Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Sentensi zinazofuata ni za aina gani? (i) Nyamari aliadhibiwa madhali alifika darasani akiwa amechelewa sana (ii) Mimi sijaelewa kamwe somo hili (iii) Watoto ambao walipotea juzi wamepatikana...(Solved)

    Sentensi zinazofuata ni za aina gani? (i) Nyamari aliadhibiwa madhali alifika darasani akiwa amechelewa sana (ii) Mimi sijaelewa kamwe somo hili (iii) Watoto ambao walipotea juzi wamepatikana leo asubuhi

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii. Wanakujua huku(Solved)

    Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii. Wanakujua huku

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Tungia sentensi moja ziara na maziara ili kubainisha maana zao.(Solved)

    Tungia sentensi moja ziara na maziara ili kubainisha maana zao.

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Andika sentensi katika wakati usiodhihirika ukitumia nomino moja ya jamii.(Solved)

    Andika sentensi katika wakati usiodhihirika ukitumia nomino moja ya jamii.

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Tumia kitenzi kishirikishi kipungufu bila kupoteza maana ya sentensi hii. Mwanafunzi mmoja angali analala bwenini(Solved)

    Tumia kitenzi kishirikishi kipungufu bila kupoteza maana ya sentensi hii. Mwanafunzi mmoja angali analala bwenini

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kisarufi – kikanushi, ngeli, wakati,kitendwa, mzizi na kiishio.(Solved)

    Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kisarufi – kikanushi, ngeli, wakati,kitendwa, mzizi na kiishio.

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/(Solved)

    Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili(Solved)

    Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kuratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hichi ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalum ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama Hawa ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe. Kwa sababu ya bongo alizonazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake na ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini; amevumbua mangala; amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu. Chambacho wavyele , akili nyingi huondoa maarifa. Binadamu amekuwa dubwana linalojenga kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole. Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lililo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri ; akamwambia binadamu, ‘’Haya, twende kazi !’’ Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambavyo ni urithi aliyopewa na muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili Maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa sum na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Joshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta mdhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’ bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi? Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni Imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe. Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemchemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia Kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu. MASWALI (a) Jadili jinsi binadamu anaweza kutumia uwezo wake vizuri. Matayarisho Jibu (b) Ukirejelea kifungu kizima, onyesha jinsi binadamu ametumia nafasi yake vibaya. matayarisho Jibu

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali. Mbuga ya Ziwa Nakuru, sasa limesafishwa katika mojawapo ya juhudi za kukabiliana na maji taka yanayoingia mbugani. Wasimamizi wa mbuga walitumia huduma za vijana wasiokuwa na ajira kutoka mitaa ya Bondeni, Kivumbini, Lake view Freearea na Flamingo kusafisha mito inayobeba uchafu huo. Vibarua walizoa jumla ya tani 1.5, na baadaye tani 4.2 idadi inayofikisha zaidi ya tani 6.0 kwa siku mbili mfululizo.Hili linaashiria jinsi kina cha uchafuzi wa mazingira kwenye ziwa Nakuru umeshamiri,na baadhi ya wafanyikazi wanaona litajwe kuwa janga la kitaifa linalokodolea macho mbuga nyingi humu nchini. Shughuli hiyo ilivutia hisia mseto huku maswali mengi kuliko majibu yakiibuka, endapo KWS ina bajeti ya kung’arisha mbuga za wanyama. Akizungumza na Taifa Leo, mwangalizi wa utalii kutoka kutoka mbuga ya wanyama ya Ziwa Nakuru Bw Sirman Kioko, alisema maji taka yamekuwa yakiingia kwenye mbuga kutokana na miundo msingi duni. Aliongezea kuwa maisha ya wanyama hasa simba, nyati, vifaru,nchui,nviboko na flamingo yalikuwa hatarini,kwa sababu ya maji taka yalikuwa yamebadili mkondo na kupenyeza kwenye mbuga. Miaka mitano iliyopita mbuga ya Nakuru ilikuwa na idadi kubwa ya ndege aina ya heroe ,lakini sasa wamebakia 200 tu. Hali hii itazidi kuwa mbaya,endapo idara husika haitaweka mikakati ya kutafuta suluhu la kudumu kwa wanyama pori wanaozidi kuangamia. Aidha uchafuzi katika ziwa Nakuru umefanya ndege kuhamia ziwa Bogoria ambapo inaaminika angalau chakula ni tele. “Tunakubali kuwa gharama ya kusafisha mbuga ni kubwa,lakini pia tunaomba umma kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki inayoziba njia za maji,”alisema. Pia aliongezea kuwa ni jukumu la mbuga kusafisha mazingira ya wanyama,lakini baraza la mji wa Nakuru pia lina nafasi kubwa ya kuhakikisha makazi ya watu ni safi,kwa kuzoa taka ipasavyo. Anaona kuna utepetevu mkubwa kutoka kwa usimamizi wa mazingira NEMA,wanaostahili kuweka sheria kali za kukabiliana na wale wanaoharibu mazingira. Aliongezea kuwa baraza la kusimamia huduma za wanyama pori (KWS),halina bajeti ya kusafisha mbuga na ndio sababu waliwaajiri vibarua saba kuendesha shughuli hiyo ya siku tatu. Uchafuzi wa mito inayoingia ziwa Nakuru hutokea msimu wa mvua ambapo maji hufurika na kusomba taka kutoka kwenye makazi ya watu. Wanyama wanaovutia watalii kama vile Nyati hupata maradhi pindi wanapokunywa maji chafu,yaliyochanganyika na mifuko ya plastiki. Licha ya KWS kumiliki kituo cha kufanyia utafiti aina ya maradhi mbalimbali yanayokabili wanyama bado hawajafanikiwa kwa asilimia kubwa kuyazuia. Hili linajiri siku moja tu baada ya wakazi wa mtaa wa Bondeni kuandamana barabarani wakilalamikia,ongezeko la kiwango cha takataka kwenye makazi ya watu. (Imenukuliwa kutoka kwa Gazeti la Taifa Leo) Maswali 1. Ipe taarifa hii kichwa mwafaka 2. Eleza sababu zinazofanya Ziwa Nakuru kuchafuka 3. Ni nini madhara ya kuchafuliwa kwa Ziwa Nakuru? 4. Eleza vizingiti vinavyofanya ziwa hili kuendelea kuchafuliwa 5. Toa mapendekezo yanayoweza kusaidia kumaliza uchafuzi wa Ziwa Nakuru kulingana na taarifa hii. 6.Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika taarifa. a. Kupenyeza b. Utepetevu

    Date posted: September 24, 2019.  

  • Andika sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo . Nimewaleta askari kituoni ili wawalinde wananchi wote wanaosumbuliwa na majambazi. Anza: Wananchi........(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo . Nimewaleta askari kituoni ili wawalinde wananchi wote wanaosumbuliwa na majambazi. Anza: Wananchi........

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Ainisha vihusishi vilivyopigiwa mstari. Atieno ndiye mtoto wa mwisho wa Ojwang lakini ni mwerevu kuliko wengine.(Solved)

    Ainisha vihusishi vilivyopigiwa mstari. Atieno ndiye mtoto wa mwisho wa Ojwang lakini ni mwerevu kuliko wengine.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Unda nomino kutokana na kivumishi kifuatacho: Tepetevu(Solved)

    Unda nomino kutokana na kivumishi kifuatacho: Tepetevu

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Andika upya sentensi kwa kutumia "O" rejeshi tamati. Gari lililoanguka si lile unalolizungumzia.(Solved)

    Andika upya sentensi kwa kutumia "O" rejeshi tamati. Gari lililoanguka si lile unalolizungumzia.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika hali ya kufanyiza. i) - La ii) - Nywa iii) -Fa(Solved)

    Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika hali ya kufanyiza. i) - La ii) - Nywa iii) -Fa

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Leteni!(Solved)

    Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Leteni!

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi. Msomi hakutuzwa siku hiyo.(Solved)

    Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi. Msomi hakutuzwa siku hiyo.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Kanusha sentensi ifuatayo :- Kuliko na vita kwahitaji amani.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo :- Kuliko na vita kwahitaji amani.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii. Nyanya ametengezewa kitanda kizuri na mjukuu wake.(Solved)

    Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii. Nyanya ametengezewa kitanda kizuri na mjukuu wake.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii. Alivyolikimbilia(Solved)

    Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii. Alivyolikimbilia

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Eleza sifa bainifu za sauti /j/.(Solved)

    Eleza sifa bainifu za sauti /j/.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo (i) Kubahatika (ii) Ubahaili(Solved)

    Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo (i) Kubahatika (ii) Ubahaili

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Akifisha sentensi ifuatayo. Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana.(Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo. Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo. Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni.(Solved)

    Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo. Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Bainisha matumizi ya kiambishi "ku" katika sentensi hii. Naomi atakupikia chai alafu aende kule uwanjani.(Solved)

    Bainisha matumizi ya kiambishi "ku" katika sentensi hii. Naomi atakupikia chai alafu aende kule uwanjani.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo. Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni(Solved)

    Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo. Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.(Solved)

    Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja.(Solved)

    Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja.

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao.(Solved)

    Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao.Ni kutokana na kilio cha mwananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo serikali imejitolea sabili kubadili hali katika idara hiyo huku tume mbali mbali zilizobuniwa zikitoa mapendekezo muhimu ya kurekebisha idara hiyo. Matokeo ya hivi punde kutoka kwa shirika la Transparency International liliorodhesha idara ya polisi kama idara fisadi zaidi nchini,maoni ambayo yalisisitiziwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu .Ufisadi bado umekita mizizi katika idara ya polisi tangu mabadiliko yaanze upande wa trafiki na hata ndani ya polisi,.Serikali imejitolea kupambana na ufisadi unaonekana kuwa kidonda ndugu katika idara ya polisi. Wananchi wanasema kuwa polisi ni mafisadi na kusahau kuwa ufisadi unashirikisha watu wawili na wote wanapaswa kufunguliwa mashtaka,lazima raia na polisi wazingatie hili.Na ili kuleta mabadiliko muhimu katika idara ya polisi,mapendekezo yote pamoja na ya tume zingine za hapo awali lazima yatekelezwa na kwa mujibu wa katiba mpya.Lazima mabadiliko yaanze kuanzia juu kwani maafisa wadogo hulazimiswa kuchukua hongo ili wapelekee wakubwa wao,ni lazima shughuli ya kuwachagua maafisa waliobora ifanyike kisheria ili mabadiliko yaanze kutoka kwa wakuu wa maafisa wa polisi. Polisi kidogo wameweza kubadili ile lugha yao ya matusi na ukali kwa rai.Raia nao hawajabadilika,bado wana uwoga dhidi ya polisi na itachukua muda kwani wanadhania kuwa kikosi ni kile kile cha kitambo.Kwa upande wa polisi, hakuna mageuzi yamefanyika.Unaposafiri kuja mjini polisi wangali wana chukua hongo kutoka kwa wenye matatu na kuwaruhusu kubeba kupita kiasi, pia usalama umedorora sana kwani kumekuwa na visa vingi vya mauaji hapa mjini.ukiangalia maafisa wa polisi hakuna mageuzi makubwa yameshuhudiwa haswa kwa upande wa maafisa wa trafiki bado ni wale wale na ufisadi ungali upo. Mabadiliko ambayo tunataka ni ile polisi wasikae mahali kwa muda hadi wanajuana na mafisadi na majambazi.Maafisa wa polisi wanafaa kuhudumu katika kituo kimoja kwa muda usiozidi miaka mitatu.Kwa kufuata njia hiyo mabadiliko yatapatikana.Juhudi nyingi zikielekezwa katika kubadili kikosi cha polisi wananchi wanapaswa kuhamasishwa ili nao wawezakubadilikahaswa kuhusuiana na mtazamo wao kwa maafisa wa polisi .Na huku tukijaribu kubadili maafisa wa polisi wananchi pia wanapaswa kuelimishwa ili waweze kubadili mtazamo wao kuhusu maafisa hao.Ni bayana kuwa ili kuweza kuleta mabadiliko ya kutamanika katika kikosi cha polisi na haswa katika kupambana na ufisadi uliokita mizizi wananchi sawia na maafisa wa polisi wanajukumu la pamoja kuleta mabadiliko hayo yatakayopelekea kuwepo kwa mlahaka mzuri kati ya maafisa wa polisi na raia.Hatimaye kuwepo kwa huduma bora itakayochangia pakubwa kuboresha uchumi wa taifa na kuafikiwa kwa ruwaza ya mwaka 2030. Maswali a) Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka. b) Thibitisha kwamba ufisadi ni kidonda ndugu ukirejelea makala haya.. c) Ni vipi ufisadi katika idara ya polisi unaweza kuzikwa katika kaburi la sahau? d) "Wananchi ndio wanapaswa kulaumiwa kwa ufisadi."Thibitisha. (e) "Serikali imepiga hatua katika kuleta mabadiliko katika idara ya polisi.Onyesha kinayacha usemi huu. (f) Taja manufaa yoyote mawili yanayotokana na mabadiliko katika idara ya polisi (g) Eleza maana ya: (i) Mlahaka (ii) Utepetevu (iii) Kujitolea sabili

    Date posted: September 23, 2019.  

  • Eleza vikwazo mbali mbali vinavyotatiza ukuaji wa Fasihi Simulizi.(Solved)

    Eleza vikwazo mbali mbali vinavyotatiza ukuaji wa Fasihi Simulizi.

    Date posted: September 23, 2019.