Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

"Rununu (simutamba) imeleta athari mbaya katika jamii." Jadili

      

"Rununu (simutamba) imeleta athari mbaya katika jamii." Jadili

  

Answers


john
Hii ni insha ya mjadala. Ifuate kanuni za mjadala ambapo patakuwa na hoja za kuunga mkono na za kupinga.

Kuunga mkono

Hatari za kuangamia kwa lugha ambazo hazitumiki kwa wingi katika mawasiliano ya simu tamba
Kupalilia uraibu wa matumizi ya rununu, vijana kujizika katika matumizi ya rununu kiasi cha kufifilisha utendaji wao kielimu
-Kuchipuka na kustawi kwa aina mpya na nyeti za uhalifu kama vile utapeli -Kuporomoka kwa misingi ya familia, ikiwa mume/mke atamdhibiti mwenzake kwa kutaka kusoma ujumbe wake mfupi au kuchunguza nani wanaompigia mwenzake simu, mtafaruku unaweza kuzuka. Pia jamaa nyingi huhiari kupigania simu badala ya kuonana ana kwa ana, hivyo kupujua mshikamano wa kifamilia -Kuvuruga lugha/sarufi. Watu wamezoea kuandika kwa ufupi.
-Kudanganya katika mtihani, hivyo kupujua thamani ya mitihani. Kuzorota kwa maadili, k.v kuharibia mtu sifa kupitia 'facebook',kudanganya moja kwa moja pale ulipo n.k.
-Kudhalilisha ubunifu/wizi wa kiusomi. Baadhi ya watu hutumia simu kuiba mawazo ya

wengine.
-Wizi wa ubunifu wa kazi za kisanii ambazo hazijapewa hakimiliki -Kurahisisha uporaji na unyakuzi wa malighafi za mataifa yanayoendelea kupitia kwa mtandao
-Upujufu wa maadili, vijana kutazama filamu chafu.

Hoja za kupinga

Rununu zina manufaa chungu nzima kama vile: (

-Kuleta wanadamu pamoja duniani na hivyo kupunguza tuhuma zinazoelekea kuleta vurugu kwa watu kutofahamiana
-Usambazaji wa teknolojia inayorahisisha maisha ya wanadamu kote duniani kupitia kwa huduma zinazotolewa na simu.
-Kuendeleza biashara - kubadilishana bidhaa na pesa kupitia mtandao kama vile MPESA.
Hurahisisha huduma za benki. Mtu anaweza kufikia akaunti yake kupitia kwenye rununu.
Huwa na vifaa kama vile vikokotoo vya kurahisisha kufanya hesabu.
-Ni chombo cha burudani - vijana hupata michezo mbalimbali. -Huimarisha utafiti. Mtu anaweza kufanya utafiti kupitia kwenye rununu. -Huweza kutumiwa kupigia picha, hivyo kuokoa pesa ambazo zingenunulia kamera au video.
-Mtu anaweza kuwasiliana na familia yake kutoka mbali, hivyo kuokoa muda na fedha ambazo angetumia kusafiri.
- Mtu anaweza kuhifadhi msahafu(Biblia au Korani) kwenye simu, hivyo kujikuza kiroho kila mara.
-Ni njia ya kupata habari kutoka kwenye mashirika ya usambazaji wa habari. Baadhi ya rununu zina redio na hata runinga. Mtu anaweza kusikiliza na kutazama habari hata akiwa safarini.
-Hufanikisha kuwanasa matapeli na magaidi. Baadhi ya rununu huonyesha simu ilipopigiwa hivyo kusaidia kudhibiti mitandao ya uhalifu.
-Huduma ya simu tamba ni njia ya kujipatia riziki. Wapo raia walioanzisha biashara ya MPESA, na wengine ukarabati wa rununu zilizoharibika. Hili limepunguza makali ya uhaba wa nafasi za kazi nchini
john3 answered the question on October 4, 2017 at 13:28


Next: State one function of the county governor in Kenya
Previous: Describe the political organization of the Mijikenda during the pre-colonial period.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions