- Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana.(Solved)
Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali
Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hata miongoni mwa vijana. Ni kilugha ambacho kinakisiwa kuzuka katika miaka ya 60 na 70 katika makazi ya mashariki mwa jiji la Nairobi kama vile Kaloleni, Mbotela/ Bahati na kadhalika.Kwa sasa ni kilugha kilichoenea kwingi nchini Kenya na kuwa kitambulisho cha takriban vijana wengi. Wataalam mbalimbali wanabainisha nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha lugha hii. Kuna nadharia mbili kuu kuhusu asili ya lugha ya Sheng: kwamba kilugha hiki kiliibuka kutokana na wahuni na wakora jijini Nairobi ambao lengo lao Iilikuwa kuwasiliana kwa siri. Nadharia nyingine ni kuwa kilichipuka kutokana na vijana ambao walizua lugha ya kuwasiliana baada ya uhuru (kwa sababu walikichukia Kiswahili ambacho walikiona kama lugha ya uboi)
Dhana hizi kwa muda mrefu, zimeathiri mitazamo kuhusiana na kilugha hiki. Kwa sasa ni kilugha ambacho ,yjiasambaa katika sehemu mbalimbali za Kenya na watu wa matabaka mbalimbali wanakitumia. Kilugha hiki kimeanza kuashiria uhalisia mkubwa wa maisha ya kisasa, zaidi katika jamii ya Wakenya. Aidha, sheng imejitanzua kutoka hali ya kuwa kilugha cha maongezi pekee na sasa kinatumiwa katika baadhi ya vitabu, hata waandishi wa vitabu wameanza kukitumia. Kwa mfano, katika miaka ya 80, David Mailu katika kitabu chake 'Without Kiinua Mgongo' alitumia Sheng. Katika siku za hivi karibuni, riwaya ya 'Kidagaa Kimemwozea' iliyoandikwa na Ken Walibora kilugha cha sheng kimepewa nafasi kama kitambulisho cha vijana kupitia kwa mhusika DJ Bob.
Vilevile kumezuka vyombo vya habari kama redio, mfano idhaa ya Ghetto, redio ambayo inaendeleza mawasiliano kwa matumizi ya Sheng. Kuna vipindi vya matangazo ya kibiashara katika runinga ambayo yanaendelezwa kwa Sheng. Kwa mfano, katika 'gazeti la Taifa Leo, kuna ukumbi wa 'Mchongoano' ambao umekuwa ukiendelezwa kwa Sheng.
Nchini Kenya ambapo asilimia 60% ya idadi ni vijana, Sheng imetokea kuwatambulisha vijana. Katika enzi hii ya Teknohama. wanaomiliki vyombo vya habari na sekta nyingine za biashara wamegundua kuwa matumizi ya Sheng ndiyo njia mwafaka zaidi ya kulifikia soko kubwa la vijana kwa ajili ya kueneza matangazo ya bidhaa na huduma za kibiashara. Kwa hivyo, Sheng imekuwa daraja la kuwafikia na kuwavutia vijana.
Hata hivyo, kwa upande mwingine matumizi ya Sheng yamelaumiwa na walimu wengi katika shule za msingi na zile za upili kuwa ni sababu mojawapo kuu ya kushuka kwa matokeo ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza miongoni mwa wanafunzi. Sheng imelaumiwa kwamba inasababisha wanafunzi kutozingatia mafunzo ya kanuni za sarufi na tahajia au maendelezo. Wataalam wanadai kuwa ni msimbo ambao hauzingatii sheria za sarufi na tahajia kwa sababu zisizofahamika, kwani ingawa muundo wake wa kisarufi hushahabiana na ule wa Kiswahili, Sheng hupuuza sarufi ya Kiswahili katika matumizi yake.
Ingawa sheng imekuwa ikipigwa vita, kuna wataalam ambao wana mtazamo kwamba juhudi hizo haziwezi kufanikiwa kwani Sheng ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa vijana na kwa hivyo ina umuhimu wake ambao hauwezi kufumbiwa macho. Wanasema kuwa ni chombo ambacho kinafumbata hisia na mshikamano wa kizazi kipya kama ilivyojitokeza katika kauli mbiu ya mgombeaji urais mwaka wa 2012,'Tunawesmake.
Katika hali ambapo kiwango cha ubora wa matokeo ya Kiswahili yalidorora katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE) mwaka wa 2012 na kuwa asilimia 35.81 pekee yakilinganishwa na asilimia 48.82 ya mwaka 2011, Sheng imekuwa ikilaumiwa kuwa ndicho chanzo cha kudorora kwa viwango vya ubora wa matokeo. Baadhi ya hao wataalamu wanasema kwamba Sheng haipaswi kuhujumiwa. kinachohitajika kufanywa ni kuwaelimisha vijana kuhusu mipaka ya matumizi yake.
Maswali
a) Taja mada ya kifungu hiki.
b) Fafanua nadharia mbili zilizoeleza asili ya lugha ya sheng.
c) Eleza matumizi bainifu ya kilugha cha Sheng katika jamii ya sasa.
d) Taja matokeo hasi ya matumizi ya Sheng katika jamii.
e) Ni kwa nini mwandishi Walibora ameshirikisha matumizi ya Sheng katika kazi yake ya Kidagaa Kimemwozea
f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu hiki.
i) Teknohama
ii) kudorora
iii) msimbo
iv) Kuhujumiwa
Date posted: September 25, 2019.
- Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii.(Solved)
Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii.
Date posted: September 25, 2019.
- "Ingawa walifahamu sababu ya kuitwa pale mpango uliokuwepo ulikuwa usiku wa giza."(Solved)
Damu Nyeusi na Hadithi nyingine : Ken Walibora na Said A. Mohamed
"Ingawa walifahamu sababu ya kuitwa pale mpango uliokuwepo ulikuwa usiku wa giza."
(a) Fafanua muktadha wa maneno haya.
(b) Eleza tamathali iliyotumika katika dondoo hili.
(c) Onyesha vile wahusika mbalimbali hadithini waiivyoathiriwa na sababu ya kuitwa pale.
Date posted: September 25, 2019.
- "Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa...(Solved)
"Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea.
Date posted: September 25, 2019.
- RIWAYA YA KIDAGAA KIMEMWOZEA.
Mtoto ni mtoto hata likiwa bonge la nyama. Mtu hupata ajaliwalo sio alitakalo.
(Solved)
RIWAYA YA KIDAGAA KIMEMWOZEA.
Mtoto ni mtoto hata likiwa bonge la nyama. Mtu hupata ajaliwalo sio alitakalo.
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza tamathali ya lugha iliyotumika katika usemi huu.
(c) Ukirejelea riwaya thibitisha kuwa mtu hupata ajaliwalo silo alitakalo.
Date posted: September 25, 2019.
- Fafanua jinsi maudhui ya unafiki yamejidhihirisha katika tamthilia ya Mstahiki Meya, ukirejelea wahusika wowote watano.(Solved)
Fafanua jinsi maudhui ya unafiki yamejidhihirisha katika tamthilia ya Mstahiki Meya, ukirejelea wahusika wowote watano.
Date posted: September 25, 2019.
- Mbona isiwe kweli? Wewe panga uwalete tule matunda ya jasho letu nao watoto.(Kwa kurejelea tamthilia "Mstahiki Meya")(Solved)
Mbona isiwe kweli? Wewe panga uwalete tule matunda ya jasho letu nao watoto.(Kwa kurejelea tamthilia "Mstahiki Meya")
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza mbinu mbili za uandishi katika dondoo hili.
(c) Eleza yaliyopangwa baada ya usemi huu.
Date posted: September 25, 2019.
- Ole wangu! Ole wangu, nisikize Mola wangu,(Solved)
Ole wangu! Ole wangu, nisikize Mola wangu,
Lipokee ombi langu, wanisikize wenzangu,
Washike ujumbe wangu, uloleta Mola kwangu,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Amri kumi za Mola, mumekwisha zikiuka
Ndipo hamuwezi lala, mumekwisha vurugika,
Mumemsahau Mola, ndipo nanyi mwasumbuka,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Mwaabudu mashetani, ushirikina ni mwingi,
Munaiba hadharani, waongo nao ni wengi,
Mwajawa na taraghani, na wazimu mwingi,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora,
Mwauana ovyoovyo, mwasemana ndivyo sivyo,
Fitina nazo zilivyo, mwarogana vivyo hivyo,
Matusi ni vile sivyo, munaisha ka isivyo,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Kuna dawa za kulevya, na hata pembe haramu,
Na ukimwi nakujuvya, unaua wanadamu,
Na mimba nazo kuavya, watoto ni marehemu,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Wengine nao hudai, waoe jinisi moja,
Ati mwingine hafai, heri sawia ya mja,
Haya maoni ni hoi, tupinge kila mmoja,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Ploti mwazinyakua, na viwanja vya mipira,
Makaburi mwala pia, mabibi mwateka nyara,
Ibada zikifikia, mwafurika kwa majira
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Wengi tuwachaguao, si viongozi ni waizi,
Tamaa walio nao, yaongoza maamuzi,
Mishahara ile yao, huongezwa kila mwezi,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Usalama hatunao, wasiwasi umezidi,
Waja kiwa makazio, huogopa magaidi,
Mabomu walipuao, huruma wamekaidi,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Beti kumi namaliza, dua yangu imetimu,
Mungu amekwisha anza, kuhukumu mwanadamu,
Wote walojipotoza.waiepuke hukumu,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
MASWALI
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
(b) Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari kadhaa. Taja na ueleze bahari zozote tatu.
(c) Taja na ueleze mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika ubeti wa kwanza.
(d) Eleza sababu ya mshairi kutumia alama ya ritifaa katika ubeti wa nne
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumika katika ubeti wa tisa mshororo wa tatu na ueleze umuhimu wake.
(f) Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi.
(g) Taja mifano mitatu ya uozo anaolalamikia mwandishi.
(h) Eleza toni ya mwandishi.
Date posted: September 25, 2019.
- 'Mkinichagua, mimi tutaimarisha masomo, huduma za afya, barabara na pia maji mtapata hivi karibuni. (makofi na vigeregere)
(i) Tambua sajili hii.
(ii) Eleza sifa sita za sajili...(Solved)
'Mkinichagua, mimi tutaimarisha masomo, huduma za afya, barabara na pia maji mtapata hivi karibuni. (makofi na vigeregere)
(i) Tambua sajili hii.
(ii) Eleza sifa sita za sajili hii.
Date posted: September 25, 2019.
- Kanusha sentensi ifuatayo bila kutumia kiunganishi.
Iwapo mvua itanyesha wakulima watapanda mapema.(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo bila kutumia kiunganishi.
Iwapo mvua itanyesha wakulima watapanda mapema.
Date posted: September 25, 2019.
- Andika kwa wingi.
Seremala huyo alikula ndizi kwa uma.(Solved)
Andika kwa wingi.
Seremala huyo alikula ndizi kwa uma.
Date posted: September 25, 2019.
- Tunga sentensi kwa kutumia kivumishi cha sifa kisichoambishika.(Solved)
Tunga sentensi kwa kutumia kivumishi cha sifa kisichoambishika.
Date posted: September 25, 2019.
- Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi - abudu.(Solved)
Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi - abudu.
Date posted: September 25, 2019.
- Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo .
Jane alitengenezewa kiti na fundi kwa nyundo(Solved)
Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo .
Jane alitengenezewa kiti na fundi kwa nyundo
Date posted: September 25, 2019.
- Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana ya vitate rika na lika.(Solved)
Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana ya vitate rika na lika.
Date posted: September 25, 2019.
- Bainisha matumizi ya 'ni'
Kimbieni! Huyu ni mnyama aliyeniuma mguuni.(Solved)
Bainisha matumizi ya 'ni'
Kimbieni! Huyu ni mnyama aliyeniuma mguuni.
Date posted: September 25, 2019.
- Bainisha matumizi ya 'po' katika sentensi ifuatayo.
Alipowasili alionyeshwa walipo.(Solved)
Bainisha matumizi ya 'po' katika sentensi ifuatayo.
Alipowasili alionyeshwa walipo.
Date posted: September 25, 2019.
- Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee cha kusisitiza katika ngeli ya U-U(Solved)
Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee cha kusisitiza katika ngeli ya U-U
Date posted: September 25, 2019.
- Taja msemo mwingine wenye maana sawa na :
piga maji(Solved)
Taja msemo mwingine wenye maana sawa na :
piga maji.
Date posted: September 25, 2019.
- Akifisha sentensi ifuatayo:
Je ni nani alingoa mti wa kiprono(Solved)
Akifisha sentensi ifuatayo:
Je ni nani alingoa mti wa kiprono
Date posted: September 25, 2019.
- Changanua kwa kutumia jedwali.
Yeye alifaulu ingawa hana adabu(Solved)
Changanua kwa kutumia jedwali.
Yeye alifaulu ingawa hana adabu
Date posted: September 25, 2019.
- Nyambua kitenzi 'chwa' katika kauli ya kutendea kisha ukitungie sentensi.(Solved)
Nyambua kitenzi 'chwa' katika kauli ya kutendea kisha ukitungie sentensi.
Date posted: September 25, 2019.
- Andika kinyume cha sentensi ifuatayo .
Mahindi ya mama yamekua kwa kupata mvua ya kutosha.(Solved)
Andika kinyume cha sentensi ifuatayo .
Mahindi ya mama yamekua kwa kupata mvua ya kutosha.
Date posted: September 25, 2019.
- Ainisha vitenzi katika sentensi ifutayo.
Wao watakuja kuwa waandishi maarufu.(Solved)
Ainisha vitenzi katika sentensi ifutayo.
Wao watakuja kuwa waandishi maarufu.
Date posted: September 25, 2019.
- Ainisha mofimu katika neno lifuatalo:
Milangoni(Solved)
Ainisha mofimu katika neno lifuatalo:
Milangoni
Date posted: September 25, 2019.
- Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.(Solved)
Soma kifungu kisha ujibu maswali
Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi. Msemo huu unaafiki kabisa ari ya watu wazima wengi ambao licha ya umri wao, wamo mbioni kutafuta elimu ili mbali na kupata nuru, wajiunge na wasomi wengine katika kuikuza na kuiendeleza jamii. Ni kwa sababu hii ndipo serikali, kwa ushirikiano na mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, imekuwa mstari wa mbele kutoa tunu hii kwa wazee ili kukata kiu yao ya elimu.
Watu wengi wa umri wa makamo ambao labda walikosa kumaliza masomo ya kiwango fulani au walikosa kabisa kwenda shuleni kwa sababu mbalimbali, hasa za kifedha, wamekuwa wakiweka elimu kama mojawapo ya majukumu yao ya utuuzima. Hii imekuwa dhahiri hasa baada ya serikali ya Kenya kuanzisha mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi, kwani idadi ya watu wazima ambao wamejitokeza kunufaika na mpango huo haisemeki. Pamoja na mpango huo, wapo wale ambao walikosa kusoma au kumaliza masomo kwa sababu ya karo, na kwa sababu sasa wana mapato, wameazimia kujiendeleza ili wapate vyeti. Hii ndiyo maana si ajabu kuona hata wafungwa kwenye magereza wakifanya mitihani ya kitaifa.
Elimu ya watu wazima hutekelezwa kwa njia mbalimbali. Kunayo elimu ambayo inalenga kuwapa watu hawa ujuzi wa kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na ufundi wanaofundishwa, ambao huwa ni kazi kama useremala, umekanika, ushoni, usonara na kadhalika, huwawezesha kujitegemea kimapato, kwa hivyo wakaweza kuwapa wanao fursa ya kufaidi kile ambacho wao walikikosa.
Kunayo pia aina ya elimu ya watu wazima ambayo inaegemea maslahi ya watu hawa, hasa mafunzo kuhusu afya na usafi, masuala ya kifamilia na mahusiano na pia suala la ulezi. Kwa kufanya hivi, watu hawa hupata motisha ya kutangamana na watu wengine na kubadilishana nao mawazo kuhusu masuala yanayoathiri maisha yao Ndiyo sababu utapata watu wa aina hii wana ujuzi mkubwa wa kila kitu kinachoendelea katika kila kona ya nchi.
Aina nyingine ya elimu kwa watu wazima ni ile ya umma, inayohusu hasa masuala ya kisiasa. Mara nyingi, utawaona wakongwe wakipishwa kwenve foleni ili kwenda kupiga kura. Hii ni kwa sababu, mbali na kuwa huenda wakawa wamestaafu kikazi, bado wana jukumu muhimu sana katika kufanya maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya vizazi vyao. Hivyo basi, serikali hufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa hamasisho imetolewa kwa kila mwananchi, pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kupiga kura ili kura zisiharibike, hasa baada ya mtu kupitia utaratibu mrefu na wenye kuchosha wa kupiga kura. Kwa hili la kisiasa, watu wazima wengi hushangaza kwa jinsi wasivyoweza kushawishika kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na maazimio yao.
Maswali
(a) Eleza masuala muhimu katika aya mbili za kwanza kwa maneno 60.
(b) Fafanua jinsi elimu ya watu wazima hutekelezwa ukitumia maneno 60
Date posted: September 25, 2019.
