Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Jaza kiambishi kifaacho: Ume__________ ona kalamu nyekundu ziliz_______potea?(Solved)

    Jaza kiambishi kifaacho: Ume__________ ona kalamu nyekundu ziliz_______potea?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Siku hiyo nilipitia mahali hapo kama nilivyokuwa nikimuona siku hizi zote, mwaka nenda mwaka rudi. Nilisimama huku nikishangaa kwa mara nyingine tena. Nilikuwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Siku hiyo nilipitia mahali hapo kama nilivyokuwa nikimuona siku hizi zote, mwaka nenda mwaka rudi. Nilisimama huku nikishangaa kwa mara nyingine tena. Nilikuwa najitayarisha kujiendea na hamsini zangu mtu huyo alipojipinda kwa mbali sana. Kwa hakika nilidhani macho yangu yananihadaa. Nikafikicha macho yangu nikitumia nishati yote iliyomo mwilini mwangu ili niyatoe matongo ambayo nilituhumu kwamba ni akili yangu tu iliyokuwa imeniadaa, nikaamua kuendelea na safari yangu kwenda kujitafutia riziki. Hatua ya kwanza na ya pili, moyo haukunipa. Sauti katika kilindi cha moyo wangu ikanisihi na kunitafadhalisha nitazame nyuma. Kutupa jicho nyuma, nikamnasa mtu huyo akeguka! Nikashtuka sana! Jambo la kwanza nildhani macho yangu yameingiwa na kitu kilichoyafanya kuona mambo yasiyokuwepo. Pili, nilidhani iwapo niliyoyaona yana msingi wowote, basi huenda ama nina wazimu, au yule mtu ni mzuka, hasa kwa vile ilionekana ni mimi tu nimuonaye. Nilikikuwa niko katika hali ya kufanya uamuzi kuhusu dhana zangu hizi aina aina mtu huyo alipojigeuzageuza, kisha akafunua macho! Moyo ulinienda mbio. Nilitaka kutifua vumbi ili wazimu usinizidie, lakini sikupata nafasi. Mtu yule alijizoazoa na kuketi kitako. Kisha akatokwa na maneno katika lugha iliyofanana sana na Kiswahili. Niliyaelewa aliyokuwa akisema. Ajabu ya maajabu, mtu huyo alidai ya kwamba tangu alipolala kivulini hapo tangu jana baada ya chakula cha mchana, hakuota ndoto hata moja bali usingizi wake ulikuwa mithili ya gogo! Sasa nilikuwa na hakika kwamba ikiwa mimi sina wazimu, basi kiumbe yule aliyevaa ngozi iliyochakaa sana katika mpito wa miaka hakika ana wazimu. Nilitaka kuhakikisha, hivyo nilimkumbusha kwamba amelala mahali hapo kwa muda wa miaka mingi sana. Kusikia hayo alianza kunikagua. Akasema nimevaa kizungu. Akanitajia tofauti nyingi baina ya vijana aliowazoea na mimi. Mwisho wa yote akauliza kama siku hiyo si tarehe kumi na nane mwezi wa pili mwaka wa 1897. Nikadhani anafanya mzaha kwa hivyo nikacheka. Nilipoona kicheko changu kinamuudhi, nikamwambia siku hiyo ni tarehe kumu na nane mwezi wa pili mwaka wa 1997. Nilipoona ameshangaa kwa dhati, nikagundua ukweli. Alikuwa amelala kwa karne nzima!. a) Eleza hoja nne muhimu zinazojitokeza katika aya tatu za mwanzo. (Maneno 75-85) b) Kwa maneno yako mwenyewe, fupisha aya mbili za mwisho bila kubadilisha maana. (Tumia maneno 40-50)

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamaake-kuu. Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume. Akanyangapo mume naye papo huutia wayo wake. Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na mwanamume. Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege, masonara, waashi, wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi. Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati. Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga hatua ya kutomrudisha ukutani. Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi. a) Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya mwanamke katika jamii? b) Jamii imemfanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua c) Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake.’ d) Zungumzia maswala ya ndoa na elimu huku ukilinganisha mwanamke wa kiasili na wa kisasa. e) Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa? f) Taja mifano minne ya ‘mawazo ya kihafidhina. g) Eleza maana ya: (i) Akafyata ulimu…………………………………………… (ii) Ukatani……………………………………………………. (iii) Taasubi za kiume…………………………………………. (iv) Aushi…………………….………………………………..

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayetii wakuu wake(Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayetii wakuu wake

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana: (i) Kuchokoachokoa maneno (ii) Kumeza shubiri(Solved)

    Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana: (i) Kuchokoachokoa maneno (ii) Kumeza shubiri

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto(Solved)

    Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama (i) Kifaru (ii) Nyati(Solved)

    Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama (i) Kifaru (ii) Nyati

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tumia kiulizio – pi – kukamilisha (i) Ni mitume ………………………. Aliowataja? (ii) Ni kiziwi ………………………. . Aliyemwona akipita?(Solved)

    Tumia kiulizio – pi – kukamilisha (i) Ni mitume ………………………. Aliowataja? (ii) Ni kiziwi ………………………. . Aliyemwona akipita?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Watu wafuatao wanafanya kazi gani (i) Mhasibu (ii) Mhazili(Solved)

    Watu wafuatao wanafanya kazi gani (i) Mhasibu (ii) Mhazili

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi: (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike(Solved)

    Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi: (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine(Solved)

    Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi: Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali(Solved)

    Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi: Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Akifisha kifungu hiki: Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika insha hii.(Solved)

    Akifisha kifungu hiki: Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika insha hii.

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata Lugha ya Kiswahili ni lugha iliyoendelea sana. Leo hii lugha hii inasema na watu wote nchini Tanzania, Rwanda na Burundi,...(Solved)

    Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata Lugha ya Kiswahili ni lugha iliyoendelea sana. Leo hii lugha hii inasema na watu wote nchini Tanzania, Rwanda na Burundi, inasemwa na watu wote nchini Kenya. Nchini Uganda, Zaire, Malawi, msumbiji, Zambia, Somalia, Bukini (Madagascar) na Ngazija (Comoro), inasemwa na asilimia kubwa za wananchi wa huko. Aidha lugha hii ina wasemaji si haba katika kisiwa cha Sokta na nchini Oman. Fauka ya maendeleo haya, Kiswahili kinatumika kwa minajili ya matangazo ya habari katika idhaa nyingi za mashirika ya habari ulimwenguni. Nchi zenye idhara za Kiswahili ni kama vile hizi zetu za Afrika ya Mashariki na kati, Afrika ya kusini, Nigeria, Ghana, Uingereza, ( shirika la B.B.C) Marekani ( shirika la V.O.A), Ujerumani ( shirika la Radio Deutch Welle, Cologue), Urusi ( Radio Moscow), China, India na kadhalika. Maendeleo mengine yanapatikana katika upande wa elimu, Marekani peke yake, kuna vyuo zaidi ya mia moja vinavyofundisha Kiswahili kama lugha muhimu ya kigeni. Huko Uingereza vyuo kama London, Carmbridge na Oxford vinafundisha lugha hii. Nci nyingine ambazo zina vyuo vinavyofunza lugha ya Kiswahili ni kama vile Japan, Korea, Ghana, Nigeria na kadhalika Kweli Kiswahili kimeendelea jamani. Lakini je, kilianza vipi? Na ilikuwaje kikaweza kupiga hatua hizi zote? Kiswahili kilianza kuzungumzwa na kabila dogo la watu waliokuwa wakiitwa wangozi. Watu hawa walikuwa wakiishi mahali palipoitwa shumgwaya. Shungata ni nchi ya zamani iliyokuwa eneo lililoko katika nchi katika nchi mbili jirani ambazo siku hizi ni Kenya na Somalia. Kabila hili la wangozi iliishi irani na makabila mengine kama vile wajikenda, wapokomo, Wamalakote ( au Waelwana) na Wangazija ( kabla hawajahamia visiwa vya Ngazija) Lugha ya wangozi siku hizo, ambayo ndiyo mzazi wa Kiswahili cha leo, ilijulikana kwa jina kingozi. Kama ilivyosemwa hapo awali, kingozi kilisemwa na watu wachache sana. Je lugha hii ilikuwaje mpaka ikapata maendeleo haya makubwa tunayoyashuhudia siku hizi? Ama kwa hakika, Kiswahili ni lugha iliyobahatika tu. Inaweza kusemwa kwamba lugha hii ilipendelewa na mazingira na historia. Jambo la kwanza, wageni waliotoka mashariki ya kati kifukia hizi janibu zetu Afrika ya mashariki walikaribishwa vizuri na hawa wangozi. Wakaingilia wageni na wenyeji kindakindaki, kidini, kitawala, kibiashara na kitamaduni kwa jumla. Punde si punde wangozi, ambao baadaye walijulikana kama waswahili na wageni hawa, wakaelimika katika dini (ya kiisilamu), biashara na mambo ya utawala aina mpya. Lugha yao nayo ikapanuka pale ilipochukua msamiati ya kigeni hususan wa Kiarabu na Kiajemi na kuufanya uwe wake, ili kueleza kwa rahisi zaidi mambo haya mageni katika taaluma za dini, biashara, siasa na hata sayansi kama vile unajimu. Wakati huo, lugha ya Wangozi sasa ikaitwa Kiswahili wala sio kiangozi. Tatizo hapa ni kuwa kwa vile Kiswahili kilichukua msamiati mwingi wa kigeni ili kuelezea taaluma hizi mpya, baadaye kimekujashukiwa kwamba ni lugha ya kigeni ilhali ni lugha ya Kiafrika asilia, na kitovu chake ni nchi mpya za kiafrika ziitwazo Kenya na Somalia hii leo. (a) Thibitisha kuwa Kiswahili kimekuwa lugha ya kimaitaifa ( maneno 35 – 40) (b) Eleza kwa ufupi asili ya Kiswahili hadi kuja kwa wageni ( maneno 20 – 25) (c) Ukitumia maneno yako mwenyewe, eleza ujumbe uliomo katika aya ya mwisho

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa katika uzalishaji mimea na uvunani. Imesemekana ya kwamba, ghairi ya wivu na kijicho baina ya jamii mbalimbali ulimwenguni, aina hii ya sayanzi ina uwezo na kuangamiza kabisa janga la njaa katika sayari hii yetu. Kivipi? Rahisi kabisa. Ni kwamba mbegu moja tu ya aina yoyote ya mmea, baada ya kuneemeshwa vyumba vyake vidogo ambavyo ndivyo hasa msingi wa uhai vinaweza kunyunyiziwa dawa maalum ili vitawanyike mara hata mamilioni na kuwa mimea kamili…. Mamilioni! Sayansi hii tarari inatumiwa kukuza viazi na vyakula vingine. Hii ina maana ya kwamba mashamba makubwa si muhimu siku hizi, yaani vyakula vingi kabisa vinaweza kukuzwa mahali padogo sana. Kwa hivyo hivi karibuni tu, kutakuwa hakuna haja ya kupigania mashamba. Vyema. Hebu sasa tuangalie zilizokwishapigishwa hii sayansi ya “kutumbisha” na mahali binadamu alipofika kimaendeleo kwa sababu ya hatua hizo. Jambo la kwanza sayansi hii tayari imeshatumiwa kuzalishia wanyama wengi, wengi sana wadogo wadogo kwa lengo la kuendeleza mbele utafiti. Kufikia sasa, wanyama hawa waliotengenezwa na binadamu katika maabara yake bado wanahifadhiwa mumo humo walimotengenezwa. Hii ni hatua kubwa na binadamu anastakili pongezi kwa jinsi anayotumia akili yake kuvumbua ibura hizi zote. Hata hivyo imesemwa kwamba kuchamba kwingi ni kuondoa mavi. Binadamu kama ijulikanavyo, anajaribu sana jujitakasa kwa kujitenga mbali sana na asili yake ya unyama ili aufikie ubinadamu mkamilifu. Hapana ubaya hapo. Lakini tukirudi nyuma tunakuta ya kwamba binadamu sasa aneingia tama kubwa sana kuliko wakati wowote ule. Tamaa hii imeletwa na ujuzi wake katika sayansi hii ya “kutumbisha.” Sasa binadamu ana jua vizuri sana kwamba kwa vile ana ujuzi wa kutengeza panya na hata kondoo katika maabara basi hata ujuzi wa kutengeneza binadamu pia anao! Na hapo ndipo tatizo lilipo. Swali hi hili: Je, ujuzi huu utatufikisha wapi? Na kikomo chake kitakuwaje? Binadamu sasa ujuzi wake unamtia wasiwasi. Wataalam wa sayansi hii wamejiuliza mara nyingi nini kitakachotokea ujuzi huu utakapomilikiwa na mwenda wazimu mweledi.” Watu kadha wa kadha, miongoni mwao wakiwa wanasiasa wamejiuliza mara zisizohesabika swali hili: kama Hitler angekuwa na ujuzi huu, angekuwa na lazima gani ya kuwaulia mbali wayahudi milioni sita wasiokuwa na hitia isipokuwa na nywele nyeusi na hawakuwa weupe sana kama