Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
- Toa visawe viwili vya ‘uchochole’ (Solved)
Toa visawe viwili vya ‘uchochole’
Date posted: October 29, 2019.
- Kanusha sentensi ifuatayo:
Aimbapo vizuri mtuze
(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo:
Aimbapo vizuri mtuze
Date posted: October 29, 2019.
- Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii
Mshikie mtoto.
(Solved)
Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii
Mshikie mtoto.
Date posted: October 29, 2019.
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa
Paka huyu aliguguna mfupa wa mtoto huyu. (Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa
Paka huyu aliguguna mfupa wa mtoto huyu.
Date posted: October 29, 2019.
- Tunga sentensi mbili kudhihirisha matumizi ya virai vifuatavyo na uvipigie mstari
a)Kirai Nomino
b)Kirai kivumishi (Solved)
Tunga sentensi mbili kudhihirisha matumizi ya virai vifuatavyo na uvipigie mstari
a)Kirai Nomino
b)Kirai kivumishi
Date posted: October 29, 2019.
- Tambua kiima na kiarifa katika sentensi hii(Solved)
Tambua kiima na kiarifa katika sentensi hii
Taa yake inatoa moshi mwingi
Date posted: October 29, 2019.
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutenda
Alikatwa mkono na jizi lile
(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kutenda
Alikatwa mkono na jizi lile
Date posted: October 29, 2019.
- Tunga sentensi ukitumia neno katika ngeli ya YA-YA. (Solved)
Tunga sentensi ukitumia neno katika ngeli ya YA-YA.
Date posted: October 29, 2019.
- Andika katika usemi halisi
Mwelekezi alimwambia Loisi kuwa safari yao ingekamilika siku iliyofuata.
(Solved)
Andika katika usemi halisi
Mwelekezi alimwambia Loisi kuwa safari yao ingekamilika siku iliyofuata.
Date posted: October 29, 2019.
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi .
Mtoto alipoumia alitibiwa haraka sana.
(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi .
Mtoto alipoumia alitibiwa haraka sana.
Date posted: October 29, 2019.
- Yakinisha katika nafsi ya pili wingi
sitakusomea kitabu hicho
(Solved)
Yakinisha katika nafsi ya pili wingi
sitakusomea kitabu hicho
Date posted: October 29, 2019.
- Bainisha shamirisho katika sentensi hii
Mpishi alikatiwa kuni kwa shoka na mpasua kuni.
(Solved)
Bainisha shamirisho katika sentensi hii
Mpishi alikatiwa kuni kwa shoka na mpasua kuni.
Date posted: October 29, 2019.
- Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo;
Kipasuo-kwamizo –
Irabu ya nyuma wastani - (Solved)
Taja mfano mmoja kwa kila aina ya sauti zifuatazo;
Kipasuo-kwamizo –
Irabu ya nyuma wastani -
Date posted: October 29, 2019.
- Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ukeketaji wa mwanamke ni hali ya kudhuru sehemu ya uzazi ya mwanmke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Barani Afrika, ukeketaji ni jinamizi ambalo licha ya kampeni za kulimaliza limekuwa ndumakuwili.
Sababu kadha wa kadha zimetolewa na wanaoendeleza uhalifu huu kutetea hatua yao. wengi wao wanadai kwamba lengo la zoezi hilo huwa ni kudhibiti hisi za kimapenzi za mwanamke. Hii ni kutokana na thamani ya ubikira kabla ya ndoa au haja ya kudhibiti huba la ibana katika ndoa, hali ambazo huwafanya wadai kuwa ukeketaji humpunguzia mwanamke hamu ya kufanya mapenzi.
Yapo pia masuala ya kiitikadi, kwamba ukeketaji ni kigezo kikuu cha kumwingiza msichana katika kundi la wanawake na kuamua majukumu ambayo mwanamke husika atapewa katika maisha ya baadaye na maisha ya ndoa. Wengine wao waniendeleza shughuli hii kwa misingi ya itikadi za kidini.
Mbali na visingizio – ni visingizio kwa kuwa havina mashiko – vinavyotolewa na jamii zinazoeendeleza uhalifu huu dhidi ya mwanamke, yapo madhara mengi san yanayotokana na kitendo cha kumkeketa mwanamke. Moja ni kwamba mhusika huweza kufariki kwa kupoteza damu nyingi au kupatwa na maumivu makali yanayoweza kuathii mfumo wake wa mwili. Aidha, anaweza kupatwa na ugonjwa wa anemia.
Mwathiriwa wa ukeketaji anaweza pia akakubwa na matatizo ya kwenda haja ndogo, hasa kwa kubana mkojo kwa kuogopa uchungu. Hali hii inaweza kusababisha maradhi katika kibofu na sehemu za kupitsha mkojo.
Pamoja na hayo, matumizi ya kijembe au kisu kichafu, tena kwa zaidi ya mtu mmoja katika mazingira machafu kunaweza kusababisha maambukizi ya maradhi mengine kama vile, virusi vinavyosababisha ukimwi au magonjwa mengine ya kuambukiza. Magonjwa kama hayo yanaweza pia kusababisha matatizo katika mfupa wa uzazi na baadaye kusababisha kusumishwa kwa damu. Hali hiyo ikikosa kupata tiba (isipokuwa ukimwi ambao hauna tiba), mhusika anaweza kuishia kufa.
Maswali
a)Fupisha kwa maneno 64 – 69 ujumbe wa aya tatu za kwanza
Matayarisho
Jibu
b)Kwa maneno 40 – 45, eleza madhara ya ukeketaji kwa wanawake.
Matayarisho
Jibu
Date posted: October 29, 2019.
- Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nilianza kusikia habari za ugonjwa wa ukimwi mnamo mwaka wa 1984. Wakati huo nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha sita na kujiunga ia chuo cha walimu kilichoko wilayani Nyeri kiitwacho Kagumo. Nilihofu sana maradhi hayo hasa nilipowaona walioambukizwa wakikondeana mthili ya ng’onda. Baada ya waathiriwa kufariki, jamaa zao hawakuruhusiwa kuwazika. Wizara ya afya ilitoa amri kali kuwa wale wore waliofariki kutokana na maradhi ya ukimwi wazikwe na kikundi maalum cha madaktari ma wauguzi wa hospitali za wilayani. Kulikuwa na kasisi mmoja tuliyehusiana kiukoo aliyefariki kutokana na maradhi ya ukimwi. Sisi hatukuruhusiwa hata kumsongea karibu marehemu alipoletwa nyumbani.
Madaktari na wauguzi walivalia majoho meupe ungedhani ni malaika. Mikononi walivaa glovu nyeupe ambazo zilitutisha machoni.
Mara nyingi nimeshangazwa na athari za ugonjwa huu. Inasemekana kuwa kuna njia kadha za usambazaji wa ugonjwa wa ukimwi. Njia moja ni kuhusika katika kitendo cha mapenzi na mtu ambaye ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo. Njia nyingine nimeelezwa kuwa ni kwa kutumia kwa pamoja vifaa vyenye makali na mtu aliyeambukizwa virusi vya ukimwi. Inasemekana kuwa kugusa damu ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo pia kunaweza kukutia mashakani.
Mama mja mzito aliyeambukizwa ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni anapojifungua na hati baadaye anapomnyonyesha mtoto wake mchanga. Kisha kuna kupokea damu kutoka kwa mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi hivyo. Yote hayo yanachangia pakubwa katika kututumbukiza kwenye janga hili la ukimwi.
Lakini nimewahi kusikia watu wakisema kuwa ukimwi si maradhi. Yaani ni
upungufu tu wa kinga ya kukabiliana na magoniwa katika mwili wa binadamu. Maadamu ukiweza kuimarisha kinga ya magonjwa katika mwili wako basi unaweza kuishi kwa miaka ma mikaka. Anachohitajika mtu ni apate chakula na lishe bora, afanye mazoezi ya kutosha, na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi na watu wenine ambao huenda wakamwambukiza aina tofauti tofauti za virusi vya ukimwi. Hayo yakifanyika mwathiriwa huwa na matumaini ya kuishi kwa muda mrefu kwani hatazidiwa na maradhi hayo na mwishowe kwenda jongomeo. Kuna haja kubwa ya kujilinda na kuepukana kabisa na janga hili lililotuzingira. Wengi tayari wameshapoteza roho zao. Wengine walioambukizwa wanaugua mahospitalini ma na majumbani mwao kisirisiri. Mungu atujalie heri na shari, kwani utafiti wote ambao umefanywa kuhusu tiba ya uwele huu haujafua dafu hata kidogo. Hata hivyo Mola hamtupi mja wake.
Maswali
a) Ipe habari hii anwani ifaayo.
b) Kwa nini mwandishi ana hofu sana ya maradhi ya ukimwi?
c)Hapo awali watu waliwachukulia vipi walioambukizwa maradhi ya Ukimwi?
d)Eleza njia mbalimbali zinazomfanya mtu kuambukizwa maradhi ya ukimwi .
e)Je, tunawezaje kuepukana na janga hili la ukimwi?
f)Eleza maana ya vifungu hivi vya maneno kama vilivyotumika katika taarifa.
i)Wauguzi
ii)Makali
iii)Virusi
iv)Uwele
v)Janga
Date posted: October 29, 2019.
- Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii.
i)Lugha ya taifa
(ii)Lugha ya ishara
(iii)Lugha mwiko
(iv)Sajili za lugha
(v)Uchanganyaji msimbo.(Solved)
Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii.
i)Lugha ya taifa
(ii)Lugha ya ishara
(iii)Lugha mwiko
(iv)Sajili za lugha
(v)Uchanganyaji msimbo.
Date posted: October 21, 2019.
- ISIMU JAMII
Ali: Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka!
Ebo: Mimi … ni … afande ni Ebo
Ali: Unatoka wapi sa ii? Hapa hakuna sheria?
Ebo:...(Solved)
ISIMU JAMII
Ali: Wee kuja hapa. Wewe ni nani? Sema haraka!
Ebo: Mimi … ni … afande ni Ebo
Ali: Unatoka wapi sa ii? Hapa hakuna sheria?
Ebo: Samahani mkubwa. Mimi niku…
Ali: Mkubwa wa nani? Wakubwa wako ofisini.
Ebo: Pole mzee.
Ali: Mzee gani? Hii mtu lazima niiwekwa store. Yaani self-contained.
Toa viatu.
Ebo: Tafadhali Bwana Askari, nilichelewa …
Ali: Mimi sitaki hadithi! Hizo pelekea nyanya yako, eh. Fanya haraka!
Ebo: Naomba mkubwa …
Ali: Hapa si kanisani. Unaomba! Hata …
Fafanua sifa tano za sajili hii.
Date posted: October 21, 2019.
- Eleza maana ya nomino.(Solved)
Eleza maana ya nomino.
Date posted: October 21, 2019.
- Eleza maana tatu zinazopatikana katika sentensi hii.
Alikuwa amenijuza kuwa angefika kwao.(Solved)
Eleza maana tatu zinazopatikana katika sentensi hii.
Alikuwa amenijuza kuwa angefika kwao.
Date posted: October 21, 2019.
- Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii.
Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi?(Solved)
Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii.
Kwa nini umeishi kwao kwa miaka mingi?
Date posted: October 21, 2019.
- Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kisha utunge sentensi katika ukubwa - wingi.(Solved)
Tumia kivumishi kionyeshi cha karibu pamoja na nomino katika ngeli ya I-ZI kisha utunge sentensi katika ukubwa - wingi.
Date posted: October 21, 2019.
- Onyesha aina tofauti za shamirisho katika sentensi hii.
Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake.
(Solved)
Onyesha aina tofauti za shamirisho katika sentensi hii.
Ali alimnunulia Asha viatu kwa pesa zake.
Date posted: October 21, 2019.
- Eleza dhana ya shamirisho.(Solved)
Eleza dhana ya shamirisho.
Date posted: October 21, 2019.
- Nyambua kitenzi ja katika kauli ya kutendewa kisha utunge sentensi.(Solved)
Nyambua kitenzi ja katika kauli ya kutendewa kisha utunge sentensi.
Date posted: October 21, 2019.
- Weka kirejeshi ‘O’ tamati kwenye kitenzi chunga kisha ukitungie sentensi.(Solved)
Weka kirejeshi ‘O’ tamati kwenye kitenzi chunga kisha ukitungie sentensi.
Date posted: October 21, 2019.
- Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya ‘na’ kama.
(i)Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda.
(ii)Kiunganishi(Solved)
Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya ‘na’ kama.
(i)Kihusishi cha ‘na’ ya mtenda.
(ii)Kiunganishi
Date posted: October 21, 2019.
- Tumia mzizi –w- katika sentensi kama:
(i)Kitenzi kisaidizi.
(ii)Kitenzi Kishirikishi.(Solved)
Tumia mzizi –w- katika sentensi kama:
(i)Kitenzi kisaidizi.
(ii)Kitenzi Kishirikishi.
Date posted: October 21, 2019.
- Sahihisha sentensi ifuatayo.
Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe.
(Solved)
Sahihisha sentensi ifuatayo.
Mtu ambaye aliyechukua kitabu chenye kilikuwa hapa arudishe.
Date posted: October 18, 2019.
- Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo kisha uelezee ni vya aina gani.
Ajapo tutamlaki kwa shangwe.(Solved)
Onyesha vishazi katika sentensi ifuatayo kisha uelezee ni vya aina gani.
Ajapo tutamlaki kwa shangwe.
Date posted: October 18, 2019.
- Andika kwa msemo wa taarifa:
Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa?
Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni jana.
(Solved)
Andika kwa msemo wa taarifa:
Askari: Ulikuwa unaelekea wapi uliposhambuliwa?
Jirani: Nilikuwa nikienda sokoni jana.
Date posted: October 18, 2019.