Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Andika sentensi ifuatayo katika umoja; Hao wenyewe hawakuzingatia mafunzo ya lishe bora.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika umoja; Hao wenyewe hawakuzingatia mafunzo ya lishe bora.

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Tumia kirejeshi - O – tamati katika sentensi ifuatayo: Kijana ambaye anapendeza ni yule ambaye hutia bidii.(Solved)

    Tumia kirejeshi - O – tamati katika sentensi ifuatayo: Kijana ambaye anapendeza ni yule ambaye hutia bidii.

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Andika kwa ukubwa; Kiti kilichokuwa kimekaliwa na mwanamke kilivunjika.(Solved)

    Andika kwa ukubwa; Kiti kilichokuwa kimekaliwa na mwanamke kilivunjika.

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Bainisha aina za shamirisho katika sentensi: Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali(Solved)

    Bainisha aina za shamirisho katika sentensi: Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Tumia neno “kimya” katika sentensi kama: (i) Kielezi (ii) Kihisishi(Solved)

    Tumia neno “kimya” katika sentensi kama: (i) Kielezi (ii) Kihisishi

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Onyesha (i) Kielezi (ii) Kitenzi katika sentensi: Mvua ilinyesha mfululizo(Solved)

    Onyesha (i) Kielezi (ii) Kitenzi katika sentensi: Mvua ilinyesha mfululizo

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo: Katiba ambayo ilipingwa na wengi haitetei maslahi ya wananchi.(Solved)

    Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo: Katiba ambayo ilipingwa na wengi haitetei maslahi ya wananchi.

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti ili kuleta dhana tatu tofauti. Babu alimchapa nyanya(Solved)

    Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti ili kuleta dhana tatu tofauti. Babu alimchapa nyanya

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Tunga sentensi moja kudhihirisha maana tofauti ya maneno yafuatayo:(Solved)

    Tunga sentensi moja kudhihirisha maana tofauti ya maneno yafuatayo:

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Onyesha shadda katika neno lifuatalo: mlima(Solved)

    Onyesha shadda katika neno lifuatalo: mlima

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Ainisha mofimu zinazopatikana katika neno lifuatalo: Angemlia(Solved)

    Ainisha mofimu zinazopatikana katika neno lifuatalo: Angemlia

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Tunga sentensi ukitumia kielezi cha; Wakati(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kielezi cha; Wakati

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Tunga sentensi ukitumia kielezi cha; i) Mahali(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kielezi cha; i) Mahali

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Andika sauti mwambatano inayotamkiwa kwenye ufizi.(Solved)

    Andika sauti mwambatano inayotamkiwa kwenye ufizi.

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Huku ukitoa mfano mmoja mmoja taja makundi mawili ya sauti.(Solved)

    Huku ukitoa mfano mmoja mmoja taja makundi mawili ya sauti.

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Jambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Jambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hili. Hata hivyo, fanaka haijapatikana, wala haielekei kamwe itapatikana leo au karne nyingi baadaye. Yamkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “tena “wa kimataifa”. Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna wale watu binafsi na hasa viongozi wa nchi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa licha ya muwashtua wao. Kulingana na maoni ya watakaburi hao,ujambazi ni wa watu ‘washenzi’ wasiostaarabika, wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosababishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo maalum za ‘’ ulimwengu wa tatu” . Kulingana na wastaarabu wa nchi zilizoendelea, vinyangarika hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma. Baada ya kusagwa sagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa ardhini itakamilika. Imani ya watu ya kuwa ujambazi wa kimataifa, hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba tarehe 11 mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa katika majumba mawili ya fahari, yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako kwa kuwa, kabla ya siku hiyo, wamarekani hawangeweza kudhani kwamba ingewezekana taifa lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao. Taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe lolote la dunia. Hakuna ulimwenguni mzima, aliyeamini kuwa Marekani ingeweza kushambuliwa. Kwa ajili hiyo, mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima imeshambuliwa, wala sio Marekani pekee. Mintarafu hiyo, Marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani ilishangilia na kusheherekea. Kwa bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara – picha ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa. Ukizingatia aya tatu za mwisho, fafanua fikira za watu na mambo yote yaliyotokea baaada ya Septemba tarehe 11, 2001 (Maneno 65 -75)

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Watu wengine hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Watu wengine hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini. Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa kuwa waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaaa ya wateule waungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri, vitumbua na kadhalika na akina yahe hawangeweza kuigharamia. Watafiti wa maswali ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa haina virutubiushi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya aside mwilini yenye sumu inayoathiri siha. Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Kwanza, huchangia kuoza na kuharibika kwa meno pamoja na matatizo ya meno kuuma. Pili, sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Pia, sukari huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na ambao unatokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii ya kolestroli inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda moyo ukachoka na kukoma kufanya kazi. Madhara haya ya sukari ndiyo yanayowafanya watu wengi kukiri kuwa sukari, ingawa ni tamu, ni sumu mwilini. Wataalamu wa lishe wamependekesa ulaji wa vyakula ka nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia. Fauka ya hayo, sukari inayotoka katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamin, madini na amino aside. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Mathalani, asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo. Licha ya hayo, asali huuchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo husaidia watoto kukua vizuri. Huwezi kuzidisha kiwango cha hemoglobini, hivyo kupunguza uwezakano wa watoto kuwa na anaemia (upungufu wa damu). Halikadhalika, asali husaidia katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani. Asali pia inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumiwa kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing’are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikatika. Halikadhalika, asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo. a) Kutokana na taarifa hii, kwa nini wazee wa zamani waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko watu wa siku hizi? b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe. c) Onyesha madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini. d) Taja aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa mwanadamu au ueleze ni kwa nini. e) Eleza manufaa ya asali: i) Ndani ya mwili ii) Nje ya mwili f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa: i) Hamu na ghamu ii) Akina yahe iii) Sugu iv)Vipodozi

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (i)Makamasi (ii)Boga(Solved)

    Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (i)Makamasi (ii)Boga

    Date posted: October 12, 2017.  

  • Eleza matumizi mawili ya parandesi kama alama za uakifishaji.(Solved)

    Eleza matumizi mawili ya parandesi kama alama za uakifishaji.

    Date posted: October 11, 2017.  

  • Eleza thana ya nomino za pekee.(Solved)

    Eleza thana ya nomino za pekee.

    Date posted: October 11, 2017.  

  • Eleza matumizi matatu ya kikomo huku ukitolea mifano mwafaka.(Solved)

    Eleza matumizi matatu ya kikomo huku ukitolea mifano mwafaka.

    Date posted: October 11, 2017.  

  • Ni nini umuhimu wa kusanifisha lugha ya Kiswahili?(Solved)

    Ni nini umuhimu wa kusanifisha lugha ya Kiswahili?

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Usanifishaji wa lugha ni nini?(Solved)

    Usanifishaji wa lugha ni nini?

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Ala tuli ni nini?(Solved)

    Ala tuli ni nini?

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Kanusha sentensi hii kwa kutumia kiwakilisho amba (alama 2) Ubao upakwao rangi hupendeza(Solved)

    Kanusha sentensi hii kwa kutumia kiwakilisho amba (alama 2) Ubao upakwao rangi hupendeza

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Unda nomino mbili kutokana na neno hudumu(Solved)

    Unda nomino mbili kutokana na neno hudumu

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Tambua chagizo Ninaenda Nakuru lakini nitarudi saa moja(Solved)

    Tambua chagizo Ninaenda Nakuru lakini nitarudi saa moja

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Bainisha matumizi ya ‘ni’ katika sentensi ifuatayo: Twendeni tuone mhubiri ni nani?(Solved)

    Bainisha matumizi ya ‘ni’ katika sentensi ifuatayo: Twendeni tuone mhubiri ni nani?

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Kanusha Mwanafunzi hodari apongezwa na rais.(Solved)

    Kanusha Mwanafunzi hodari apongezwa na rais.

    Date posted: October 10, 2017.  

  • Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendama Habari za kifo chake zilifichwa(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendama Habari za kifo chake zilifichwa

    Date posted: October 10, 2017.