Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata. Ajabu hino ajabu, dunia rangi rangile Naomba mie jawabu, wenzangu mniambile Ila pasi hilo jibu, nachukizwa Mteule Thamani ya mwanamke, haipo katika...

      

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ajabu hino ajabu, dunia rangi rangile
Naomba mie jawabu, wenzangu mniambile
Ila pasi hilo jibu, nachukizwa Mteule
Thamani ya mwanamke, haipo katika ngozi!

Mweupe au mweusi, malenga nasisitiza
Awe atoka Urusi, au bara lenye giza
Wapewe wote nafasi, pasi yeyote kusaza
Thamani ya mwanamke, ni zaidi yake ngozi!

Hujafa hujaumbika, msemo wao wahenga
Hilo muweze kumbuka, lisije wapiga chenga
Ubaguzi si mwafaka, tuungane kuupinga
Thamani ya mwanamke, siyo rangi yake ngozi!

Nudhumu naweka tuo, nne beti nimefika
Maadili nd'o ufunguo, na thamani Afrika
Kitwa hadi fumbatio, hamna 'lokamilika
Thamani ya mwanamke, ni zaidi yake ngozi!
(D. W. Lutomia: Malenga Mteule)

Maswali
(a) Pendekeza anwani mwafaka kwa shairi hili.
(b) Hili ni shairi la aina gani? Eleza.
(c) Fafanua bahari zozote mbili zinazojitokeza katika shairi hili.
(d) Taja maudhui yanayoelezwa katika shairi.
(e) Bainisha toni ya shairi hili.
(f) Tambua nafsineni na nafsinenewa wa shairi.
(g) Onyesha aina za urudiaji katika shairi hili.
(h) Fafanua umbo la shairi hili.

  

Answers


Francis
(a) Pendekeza anwani mwafaka kwa shairi hili.
? Thamani ya mwanamke

(b) Hili ni shairi la aina gani? Eleza.
? Tarbia – lina mishororo minne katika kila ubeti.

(c) Fafanua bahari zozote mbili zinazojitokeza katika shairi hili.
? Mathnawi – lina vipande viwili yaani ukwapi na utao.
? Ukaraguni – vina vinabadilikabadilika katika beti zote.
? Tarbia – lina mishororo minne

(d) Taja maudhui yanayoelezwa katika shairi.
? Ubaguzi wa rangi

(e) Bainisha toni ya shairi hili.
? Toni ya kukashifu – mshairi anakashifu ubaguzi wa wanawake kwa misingi ya rangi ya ngozi.

(f) Tambua nafsineni na nafsinenewa wa shairi.
? Nafsineni – Mteule (mshairi ametaja jina lake katika ubeti wa kwanza). Pia anaweza akawa mtetezi wa haki za wanawake.
? Nafsinenewa – wabaguzi wa rangi.

(g) Onyesha aina za urudiaji katika shairi hili.
? Urudiaji wa neno – ngozi
? Usambamba – thamani ya mwanamke

(h) Fafanua umbo la shairi hili.
? Lina beti nne
? Vipande viwili katika kila mshororo (ukwapi na utao)
? Mishororo minne katika kila ubeti
? Mizani 8,8
? Vina vinabadilika katika beti zote
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 12:37


Next: Hakiki umuhimu na idhini mbalimbali za utunzi wa mashairi.
Previous: Define the term acquisition

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions