Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili Fasihi

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

265 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Taja kitamkwa chenye sifa ifuatazo. Vokali ya nyuma, kati(Solved)

    Taja kitamkwa chenye sifa ifuatazo. Vokali ya nyuma, kati.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Kuna sababu kadha za kuwako na kushamiri kwa ajira ya watoto.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Kuna sababu kadha za kuwako na kushamiri kwa ajira ya watoto. Moja ya sababu hizo ni umaskini unaozikumba jamaa nyingi pamoja na welewa mdogo wa thamani ya elimu wa baadhi ya watu katika jamii. Wapo watoto ambao hushurutika kubeba jukumu la kujizumbulia riziki wenyewe kutokana na hali duni ya familia zao. Hali hii huweza kutokana na baadhi ya wazazi kutelekeza majukumu yao ya kimsingi ya kuikimu jamaa yao. Aidha kuna sehemu nyingine ambapo hali hii imetokana na janga sugu la ukimwi. Yapo maeneo ambako kuenea kwa ugonjwa huu kumewafanya viongozi wa jamaa kupukutika kama majani ya mti na kuwalazimisha watoto kuyakatiza masomo yao ili wawakidhie haja wadogo zao. Kuhusiana na kutelekeza majukumu, kuna wazazi ambao wanakosea kwa kutowaelekeza watoto wao kujua maadili mema ni yepi. Kwa njia hii watoto hao wanaishia kutumbukia kwenye matatizo makubwa. Baadhi ya ajira zina athari kubwa sana kwa watoto. Ukahaba, kwa mfano, ni mojawapo ya ajira ambazo watoto wa kike hulazimika kujiingiza. Hii ni ajira ambayo inaweza kuwatumbukiza watoto hao katika hatari kubwa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuambukizwa maradhi ya ukimwi. Asillimia kubwa ya watoto wanaotumbukia katika ajira hii, inapatikana katika maeneo ya mijini na sehemu ambako utalii umeshamiri sana. Umaskini pamoja na dhiki za mijini huwalazimisha watoto hao wa kike kuishia kwenye biashara za aina hiyo. Wengine hufanyiwa hila na wafanyabiashara ambao wametovukwa na utu kutokana na tamaa yao kubwa ya kujitajirisha. Katika maeneo ambako utalii umeshamiri, ukahaba wa watoto unatokana na umaskini pamoja na kusambaa na kuenea kwa maadili ajinabi, ya ulimwengu usio wetu. Ikiwa umaskini ni chocheo kubwa la kuwapo kwa ajira ya watoto, basi inahalisi serikali zetu zifanye kila juhudi kuhakikisha kuwa umaskini umepigwa vita. Pana umuhimu wa kuhakikisha kuwa wanajamii wote wamepewa nafasi sawa za kujikwamua kutoka lindi la umaskini. Isitoshe, pana umuhimu wa juhudi nyingi kufanywa kuhakikisha kuwa nafasi za shule zimepanuliwa ili kuikidhi idadi kubwa ya watoto ambao wana kiu ya elimu. Serikali haina budi pia kuhakikisha kuwa zimepitishwa sheria zinazomlinda motto dhidi ya ukatili unaotokana na watu waliokosa hisia za utu na ubinadamu. Upo pia umuhimu wa kuvisaidia vikundi vinavyojitahidi kuwasaidia watoto ili kuzifanikisha juhudi zao kwa kuwa chanda kimoja hakivunji chawa kama tujuavyo. Hatua nyingine ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kupunguza ajira ya watoto ni kuwahamasisha wanajamii kuhusu haki za mtoto. mtoto yeyote yule ana haki ya kupata elimu ya msingi. Mtoto pia ana haki ya kuishi na kupata mahitaji ya kimsingi na ya lazima kama chakula, malazi au makazi na matunzo ya kiafya. Aidha mtoto ana haki ya ukuaji, yaani kukua kikamilifu pasi na kizuizi na katika mazingira yasiyombana kwa njia yoyote ile. Isitoshe, mtoto ana haki ya kupata ulinzi dhidi ya unyanyaswaji au udhalilishwaji wa aina yoyote ile au hata maonevu kwenye misingi yoyote iwayo. Mtoto pia ana haki ya kuwa huru kushiriki katika jumuiya yake, kutoa maoni na kujieleza, kushirikiana na kujiunga na vikundi. Mwisho, na muhimu zaidi, mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya ajira au aina yoyote ya kazi ambayo inaihatarisha afya na siha yake au inamzuia asipate elimu. (a) Fupisha aya mbili za mwanzo bila kubadilisha maana. (maneno 60-70) (b) Eleza hoja muhimu zinazojitokeza katika aya mbili za mwisho. (Maneno 50-60)

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Tamaa mbele mauti nyuma. Thibitisha ukweli ya methali hii ukirejelea hadithi ya Tazamana na mauti.(Solved)

    Tazamana na Mauti” (S.A. Mohammed) Tamaa mbele mauti nyuma. Thibitisha ukweli ya methali hii ukirejelea hadithi ya Tazamana na mauti.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Uniulie nini na ndoa yetu na wewe inamhusu pia yeye?"(Solved)

    Mwana wa Darubini (K. Mwende Mbai) "Uniulie nini na ndoa yetu na wewe inamhusu pia yeye?" a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Eleza sifa zozote nne za msemewa. c) Jadili madhila yanayomkumba mwanamke katika hadithi hii.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Lazima kwanza mnihakikishie kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili."(Solved)

    Mstahiki Meya "Lazima kwanza mnihakikishie kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Taja sifa zozote nne za msemaji. c) Andika umuhimu wa huyo sumu.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Tayari nimemkabidhi barua ya kujiuzulu ninapohusika."(Solved)

    Mstahiki Meya Tayari nimemkabidhi barua ya kujiuzulu ninapohusika." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Mbali na changamoto inayofanya msemaji kujiuzulu, jadili changamoto nyinginezo zinazowakumba wanacheneo.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Eleza namna mbinu ya Taharuki ilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    Eleza namna mbinu ya Taharuki ilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Kwa kufafanua hoja saba thibitisha kwamba kuna haja ya kuwa na Revolution.(Solved)

    Kidagaa kimemwozea Kwa kufafanua hoja saba thibitisha kwamba kuna haja ya kuwa na Revolution.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Lakini bila matumaini hatuwezi kwenda mbele na Revolution."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea "Lakini bila matumaini hatuwezi kwenda mbele na Revolution." i) Eleza muktadha wa dondoo hili. ii) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Naingia ukumbini, nyote kuwakariria, Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia, Mnipe masikioni, shike nachoelezea, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Naanza kwa uzalendo, nchi yetu tuipende, Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuilinde, Wa kila mtu mwendo, usije kawa mpinde, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili Wote tuwe na umoja, tuuache ukabila Kabila lisiwe hoja, mwenza kumnyima hela, Taifa letu ni moja, Mkenya ndilo kabila, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Linda demokrasia, uongozi tushiriki, Haki kujielezea, wachotaka na hutaki. Changu naweza tetea, demokrasia haki, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Tena adili usawa, mgao raslimali, Bajeti inapogawa, isawazishe ratili. Idara zilizoundwa, ‗faidi kila mahali, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Tuwe na uadilifu, twache tamaa ya hongo, Tusiwe na udhaifu, wa kuwa watu waongo, Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Ubinafsi si adili, ila ni kusaidia, Ukiwa nayo mali, asiyenacho patia, Kama mtu mswahili, ubinafsi achia, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. Na inavyoelezea, katiba ni kielezi, Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi, Kwa hayo nitamwachia. hiyo ya ziada kazi, Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili a) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na aadili. b) Taja tamathali yoyote moja inayojitokeza katika shairi hili. c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia kigezo kifuatacho : Mpangilio wa vina d) Bainisha nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili. e) Eleza toni ya shairi hili f) Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa nne g) Andika ubeti wa pili kw lugha nathari h) Eleza maana ya neon lifuatalo kama ilivyotumiwa katika shairi: i) hongo

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Vijana wana kumbwa na changamoto kadhaa katika jamii.Jadili baadhi ya changamoto hizi kwa kurejelea hadithi zozote tano kutoka diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.(Solved)

    Vijana wana kumbwa na changamoto kadhaa katika jamii.Jadili baadhi ya changamoto hizi kwa kurejelea hadithi zozote tano kutoka diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendowe" Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi Mzizi na Matawi.(Solved)

    "Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendowe" Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi Mzizi na Matawi.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Hivi vitu lazima viwepo,au kama havipo ni lazima viwe ni vipengee mahususi vya uhalisia wamaisha yetu:(Solved)

    Damu Nyeusi Na Hadithi Nyingine-Ken Wal'ibora Na S.Ahmed "Hivi vitu lazima viwepo,au kama havipo ni lazima viwe ni vipengee mahususi vya uhalisia wa maisha yetu: (a) Liweke dondoo katika muktadha wake faafu. (b) Fafanua sifa zozote nne za msemaji wa maneno haya. (c) Eleza kwa tafsili matatizo yoyote mawili yanayoikumba jamii ya hadithi mlimotolewa nukuu hii.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Wewe,Utazame mlolongo wa(Solved)

    SHAIRI A Wewe, Utazame mlolongo wa Waja unaoshika njia likiwapo; Unaofuata pembe za barabara zisokuwapo, Kwenda kuisaka auni, Kuitafuta kazi inayowachenga. Itazame migongo ya wachapa kazi, Watokwao na jasho kapakapana, Wanaotafunwa uhai na jua liso huruma: Wakiinua vyuma na magunia, Wakiinua makontena, Wakichubuka mashambani, Wakiumia viwandani, Wakiteseka makazini, Halafu Uangalie ule ujira wa kijungu meko, Mshahara uso kifu haja, Nguo zisizositiri miili dhaifu, Kilio chao kisichokuwa na machozi, Na Ujiangalie Mwili wako unaomereta ujana wa ufanisi, Gari lako la kifahari lililozibwa vioo, Jumba lako la kujishasha kama uwanja mdogo, Malaki yapesa unayomiliki, Ujiitapo mwajiri kwa raha, hunusi usaha wa hali yao? SHAIRI B Dunia kitendawili, hakuna ateguaye; Dunia kama tapeli, hadaa nyingi ujuye; Dunia mwenye akili, inampiku na yeye; Dunia ina mizungu, tena yapika majungu. Dunia na yake hali, hupumbaza hatimaye; Dunia ina akili, binadamu sichezeye; Dunia uwe na mali, huiwezi dhorubaye; Dunia ina mizungu, tena yapika majungu. Dunia wenye muali, ambao waichezeye; Dunia kipigo kali, huwakumba hatimaye; Dunia wakaja kuli, ?menipata nini miye? Dunia ina mizungu, tena yapika majungu Maswali (a) Je, mashairi haya mawili ni ya aina gani? Toa sababu. (b) Taja dhamira kuu katika kila shairi. (c) Kwa kutoa hoja zozote tatu linganua mashairi haya kiumbo. (d) Taja na uelezee nafsi-pokezi katika mashairi haya mawili. (e) Kwa kutolea mfano mmoja mmoja eleza matumizi ya mbinu hizi (i) Kweli –kinzani (ii) Mishata (f) Tambua idhini ya kishairi iliyo tumika katika neno ?Waichezeye" Na uelezee dhima yake katika utoshelezi wa kian ldhi. (g) Dondoa mfano mmoja mmoja wa mbinu ya tashihisi kutoka kwenye Mashairi yote mawili. (h) Andika ubeti wa tatu katika shairi la A kwa lugha nathari. (i) Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotu? nika katika vifungu hivi. (i) Inampiku. (ii) Makontena.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.(Solved)

    Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana.Siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea "Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana.Siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu." (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Wahusika hawa wawili ni kama shilingi kwa ya pili.Thibitisha.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."(Solved)

    Timothy Arege, Mstahiki Meya "...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Fafanua sifa tano za msemaji (c) Tunagawana sote ni kinyume ejia hali halisi. Thibitisha.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali, (Solved)

    SIPENDI KUCHEKA Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali, Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili Sipendi mimi kucheka Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika Halafuye nikacheka! Masikini akiteswa Yatima akinyanyaswa Mnyonge naye akinyonywa Sipendi hata ikiwa Unazo nguvu najuwa Ni hili sitatekezwa Mbona lakini nicheke, kwayo furaha? Na wewe ukajiweke, uli na siha? Na yatima ali pwek.e, wa anahaha? Amenyimwa haki yake, hanayo raha! Na moyo wangu ucheke, kwa ha ha, ha! Kucheka kwa kucheka Mimi katu sitacheka. MASWALI a) Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha. b) Taj a sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka. c) Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho. d) Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili. e) Tambua toni ya shairi hili. f) Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili. g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi i) Mawi ii) Nyemi

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.(Solved)

    “Shaka ya Mambo” (Farouk Topan) Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Nashangaa vile kwetu tunavyoabudu watu hao wasiotujali."(Solved)

    “Damu Nyeusi” (Ken Walibora) "Nashangaa vile kwetu tunavyoabudu watu hao wasiotujali." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Bainisha matumizi ya mbinu ya ishara kwa kurejelea hadithi ya gilasi ya mwisho makaburini.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.(Solved)

    Mstahiki Meya Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."(Solved)

    Mstahiki Meya "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya? c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Taja aina nne za hadithi.(Solved)

    Taja aina nne za hadithi.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.(Solved)

    Kidagaa kimemwozea Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Siwe ulosema jana, ya kuwa u mashuhuri? Ya kuwa wajuwa sana, aidha huna kiburi? Nchini wajulikana, mwanasiasa mahiri, Bungeni tukuajiri?(Solved)

    SIWE? 1. Siwe ulosema jana, ya kuwa u mashuhuri? Ya kuwa wajuwa sana, aidha huna kiburi? Nchini wajulikana, mwanasiasa mahiri, Bungeni tukuajiri? 2. Siwe ulotushawishi, kwa chumvi na kwa sukari, Na matamu matamshi, ukaziteka suduri, Ukanena penya moshi, moto ndiyo yakwe siri, Nawe ndiye hiyo nari? 3. Siwe uloji‘ta moto, uwakao biribiri, Kamba ‗tatia fukuto, Litakalo leta kheri‘, Utatufunua mato, Maisha yawe mazuri, Tukupe kura waziri? 4. Siwe ulosema hayo, na mengi ukabashiri, Ukamba wafata nyayo, nyayo ziso utiriri, Tusiwe na wayowayo, wa kufikirifikiri, Tukuachie ujari? 5. Siwe tulokuinua, Mabegani kama mwari, Tungawa twalemelewa, waume tukajasiri, Kamba tukikuchaguwa, mema kwetu yatajiri, Tukakeyi kusubiri? 6. Siwe ulotugeuka, kwamba leo u waziri, Wajiona melimuka, tena ukawa ayari, Walaghai ukicheka, ukuu umekughuri, Leo mekuwa hodari? 7. Siwe ulojawa raha, za hino yetu sayari, Ukawa ja vile shaha, hatukupati shauri, kutuona ni karaha, wakatiwo twahasiri, Ushakiya msitari? 8. Siwe uliyetughura, ukafunga na safari, Ukaelekea bara, Kwa wenzio matajiri, Ukatuacha majura, na tama kukithiri, Kanama Ushaghairi? 9. Siwe uliyetuasi, ukenda pasi kwaheri, Mbona hutwambii nasi, tukajua yetu shari, Leo una masidisi, husemi na aso gari, Ndio mezidi jeuri? 10. Siwe‘lotwaa mgwisho, ukawa wajifakhiri? Chenye mwanzo kina mwisho, hilo wajuwa dhahiri, Vyaja kutoka vitisho, kwani hayo sidahari, Mambo mengimdawari? 11. Siwe utakayeiza, mwishowo ukidhihiri, Siku itayoteleza, kuja kwetu ansari, Kuja kutubembeleza, kwa nyunga nalo khamri, Tauya nazo nadhiri. MASWALI a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? b) Taja na ueleze bahari tatu za shairi hili? c) Onyesha jinsi mtunzi alivyotumia idhini ya kishairi. d) Taja na ufafanue tamahali ya usemi iliyotawala katika shairi hili. e) Anayerejelewa alibailika vipi? Eleza. f) Andika ubeti wa tisa kwa lugha ya nathari. g) Mshairi ana maana gani kwa kusema: (i) Wakatiwo twahasiri. (ii) Ukaziteka suduri.

    Date posted: October 3, 2019.  

  • Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.(Solved)

    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Nimemwita bwana huyu aje huku juu kusudi mumwone."(Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine "Nimemwita bwana huyu aje huku juu kusudi mumwone." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Eleza sifa tatu za mzungumzaji. c) Jadili maudhui ya ubaguzi namna yanavyojitokeza katika hadithi husika

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"(Solved)

    Riwaya ya Kidaa Kimemwozea. "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …" a) Eleza muktadha wa maneno haya. b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya. c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Kutowajibika kwa viongozi baada ya mkoloni kuondoka ni dhahiri." Jadili kauli hii kwa mujibu wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    "Kutowajibika kwa viongozi baada ya mkoloni kuondoka ni dhahiri." Jadili kauli hii kwa mujibu wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019.  

  • "Nashukuru sasa umeanza kuona mambo yanavyostahili kwenda."(Solved)

    Mstahiki Meya. "Nashukuru sasa umeanza kuona mambo yanavyostahili kwenda." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Eleza sifa zozote nne za msemaji. c) Fafanua maudhui ya ufisadi kama yalivyoangaziwa na mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 2, 2019.