Hakiki umuhimu na idhini mbalimbali za utunzi wa mashairi.

      

Hakiki umuhimu na idhini mbalimbali za utunzi wa mashairi.

  

Answers


Francis
Utunzi wa mashairi huhitaji ubunifu wa hali ya juu. Hali hii hupelekea wakati mwingine watunzi kuenda kinyume na kaida za matumizi ya lugha kimaksudi. Jambo hili huibua dhana ya uhuru wa kishairi. Uhuru wa kishairi ni idhini au ruhusa ya mshairi kutunga shairi kwa namna fulani bila kuzingatia kanuni za kisarufi. Uhuru wa kishairi huhusisha yafuatayo:
? Mazida – uhuru huu humruhusu mtunzi kuyarefusha maneno fulani. Mazida husaidia kuleta utoshelezo wa idadi ya mizani katika kipande au mshororo.
? Inkisari – huu ni uhuru wa mshairi kuyafupisha maneno fulani. Kama ilivyo katika mazida, inkisari husaidia kutosheleza idadi ya mizani katika kipande cha mshororo.
? Tabdila – ni uhuru wa mshairi kubadilisha herufi au hata sauti ya neno bila kubadili maana ya neno hilo. Kwa mfano daraza badala ya darasa. Tabdila husaidia kuleta urari wa vina katika kipande cha mshororo.
? Kuboronga/kufinyanga/kubananga sarufi – pia huitwa miundo ngeu/ukiushi wa kisintaksia/ukiushi wa kimiundo. Huu ni uhuru wa mshairi kutofuata kanuni zinazotawala sarufi. Kusudi la kufanya hivi ni kuleta urari wa vina katika mishororo. Kwa mfano, kunapopambazuka kila, amka mwanadamu badala ya kila kunapopambazuka, mwanadamu amka
? Kikale – ni matumizi ya msamiati wa kale, kwa mfano, nyuni badala ya ndege, mgunda badala ya shamba n.k
? Vilugha/vilahaja – ni matumizi ya msamiati wa lahaja za Kiswahili badala ya Kiswahili sanifu.
? Utohozi – kutohoa ni kuswahilisha msamiati wa lugha nyingine na kuwa Kiswahili. Kwa mfano, skuli badala ya school, eropleni badala ya aeroplane.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 12:32


Next: Jadili aina mbalimbali za kinaya.
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Ajabu hino ajabu, dunia rangi rangile Naomba mie jawabu, wenzangu mniambile Ila pasi hilo jibu, nachukizwa Mteule Thamani ya mwanamke, haipo katika...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions