- Tunga sentensi sahihi ukidhihirisha wingi wa majina yafuatayo:
i) Ukanda
i) Uzee(Solved)
Tunga sentensi sahihi ukidhihirisha wingi wa majina yafuatayo:
i) Ukanda
i) Uzee
Date posted: June 27, 2019.
- Andika ukubwa wa
Mwizi aliiba kikapu na ngo’mbe(Solved)
Andika ukubwa wa
Mwizi aliiba kikapu na ngo’mbe
Date posted: June 27, 2019.
- Andika umoja wa sentensi hizi:
(i) Kwato za wanyama hutufaidi
(ii) Mnataka vyeti vya kuwasaidia?(Solved)
Andika umoja wa sentensi hizi:
(i) Kwato za wanyama hutufaidi
(ii) Mnataka vyeti vya kuwasaidia?
Date posted: June 27, 2019.
- Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia
mbili tofauti.
Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.(Solved)
Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia
mbili tofauti.
Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.
Date posted: June 27, 2019.
- UFUPISHO
Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama
himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua
watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo...(Solved)
UFUPISHO
Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama
himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua
watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo basi, badala ya kusubiri waje wazitie baruti
nyumba na kuzilipua, badala ya kungojea waje wawachinje raia wake kama kuku, badala
ya kungonja ashuhudie minazi yote kisiwani na miti mingine ya manufaa kukatwa katwa
na makatili hao, badala ya kujitayarisha yeye mwenyewe mji, faua ya kuikatakata miti
yote ili Waareno wakija wasikute chochote cha kuvutia macho na watokomee kabisa.
Alijua asipotekeleza uamuzi huo mkali, basi Wareno watakujja na hasira zote na
kuadhibu waliomo na wasiokuwemo, kama walivyofanya Faza.
Unyama uliofanyika huko alikuwa ameusikia ukisimuliwa mara zisizohesabika. Katika
masimulizi hayo, alikuwa amesikia ya kwamba Falme hiyo ya Faza ilipoasi utawala wa
Kireno, askari wa Kireno, chini ya uongozi wa Martin Affenso de Mello, walifanya
unyama hapo mjini Faza ambao ulikuwa haujawahi kutokea, hata katika mawazo.
Inavyosemekana ni kwamba Wareno waliamua kuangamiza chochote chenye uhai, hata
wanyama na miti na wakautimiza muradi wao. Ajabu ni kwamba, hata kasisi
aliyeheshimika sana wa Kireno enzi hizo, Baba Joao dos Santos, aliunga mkono tukio hili
akisema ya kwamba wafaza walistahili kuadhibiwa. Hakuna mtu hata mmoja upande wa
Wareno aliyekilaani kitendo hiki cha kutisha.
Hii ndiyo sababu Mfalme Yusuf na raia wake walipowazima wareno hapo Mombasa,
aliwaamuru watu wajitolee kuwashabulia kwenye vituo vyao vyote kaitika mwabao
mzima wa mashariki ya Afrika. Baada ya kuamua hivyo, alienda Uarabun kutafuta silaha
ili atekeleze azimio lake.
Alipopata zana za kutosha, ikiwa ni pamoja na silha na meli, alianza kupambana na
wareno kuo huko Arabuni, mahali pitwapo Shihr. Halafu alielekea mwambao wa pwani
ya AFrika aliwasumbua sana maadui zake, Mwisho alikita makao yake Bukini ambako
aliendelea kuwashambulia Wareno kokote walikokuwa.
a) Eleza sababu zilizomfanya Mfalme Hassan kuuangamiza mji wake, na halafu
kuuhama (maneno 30-40)
b) Ukitumia Maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha kuanzia aya
ya pili hadi mwisho wa kifungu (maneo 75-80)
Date posted: June 27, 2019.
- Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata.
Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira.
Alipopata umri wa miaka kumi na...(Solved)
Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata.
Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira.
Alipopata umri wa miaka kumi na mine tu, Mwanakishwira alikuwa tayari ni mrefu na
mkubwa, na alionekana kuwa msichana mzima mwenye umri wa miaka kumi na minane.
Alikuwa nadhifu na mzuri sana wa sura, kiasi cha kubandikwa lakabu ya malaika.
Lipendeza sana macho fauka ya kuwa alikuwa na akili nyingi mno. Katika umri huo,
alikuwa amemaliza masomo yake yote katika madrassa iliyokuwa hapo, na aliweza
kuikariri. Kurhani yote bila kigezigezi. Babake, Mfalme, aliuma videole akilia ngoa kuwa
motto mwenye akili hiyo ni mke wala sio mume. Aliwaza ya kuwa kama angekuwa
mvulana, angempeleleka zutafindaki ya Al-Azhar huko Misri kuendelea na masomo ya
juu katika chuo hicho kisifika.
Wakati mfalme akiuma vidole kuhusu junsia ya motto wake, wanaume wengi hapo mjini
walikuwa wakimeza mate. Mtu aliyememezewa mate alikuwa ni yeye huyo
Mwanakishwira. Walimmezea mate kwa sababu kila mmoja wao alitaka kumwoa awe
mkewe. Kumwoa Mwanakishwira kulikuwa na manufaa ya kupata mke mwenye uzuri
wa shani, kama nyota, na aidha kuwa Mfalme baada ya mwenye kukikalia kuaga dunia,
sababu yeye hakuwa na mrithi mwingine.
Basi ikawa ni kila mtu kujipendekeza kwa mfalme…Kila mtu bila kujali nasaba.
Walijipendekeza wakwasi na mwakata pia. Mwisho Mfalme, Kwa vile alikuwa
anasumbuliwa sana, na wakati huohuo aliogopa kuwa asipomwoza mapema binti yake
huenda akaharibika, akaamua kuruhusu wachumba wamchumbie.
Uamuzi huu ulimshtua sana Mwanakishwira, Mshutuko aliopata ulimtia ugonjwa na
kumdoofisha kabisa. Akadhoofu hadi Mfalme akaingiwa na hofu ya kuwa motto wake
atakufa. Akaamua kumwuliza kinachomdhoofisha. Mwanakishwira. Mwanakishwira
akasema kimdhoofishacho ni mwezi. Akipata mwezi, na nafuu pia ataipata.
Kusikia hivyo, Mfalme akatokwa na kijasho chembachemba. Akafikiria kwamba labda
motto wake amemalizwa kabisa na uwele, na sasa yaweweseka tu, wala hana akili razini
ya kutambua na kupanga mambo.
Hata hivyo hakuvunkika moyo kabisa. Akaamua kupata tafsiri ya kitendawili hicho
kutoka kwa waheshimiwa wake hapo mjini. Ambao wote walitaka mumwoa
Mwanakishwira.
Kwanza akamwendea Waziri Mkuu akamwulia tafsiri ya mwezi autakao binti yake.
Waziri akasema mwezi utakikanao ni wa dhahabu. Alipoambiwa hivyo motto akzidi
kudhoofu. Mfalme akakasirika sana. Akawaendea wakwasi wengine kama vile Kadhi, Mnajimu na Kadhalika. Hawa wote wakamzidisha ugonjwa binti Mfalme kwa sababu
jawabu walizotoa ni kuwa mgonjwa alihitaji mwezi wa almasi, fedha na hata hatua!
Mwisho kabisa, Mfalme akamwendea Mvulana aliyeckuwa mchungaji. Huyu
akamwaidhi Mfalme kwamba aulize mgonjwa aseme mwenyewe aina ya mwezi
aitakayo. Jawabu hili halikumfurahisha Mfalme, japo alienda kamwuliza binti yake,
kama alivyoambiwa. Alipoulizwa Mwanakishwira akasema mwezi autakao ni kishaufu
kilicho na umbo la mwezi mchanga kilichotengenezwa na chuma. Mfalme alishangaa
sana, Hata hivyo akamfulia kisaufu alichokitaka mgonjwa. Alipokivaa, Mwanakishwira
akapata nafuu mara moja na akaendelea na nafuu hiyo hadi akapona kabisa.
Kuona hivyo, Mfalme akawateremsha vyeo wakwasi wote humo mjini, na kuteua
wengine mahali pao. Kwa upande mwingine, mchungaji akaozwa binti Mfalme na
kupewa madaraka ya Waziri Mkuu. Hatimaye, Mfalme alipoaga dunia, mchungaji akawa
Mfalme na Mwanakishwira akawa Malkia.
a) Zungumzia swala la meuke (yaani mahali pa mwanamke au mwanamume katika
jamii) katika falme ya pate ya enzi hiyo.
b) i) Kwa nini Mfale iliwauliza wakwsi kwanza tafsiri ya kitendawili
ii) Kwa nini mfalme alishangazwa na jawabu la binti yake?
c) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake” Dhihirisha jinsi methali hii inavyobainika
katika hadithi hii
d) Ni nini maoni yako kuhusu mwanamume aliyemwoa Mwanakishwira na kwa nini
alikubali kuolewa na huyo?
e) Eleza maana ya maneno na tamathali za semi zifuatazo
i) Fauka ya kuwa
ii) Akilia ngoa
iii) Uzuri wa shani
iv) Akamwaidhi
Date posted: June 27, 2019.
- Eleza maana ya:
i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji
ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.(Solved)
Eleza maana ya:
i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji
ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.
Date posted: June 27, 2019.
- Kamilisha:
i) Bumba la ……………………..
ii) Genge la……………………..(Solved)
Kamilisha:
i) Bumba la ……………………..
ii) Genge la……………………..
Date posted: June 27, 2019.
- Tunga sentensi tatu zikionyesha maana tatu za neno chungu.(Solved)
Tunga sentensi tatu zikionyesha maana tatu za neno chungu.
Date posted: June 27, 2019.
- Taja methali inayoafikiana na maelezo haya:
i) Wengine wanapoozana na kugombana, kunao
wanaofurahia kabisa hali hiyo.
ii) Afadhali kuhudhuria huo mkutano hata kama umechelewa(Solved)
Taja methali inayoafikiana na maelezo haya:
i) Wengine wanapoozana na kugombana, kunao
wanaofurahia kabisa hali hiyo.
ii) Afadhali kuhudhuria huo mkutano hata kama umechelewa
Date posted: June 27, 2019.
- Tunawaitaje watu hawa?
(i) Mtu anayebeba mizigo kwa ujira
(ii) Mtu anayeshughulikia elemu ya nyota(Solved)
Tunawaitaje watu hawa?
(i) Mtu anayebeba mizigo kwa ujira
(ii) Mtu anayeshughulikia elemu ya nyota
Date posted: June 27, 2019.
- Sahihisha sentensi hizi:
(i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri
(ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana(Solved)
Sahihisha sentensi hizi:
(i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri
(ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana
Date posted: June 27, 2019.
- Andika upya sentensi zifuatazo ukitumia neno amba
(i) Kijiti kilichovunjika kilimwumiza Amina guu kenyaplex
(ii) Barua zitakazoandikwa na baba kesho zitatumwa mwaka
ujao.(Solved)
Andika upya sentensi zifuatazo ukitumia neno amba
(i) Kijiti kilichovunjika kilimwumiza Amina guu kenyaplex
(ii) Barua zitakazoandikwa na baba kesho zitatumwa mwaka
ujao.
Date posted: June 27, 2019.
- Andika kwa wingi:
(i) Uta wake ni mrefu na mkubwa sana
(ii) Merikebu itayokayofika kesho itango’a nanga kesho kutwa.(Solved)
Andika kwa wingi:
(i) Uta wake ni mrefu na mkubwa sana
(ii) Merikebu itayokayofika kesho itango’a nanga kesho kutwa.
Date posted: June 27, 2019.
- Taja na ubainishe aina za viwakilishi katika sentensi zifuatazo
(i) Ile minazi yangu niliyopalilia inakua vizuri
(ii) Mimi ninataka kumwona mwanariadha aliyepata nishani ya
dhahabu(Solved)
Taja na ubainishe aina za viwakilishi katika sentensi zifuatazo
(i) Ile minazi yangu niliyopalilia inakua vizuri
(ii) Mimi ninataka kumwona mwanariadha aliyepata nishani ya
dhahabu
Date posted: June 27, 2019.
- Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya vitenzi vya silabi moja
katika jinsi ya kutendesha ukitumia silabi hizi
(i) -la
(ii) nywa
(iii) fa(Solved)
Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya vitenzi vya silabi moja
katika jinsi ya kutendesha ukitumia silabi hizi
(i) -la
(ii) nywa
(iii) fa
Date posted: June 27, 2019.
- Tunga sentensi moja moja ukitumia alama zifuatazo za uakifishaji
(i) Ritifaa
(ii) Parandesi
(iii) Dukuduku
(iv) Mshangao.(Solved)
Tunga sentensi moja moja ukitumia alama zifuatazo za uakifishaji
(i) Ritifaa
(ii) Parandesi
(iii) Dukuduku
(iv) Mshangao.
Date posted: June 27, 2019.
- Andika kwa msemo halisi
Yohana alisema kwamba njiani kulikuwa kumenyesha sana ndio sababu tulichekelewa(Solved)
Andika kwa msemo halisi
Yohana alisema kwamba njiani kulikuwa kumenyesha sana ndio sababu tulichekelewa
Date posted: June 27, 2019.
- Taja vielezi vinavyopatikana katika sentensi hizi; kisha ueleze ni vielezi vya aina gani
(i) Aliamka alfajiri
(ii) Mtu huyu ni hodari sana(Solved)
Taja vielezi vinavyopatikana katika sentensi hizi; kisha ueleze ni vielezi vya aina gani
(i) Aliamka alfajiri
(ii) Mtu huyu ni hodari sana
Date posted: June 27, 2019.
- Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
Wimbo Mwimbaji Uimbaji
Jengo ……………. ……….
Pendo ……………. ……….(Solved)
Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
Wimbo Mwimbaji Uimbaji
Jengo ……………. ……….
Pendo ……………. ……….
Date posted: June 27, 2019.
- Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
Wimbo Mwimbaji Uimbaji
Jengo ……………. ……….
Pendo ……………. ……….(Solved)
Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
Wimbo Mwimbaji Uimbaji
Jengo ……………. ……….
Pendo ……………. ……….
Date posted: June 27, 2019.
- Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi.
Alimpatia soda ya chupa
Alimpatia soda kwa chupa.(Solved)
Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi.
Alimpatia soda ya chupa
Alimpatia soda kwa chupa.
Date posted: June 27, 2019.
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Raha ni kitu gani? Je, ni kitu kizuri au kibaya? Mbona kila mutu hipigania na
kama ionekanavyo, kila aionjaye hatimaye humwunguza?...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Raha ni kitu gani? Je, ni kitu kizuri au kibaya? Mbona kila mutu hipigania na
kama ionekanavyo, kila aionjaye hatimaye humwunguza? Au pengine wako
wengine wasiooungua? Hebu basi tuzingatie wale wasemekanao huitafuta sana
raha na, penginepo wakafanikiwa kuipate.
Chukua mfano wa msichana na mvulana wapendanao. Hawa wawili
wanapopendana, lengo lao huwa ni kuoana na wakishaoana, waishi raha
mustarehe milele na milele. Hata hivyo, jambo la kwanza ni kwamba, hata kabla
hawajaoana, wanadhikika na kudhikishana kwa kutaka sana kuaminiana si mara
haba wakati wakiwa wapenzi mar. Mara kadha wa kadha husameheanana
kuendelea na mapenzi. Baadaye wakiwa na bahati, huona.
Mara tu wanapooana hugundua kuwa huko kuishi raha mustarehe ilikuwa ni
ndoto tu ya ujana iliyotengana kabisa na uhalisia. Uhalisia unapowabinikia huwa
ni kuendelea na huko kudhikishana,kutoridhishana, kutiliana shaka, kuombona
mamaha na kuendelea tu.
Ama tumwangalie mwanasiasa. Huyu anapigania usiku na mchana ili awe
mjumbe. Mwisho anachanguliwa, lakini afikapo bunge, anakuta hakuna
anayemtambua kama bwana mkubwa. Inambainikia kwamba ubawana- Mkubwa
hautegemei kuchaguliwa tu, bali unategemea mambo mengine pia, kama vile pesa
nyingi, magari makibwa, sauti katika jamii na wadhamini wanotambulikana. Raha
kwa mwanasiasa huyu inakuwa mithili ya mazigzi tu, “maji” uyaonayo kwa mbali
wakati una kiu kali sana, kumbe si maji bali ni mmemetuko wa jua tu.
Mwingine wa kupigiwa mfano ni msomi. Huyu huanza bidii yake akiwa mdogo
sana. Lengo lake huwa ni atambuliwe kote kwa uhohadri wake katika uwanja wa
elimu. Basi mtu huyu husoma mpaka akaifikia daraja ya juu kabisa ya usomaji.
Akapata shahada tatu: ya ukapera, ya uzamili nay a uzamifu. Akajiona yu upeoni
mwa ulimwengu. Akatafuta kazi akapata. Kisha akagundua kwamba watu
hawakijali sana kisomo chake. Wakamwona ni kama mwehu tu. Fauka ya hayo
wakamlumu kwa kupoteza muda wake mwingi kupekuapekua vitabu.
Wakamfananisha na mtu mvivu.
Mwisho tuangalie mfano wa mwanamuziki . Huyu anahaghaika na wazo la
kwamba sauti yake ikiwaonga watu, atapendwa sana na wengi na kuwazuzua
wengi kama mbalamwezi au kuwaongoza kama nyota. Mtu huyu anapofikia kilele
cha malengo yake hata husahau kama ni binadamu wa kawaida, akawa anaishi
katika muktadha wa watu kuzirai kwa sababu ya akili kujawa pomoni na upungaji
wake. Watu hutamani hata kumgusa tu. Hata hivyo, mtu huyu huishis kujisikia
mkiwa pale wakati unapowadia wa kupumzika. Je, raha yote huwa imekimbilia
wapi?
a) “Mapenzi ni kuvumiliana.” Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jinsi
msemo huu ulivyo muhtasari mwafaka way a pili nay a tatu ya habari hii.
(Maneno 30-35)
b) Kwa muhtasari, raha ni “asali chungu. “Fafanua dai hili huku ukirejelea
mwanasiasa, msomi na mwanamuziki (maneno 45-55)
Date posted: June 27, 2019.
- Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta
zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila...(Solved)
Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta
zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila uchao
zinatengana kiasi cha kukaribia kupigwa mfano wa masafa ya ardhi na mbingu. Seher
zenyewe ni mijini na mashabani. Sehemu hizi, hasa ukizitia katika mizani ya hali na jia
za watu za maisha, zimetofautiana mno. Kiasi cha tofauti hizi ni kikubwa hadi
kuonekana kama kwamba hazina uhusiano kamwe, mithili ya nchi mbili tofauti.
Hebu sasa tuzingatie yale yana yozifanya sehemu hizi kukosa kufanana. Hapa
tutawajibika kuzizingatia tofauti zilizo bayana baina ya watu wa shamba na wa mijini,
hasa kufungamana na jinsi wanavyoyaendesha maisha yao.
Jambo lililo wazi ni kwamba watu wa mashambani hawajapiga hatua ya maana kuhusu
jinsi wanavyuotakikana kuishi katika karne ya ishirini. Watu hawa bado wanaishi kama
walivyoishi mababu zao. Hawahisi halahala ya jambo lolote. Mategemeo yao ni shamba;
usubiriwe msimu mzuri wa mvua, watu walime, Mungu akineemeshe kilimo, wavune
mavuno mema, Chakula kikiwa tayari, wale, walale, siku nyingine warudie mkondo uo
huo wa kuendesha maisha yao.
Watu hawa maisha yao yamepangika mikondo mitatu tu: kuzaliwa, kuoa au kuolewa, na
kufa. Zaidi ya mikondo hii, maisha ya viumbe hawa hayana mabadiliko makubwa.
Mabadiliko haypendelewi sana huko mashambani. Huko, wanaume ni mabwana,
wanawake ni mfano wa vijakazi na watoto hawana tofauti kubea na watwana. Mwanume
akikohoa, mkewe akimbilie kulikokoholewa, na watoto watetemeke. Wanawake wa
shamba na watoto hawana haki hata ya kunena, wala hawajui haki ni nini.
Kwa upande mwingine, mijini kuna viwanda, kuna majumba, kuna magari na kuna
vyombo vingi sana vya maendeleo ya kisiku izi. Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu
kote, wala si watu wa mji mmoja tu. Watu wa mji wowote ulimwenguni huweza
kuwasiliana na wenzao wa miji mingine kokote kule ulimwenguni kwa njia ya runinga.
Pia, kwa watu wa mjini, kuona kiumbe kidogo kabisa kisichoweza kuonekana kwa
macho si ibura hata. Kiumbe cha namna hiyo huonekana kupitia mangala. Na kwa wale
walioondokea kuwa wanajimu wa kisasa, kuziona sayari na thurea zilizoko mbali sana
nasi kupitia ningala ni jabo la kawaida sana.
Watu wa mjini huwa na mabadiliko mengi sana katika maisha yao, wala sio mikondo
aina tatu tu. Kwa mfano, wanawake wa mijini hawakubali tena kuonewa na wanaume.
Wanajua vyema sana maslahi yao na wameiweka menke yao mbele; yaani mahali pao
katika jamii, wakiwa wao ni wanawake. Kupigania haki sawa na wanaume bila kulegeza
kamba. Huku kupambana kimaisha kama wapambanavyo wanaume na kufanikiwa kufanya kazi za kusikika kam vile uwakili, udaktari, uhandisi, urubani na nyinginezo
zilizokuwa zikifanywa na wanaume tu. Wanawake wengine hata ni maprofesa! Kweli
watu wa mijini wameendelea.
a) Toa maelezo kuhusu tofauti zinazosemekana ni bayana baina ya maisha ya watu
wa shamba nay ale ya watu wa mijini.
b) Rejelea “Mungu” katika aya ya tatu na neon “viumbe” katika aya ya nne.
Bainisha uhusiano uliopo baina ya manen haya mawili, hasa ukizingatia jinsi
yavyotumiwa katika habari. Je matumizi haya yankupa hisia gani?
c) Unadhani mwandishi ana maana gani anaposema ya kwamba huko mashambani
“wanawake ni mfano wa vijakazi, na watoto hawana tofauti kubwa na watwana?”
d) Orodhesha vifaa vyovyote vitano vilivyotajwa katika taarifa hii, kisha ueleze
umuhimu wa kila kimoja wapo.
e) “Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu kote” Hapa mwandishi anamaanisha
nini?
f) (i) Ni nini maana ya neon menke?
(ii) Mwandishi anamaliza taarifa yake kwa kusema “Kweli watu wa mijini
wameendelea.” Kwa muhtasari, ni tabia gani za wanamiji zilizomfanya
kukiri hivyo.
Date posted: June 27, 2019.
- Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata
hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi.
Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe...(Solved)
Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata
hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi.
Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe viambilshi hivyo tofauti
vya ngeli (Katika umoja na Wingi)
Date posted: June 27, 2019.
- Eleza maana mbili za sentensi:
Jua nisemalo ni muhimu kwetu.(Solved)
Eleza maana mbili za sentensi:
Jua nisemalo ni muhimu kwetu.
Date posted: June 27, 2019.
- Akifisha:
Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza
sijaona.(Solved)
Akifisha:
Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza
sijaona.
Date posted: June 27, 2019.
- Ondoa- amba-bila kubadilisha maana.
(i) Kuimba ambako kulisifika siku nyingi sasa kunatia shaka
(ii) Mibuni ambayo hupandwa wakati wa mvua hustawi(Solved)
Ondoa- amba-bila kubadilisha maana.
(i) Kuimba ambako kulisifika siku nyingi sasa kunatia shaka
(ii) Mibuni ambayo hupandwa wakati wa mvua hustawi
Date posted: June 27, 2019.
- Nyambua vitenzi vifuatavyo ili kupata majina (nomino) mawili mawili
tofauti:
(i) Kumbuka
ii)Cheka(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo ili kupata majina (nomino) mawili mawili
tofauti:
(i) Kumbuka
ii)Cheka
Date posted: June 27, 2019.
- Andika kwa umoja
Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru.(Solved)
Andika kwa umoja
Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru.
Date posted: June 27, 2019.