleza toni ya shairi hili.
g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
h) Changanua muundo wa shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka.”
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka
Jambo moja nakukumbukia: Mungu
Je, nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(a) Eleza toni ya shairi hili.
(b) Tambua nafsineni katika shairi hili.
(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu?
(d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka.
(e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
(f) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami...(Solved)
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa
Mwasema sayansini, siku ningalitosa
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika
Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana
Kukua imeridhia, msamiati kufana
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.
Maswali
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu
(b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
(f) Bainisha nafsineni katika shairi.
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
i. nasongwa
ii. kuriaria
iii. adinasi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)
Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
(Abdalla Said Kizere)
Maswali
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
d) Eleza umbo la shairi hili.
e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)
Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)
Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)
Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)
Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)