Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu. ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika(Solved)

    Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu. ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa aina yoyote. Neno huzuni linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto dunia imejaa raha, starehe na vicheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya kufurahisha na kustarehesha tu, sio KUDHIKISHA NA KUHUZUNISHA. Huyu tunayemzumgumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha kitendekacho mkono wake wa kushoto na kile kinachofanyika hasa katika mkono wake wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo, vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi machungu ambayo huleta huzuni, sio raha. Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, mcha mwana kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule, huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Ili wasome kama inavyotakikana, ni sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaadhibu, hasa wale watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ilivyo. Watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ilivyo. Watoto wa aina hii wanapotiwa adabu raha hujitenga na huzuni huwatawala. Huzuni, hivyo basi, inaonekana ya kuwa ni uso wa pili katika maisha ya mwanadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana, ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa humo katikati ya kustarehe. Si tu, inajulikana dhahiri shahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo watu wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao. Zingatia mtoto anaezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali, kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote. Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, aliyempata bila kupanga. Hata mtoto huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni mlevi na unalojua ni kurudi nyumbani kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa aina hiyo atakayoijua ni huzuni tu, sir aha asilani. a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (Maneno -100) b) Ukizingatia aya ya mwisho, eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto huzuni. (Maneno 40-45)

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno utandaridhi ni neno mseto ambalo maana yake ni utamaduni uliotanda au kuenea ardhi nzima. Mtu mtandaridhi’ hivyo basi ni mtu aliyebebea kikamilifu katika utamaduni huu mpya kwa jinsi moja au nyingine. Matandaridhi hujihusisha sana katika kutandaridhisha aina moja au nyingine ya amara muhimu za kitandaridhi. Hizo ni kama vile biashara za kumataifa, lugha za kimataifa, aina za mavazi zilizotokea kupendwa ulimwenguni kote, muziki wa kisiku hizi, hasa vile pop, reggae, raga, rap, ambao asili yake ya hivi majuzi ni Marekani. Muziki huo waimbaji wake hutumia, sana sana, lugha ya Kiingereza hususan kile cha Marekani na kadhalika Watandaridhi wana nyenzo zingine kadha wa kadha za kuendeshea maisha yao au kujitambulisha. Wao huwasiliana kutoka pembe moja ya duni hadi nyingine wakitumia vitumeme, yaani vyombo vitumiavyo umeme kufanya kazi vya hali ya juu, kama vile tarakilishi na simu, hata za mkono. Watu hawa hawakosi runinga sebuleni mwao, usiseme redio. Hawa husikiliza na kutazama habari za kimataifa kupitia mashirika matandaridhi ya habari kama vile BBC la uingereza CNN la marekani. Aidha watu hawa husafiri mara kwa mara kwa ndege na vyombo vingine vya kasi. Hawa hawana mipaka. Wale wanaohusudu utandaridhi wanaamini kindakindaki kwamba utamaduni huu wa kilimwengu umeleta mlahaka mwema baina ya watu binafsi, makampuni makubwa makubwa ya kimataifa na usiano bora baina ya mataifa. Watu hawa husikia wakidai ya kuwa aina hii ya utamaduni imeupigisha mbele ustaarabu wa wanadamu ulimwenguni kote. Kwa upande mwingine, wakereketwa wa tamaduni za kimsingi za mataifa na makabila mbalimbali ulimwenguni wanadai ya kwamba utandaridhi umeleta maangamizi makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umeleta maangamizi makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umesemekana kwamba unasababisha kutovuka kwa utu miongoni mwa wanadamu wote, ambao wamo mbioni kusaka pesa na kuneemesha ubinafsi. Inadaiwa pia kwamba utandaridhi umesababisha kutovuka kwa adab kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka kwa adabu kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka kwa adabu kwa vijana, hasa wale wa mataif yanayojaribu kuendelea, kumeleta zahama chungu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuenea kwa UKIMWI kwa kasi ya kutisha. a) i) Bainisha kwa kutoa maelezo kamili kwamba utandaridhi ni neno mseto. ii) Tohoa maneno mawili kutokana na neon kutandaridhisha kisha ueleze maana za maneno hayo. b) i) Nini maana ya ‘hawa hawana mipaka?’ ii) Kwa nini watandaridhi wanpenda kusikiliza na kutazama habari kupitia BBC na CNN? c) i) Eleza kikamilifu maoni ya watandaridhi kuhusu utamaduni wao ii) Je, Utandaridhi unalaumiwa kwa nini katika kifungu hiki? d) Msemo: “ chungu mbovu” ni msemo wa kimtaani tu. Msemo sawa ni upi e) Eleza maana ya maneno yafuatayo i) Amara ii) Mlahaka iii) Wakereketwa

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza maana ya methali Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni(Solved)

    Eleza maana ya methali Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza maana mbili tofauti za Rudi(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za Rudi

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tumia misemo ifuatayo katika sentensi; i) Enda nguu ii) Chemsha roho(Solved)

    Tumia misemo ifuatayo katika sentensi; i) Enda nguu ii) Chemsha roho

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tunga Sentensi zitakazobainisha maana ya jozi za maneno zifuatazo: i) Mbari Mbali ii) Kaakaa Gaagaa(Solved)

    Tunga Sentensi zitakazobainisha maana ya jozi za maneno zifuatazo: i) Mbari Mbali ii) Kaakaa Gaagaa

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya i) –enye ii)-enyewe(Solved)

    Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya i) –enye ii)-enyewe

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Ukizingatia nenolililo katika mabano, andika sentensi hizi atika hali ya kutendeka. i) Daraja hili (vuka) tu wakati wa kiangazi. ii) Kitabu hicho (soma) ijapokuwa sura zingine sura...(Solved)

    Ukizingatia nenolililo katika mabano, andika sentensi hizi atika hali ya kutendeka. (alama 2) i) Daraja hili (vuka) tu wakati wa kiangazi. ii) Kitabu hicho (soma) ijapokuwa sura zingine sura zingine hazimo.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Yapange majina yafuatayo katika ngeli zake i) Neno ii) Kiongozi iii) Mate (Solved)

    Yapange majina yafuatayo katika ngeli zake i) Neno ii) Kiongozi iii) Mate

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika sentensi hizi upya ukitumia o-ote. i) Chakula kikibaki hutupiliwa mbali ii) Kila nyumba unayoingia unapata watoto wawili(Solved)

    Andika sentensi hizi upya ukitumia o-ote. i) Chakula kikibaki hutupiliwa mbali ii) Kila nyumba unayoingia unapata watoto wawili

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Sahihisha sentensi zifuatazo i) Kile kitabu kilipasuka ni changu ii) Matofali haya yanatumiwa kwa ujenzi wa nyumba(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo i) Kile kitabu kilipasuka ni changu ii) Matofali haya yanatumiwa kwa ujenzi wa nyumba

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika sentensi hizi kwa umoja i) Mafuta haya yanachuruzika sana ii) Miinuko ile ndiyo mwanzo wa milima ya Chungu.(Solved)

    Andika sentensi hizi kwa umoja i) Mafuta haya yanachuruzika sana ii) Miinuko ile ndiyo mwanzo wa milima ya Chungu.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Akifisha sentensi hii: Watu wengi wamezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini kufanya hivyo ni sawa.(Solved)

    Akifisha sentensi hii: Watu wengi wamezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini kufanya hivyo ni sawa.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo, halafu uzigeuze sentensi hizo kwa wingi. (i) Nilisoma kitabu chake (ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia (iii) Alishinda nishani ya dhahabu(Solved)

    Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo, halafu uzigeuze sentensi hizo kwa wingi. (i) Nilisoma kitabu chake (ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia (iii) Alishinda nishani ya dhahabu

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.(Solved)

    Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Samaki anayejirusha kutoka majini huitwa?(Solved)

    Samaki anayejirusha kutoka majini huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Anayefundisha mwari mambo ya nyumbani huitwa?(Solved)

    Anayefundisha mwari mambo ya nyumbani huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika kinyume cha i) Shari ii) Oa(Solved)

    Andika kinyume cha i) Shari ii) Oa

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Kwa kila jozi ya maneno uliyopewa tunga sentensi mbili kutofautisha maana: (i) Ini- Hini (ii) Tairi- Tahiri(Solved)

    Kwa kila jozi ya maneno uliyopewa tunga sentensi mbili kutofautisha maana: (i) Ini- Hini (ii) Tairi- Tahiri

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika visawe ( maneno yenye maana sawa) vya maneno haya: (i) Sarafu (ii) Keleji. (iii) Daktari.(Solved)

    Andika visawe ( maneno yenye maana sawa) vya maneno haya: (i) Sarafu (ii) Keleji. (iii) Daktari.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza katika sentensi maana ya misemo ifuatayo (i) Uso wa chuma (ii) Kuramba kisogo(Solved)

    Eleza katika sentensi maana ya misemo ifuatayo (i) Uso wa chuma (ii) Kuramba kisogo