- Nyumba ya Ndolo ya vyumba viwili ilikumbwa na hali mbili tofauti usiku huo.(Solved)
Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali
Nyumba ya Ndolo ya vyumba viwili ilikumbwa na hali mbili tofauti usiku huo. Chumbani alimolala Ndolo mwenyewe, kimya cha kaburi kilikatizwa na misono yake. Mara mojamoja alijigeuza kitandani na kuzifanya mbavu za kitanda zilalamikie : uzito wake. Katika chumba kingine, misono ya Ndolo na milio ya chenene ilimkirihi Msela. Kuzidisha, mawazo kuhusu hali ya mamake na unyama aliotendewa babake yalimtoroshea usingizi. Akasalia kujilaza kwenye mkeka wake.Kila alipotafakari maneno ya mzee Ndolo ndivyo Msela alivyozidi kuamini kwamba matatizo ya familia yao yalisababishwa na Mzee Bonga. Lakini yote hayo akayapuuza. Kubwa kwake lilikuwa ni kumwona mama yake na kujua ni hatua gani atakayochukua licha ya uzito aliouona mbele yake kwa kutokuwa na kipato. Msela alijikuta kwenye mtihani mgumu ulioifanya mishipa ya kichwa kusimama na kichwa kumuuma.Kwa sababii ya maiimivu hayo, Msela alijisogeza na kujiegemeza kwenye ukuta. Akawa anatazama iinsi Mungu alikuwa akiufanya muujiza wake ambao alikuwa ameukosa kwa muda. Alifurahi kuliona jua likipenyeza miale yake kisha kujitokeza na kuangaza dunia. Ingawa macho yake yalifurahia mapambazuko hayo, moyo wake ulikuwa na machungu. Akili yake ilikuwa na zigo zito la kutafuta ufumbuzi ambao kwa upande wake ilikuwa ni ndoto.Msela alijiuliza mengi katika nafsi yake. Aliisaili nafsi yake kuhusu hisi za ndugu zake, kuhusu hali ya mama yao aliyesemekana kuwa mwendawazimu, na ikiwa walifahamu hilo. Alitaka kujua alikokula na alikolala mamake katika hali yake hiyo. Kila fikira iliyompitikia akilini ilitaka kupasua mishipa ya kichwa chake. 'Ina maana hawaoni au nao wamekuwa na roho ya korosho kama Mzee Bonga?' alijisaili Msela. Katika maswali yote hayo, alikosa majibu isipokuwa kuzidisha maumivu ya kichwa. Isingekuwa kwa machozi yaliyompunguzia baadhi ya machungu, labda angegeuka hayawani.Macho ya Msela yalikuwa yamevimba, tena mekundu kutokana na ukosefu wa usingizi. Mwili wake nao ulionekana kunyong'onyea kwa sababu ya mazonge ya mawazo. Alichukua kikopo kilichochoka cha maji na kunawa uso kisha akaenda kukaa juu ya jiwe. Kibaridi kilichotokana na mvua iliyokuwa ikinyesha kilimpiga lakini hakujali. Angejali vipi yeye katika mtafaruku wa hali ya mamake?
Ingawa Mzee Ndolo alimwita ndani ili aipishe mvua, Msela alidinda. Badala yake, aliendelea kuuachilia mwili wake kuloweshwa na michonyoto ya mvua. Kila alivyofikiria maisha ya wendawazimu ndivyo moyo ulivyozidi kumuuma. Akawa yuajiuliza mama yake aliukosea nini ulimwengu hata apate adhabu ile. Halafu fumo lake la mwisho moyoni ni madhara ya mvua na baridi ile kwa mamake. Hana makao, hana mavazi mazito, hana chochote! Alipowazia makazi ya jalalani na majumba mabovu ambayo siku zote amekuwa akiwaona wendawazimu wakifaliwa kwayo, aliachama.
Maswali
(a) Eleza ukinzani ulio katika nyumba ya Ndolo.
(b) Ni yapi yaliyomkosesha usingizi msela?
(c) Kwa nini Msela hakuweza kuibadili hali yake.
(d) Taja chanzo cha madhila ya Msela.
(e) Muujiza wa Mungu unatoa taashira gani kwa hali ya msimulizi?
(f) Eleza maana ya msamiati ufuatao ukirejelea taarifa.
i) robo ya korosho
ii) alichama
iii) kunyong'onyea
Date posted: September 25, 2019.
- Tunga sentensi yenye muundo wa:
N + V + T + H + N + E + U + T.(Solved)
Tunga sentensi yenye muundo wa:
N + V + T + H + N + E + U + T.
Date posted: September 24, 2019.
- Eleza matumizi ya kiambishi "ku"
Kulia kwake kulisababisha msongamano wa watu alikoKuwa.(Solved)
Eleza matumizi ya kiambishi "ku"
Kulia kwake Kulisababisha msongamano wa watu alikoKuwa.
Date posted: September 24, 2019.
- Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli zipi?
i) Chumvi:
ii) Nywele:
iii) Mafuta:(Solved)
Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli zipi?
i) Chumvi:
ii) Nywele:
iii) Mafuta:
Date posted: September 24, 2019.