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata kuweza kuwatawala na kuwapangia maisha yao. Binadamu amekirimiwa uwezo wa kuyatawala mazingira na kukabidhiwa hekima ya kuweza kusana ala mbalimbali ili kuyakabili mazingira hayo. Hekima hii humwezesha kusitiri kizazi chake. Aidha, ametunukiwa uwezo mkubwa wa kuivinjari sayari hii yetu katika ilhamu yake ya kutaka kuvumbua ‘siri’ za maumbile, amejasiri hata kuzitalii sayari nyingine nje ya uso wa ulimwengu huu. Si ajabu kwamba iwapo wanyama wengine wangepewa urazini wa kuongea kama yeye, wangalimwandikia tumbi la vitabu kusiuf busara yake. Sifa za ujasiri wake kamwe hazingewatoka vinywani mwao! Hata hivyo, kuna tofauti nyingine kubwa kati ya binadamu na hayawani, Tofauti hii inaweza kumvua binadamu sifa zake zote na kuuona ukwasi wa maarifa yake kama ishare ya maangamizi ya ulimwengu. Hii ni kutokana na hasara anayosababisha katika mazingira tulivu walivyoumbiwa viumbe wote. Uzuri wa ulimwengu tunamoishi humpendeza kila kiumbe hata yule anayemchukia binadamu kama nzi. Wote hufurahia mazingira yao; hewa safi itokayo milimani, chemichemi, mito na vijito mnamotiririka maji safi, vilele vya milima vilivyokumbatiwa na theluji daima dahari, yakiwemo mabonde na tambarare zinazohimili uhai wa viumbe wengi. Urembo huo wa kiasili hauwezi kukamilika bila vichaka na misitu inayoipamba sayari hii huku ikileta mvua. Mapambo yote haya huendeshwea na nguvu za maumbile; nguvu ambazo hazisababishwi na kuwa hatari kwa uhai wake na ule wa viumbe wenzake kwa sababu anayaharibu maumbile kwa kiasi kikubwa kinachomtisha yeye mwenyewe. Hii ni kwa sababu gani? Sababu zipo nyingi. Sababu mojawapo ni uchafuzi wa maji kama rasimali muhimu ya kiasili. Uchafuzi huu umewaletea viumbe na mimea maafa mengi, yakiwemo maradhi mbalimbali. Kwa kweli bila maji, uhai utatoweka duniani. Uharibifu mkubwa wa maji machafu yenye sumu hasa kutoka viwandani na kuingia kwenye mito na bahari, huwadhuru biumbe wengine ambao makao yao ni majini. Maji huleta madhara si tu kwa mimea bali hat kwa binadamu kupitia kwa ulaji wa vyakula. Misituni rasilimali nyngine inayokimu viumbe, lakini binadamu anaiponza. Ukataji wa miti kiholela hasa kwenye sehemu za chmichemi husababisha uhaba wa mvua. Uhaba huo nao huleta kiangazi kinachokausha mimea na visima vya maji. Mchapuko wa ujenzi wa viwanda hasa katika nchi zilizostawi wanasayansi wanaohusika na hali za anga umesababisha taharuki na wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu umenyosha kuwa ule utandu unaozuia miale ya jua kupenya moja kwa moja kweye sayari hii na juhatarisha uhai, sasa unaanza kutoweka taratibu. Hii ni kutokana na hewa chafu itokayo viwandani. Kwa kadri binadamu anavyozidi kujiimarisha kiviwanda ndivyo ambavyo mabaki yaviwanda yanavyozidi hatua hii, ni binadamu atakuwa amechangia pakubwa katika kutowesha uhai wa viumbe wote ulimwenguni. Mikutano mingi ya kmataifa imefanywa nab ado inaendelea kufanywa kila uchao ili kutahadharisha umma wa ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na mali asili. ‘Ajenda’ za mikutano hiyo hasa zinalenga nchi zilizostawi kwani hizi ndizo zinazochafua mazingira kwa kasi zaidi kuliko zile zinazostawi . Mapendekezo mengi yametolewa katika vikao hivyo ili kusuluhisha tatizo hili lakini ni hatua chache mno zinazochuliwa kurekebisha mamba. Inatupasa sisi wenyewe kuchukua jukumu la kusafisha mazingira yetu. Tuwafunze pia watoto wetu kuhifadhi mazingira yanapochafuliwa au kuharibiwa. Tukumbuke kuwa Mwana hufuata kisogo cha nina.Mazingira yanpochafuliwa au kuharibiwa, afya zetu zimo hatarini, na hali hii pia ni tisho kwa viumbe wengine, hata vimatu! Kila mmoja wetu anawajibika kutunza mazingira anamoishi kwa manufaa yetu sote na kwa vizazi vijavyo. a) Kulingana na taarifa hii, kwa nini binadamu anahesabiwa kuwa na uharibifu mkubwa kushinda wanyama wengine? b) Onyesha uhusiano uliopo baina ya maendeleo ya binadamu na uharibifu wa mazingira. c) Ni kwa nini mwandishi anahofia zaidi athari za miale ya jua? d) Eleza kwa ufupi hasara zinazoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira. e) taja hatua mbili ambazo mwanadamu angeweza kuchukua ili kupunguza madhara ya viwanda. f) Kulingana na makala haya ni nini maana ya methali “mwana hufuata kisogo cha nina?” g) Eleza maana ya (i) Kusana (ii) Mchapuko

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani(Solved)

    Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika sentensi za mseto kutokana na mbili fupi ulizopewa a) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka kupita mtihani b) Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi hapa(Solved)

    Andika sentensi za mseto kutokana na mbili fupi ulizopewa a) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka kupita mtihani b) Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi hapa

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Kwa kurejea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja(Solved)

    Kwa kurejea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa i) Yule Ngo’mbe alizaa ndama mkubwa jana ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa mda mrefu.(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa i) Yule Ngo’mbe alizaa ndama mkubwa jana ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa mda mrefu.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tunaweza kusema katika chumba au i) …………………………………………………..ama ii) ……………………………………………………..(Solved)

    Tunaweza kusema katika chumba au i) …………………………………………………..ama ii) ……………………………………………………..

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana i) Kikombe chenye kimevunjika ni kipya ii) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana i) Kikombe chenye kimevunjika ni kipya ii) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu

    Date posted: June 27, 2019.