wazungu? Hitler aliamini ya kwamba “mtu mzuri” ni mwenye pua ya upanga (kama mzungu), macho ya buluu nywele rangi ya dhahabu na mwenye kimo cha futi sita au zaidi kidogo. Hivyo lengo lake lilikuwa ni kubuni taifa la watu wazuri pekee ambao mwisho watautawala ulimwengu na kuenea duniani kote. Katika mpango wake, watu weusi wote wangefaa kuangamizwa tu ili watoe nafasi kwa watu aliowaona yeye kuwa bora. Sasa baada ya sayansi hili ya “kutumbisha” kuvumbuliwa, wataalam wametishika sana. Wamewaza jinsi ambavyo Hitler angeweza kufanya kama angekuwa mjuzi wa taaluma hiyo. Kitisho hiki kimezidi kuwatwanga wataalam na wasiokuwa wataalam hivi majuzi tu ilipogunduliwa maiti ya msichana wa miaka kumi na mine huko milima ya Andes, Amerika ya kusini. Msichana huyo alikuwa ametolewa kafara miaka karne tano zilizo pita lakini hakuoza kwa sababu ya baridi kali ya barafu milimani. Kwa sababu ya dukuduku la uvumbuzi ambalo haliishi dhana za kiajabu ubongo wa binadamu, wataalamu wa “kuchezea” maumbile walipomwona msichana huyo maiti, upesi upesi wakampima. Walipofanya hivyo wakagundua ya kwamba mayai yake ni timamu kabisa wala hayajaharibiwa na mpito wa karne. Papo hapo wengine wakajiwa na wazo la kuyatoa mayai hayo na kuyahifadhi kwenye mabara. Tamaa ikazidi zaidi ya zaidi. Baadhi ya wataalamu wakajiwa na wazo la “kuyaneemesha” mayai hayo na mbegu za uzazui za wanaume. Kwa lengo gani? Kuunda watoto amabo mama yao alikufa zamani za kale ili waonekane watakuwa watu wa aina gani! Sasa fikiria mwenyewe! Watoto hawa wa maabara wakiwa weledi zaidi ya binadamu yeyote yeyote wa kisasa lakini watiifu kama mbwa na paka itakuwaje? Hakuna atakayefikiria “kutumbisha” ili tuwe na vijitumwa vyetu vipenzi majumbani mwetu vinavyofanana nasi badala ya paka na mbwa wasiovishwa nguo? (a) Andika kichwa kifaacho kwa nakala hii (b) Kutumia sayansi ya “kutumbisha” kunaweza kumsaidia binadamu kuangamiza mabaa gani mawili yanayomkabili sasa? (c) Unadhani ni kwa nini wanyama waliozalishwa kwa kutumia sayansi hii bado wamo maabarani? (d) Fafanua methali “kuchamba kwingi nikuondoka na mavi” kulingana na muktadha wa habari hii (e) Kuna ubaya gani kutumbisha watu? (f) Mwandishi anaonekana kutishwa sana na uwezekano wa sayansi ya kutumbisha kuishia mikononi mwa “wendawazimu weledi” kwani kuna hatari gani? (g) Eleza kwa ukamilifu matatizo yanayoweza kuukumba ulimwengu iwapo mayai ya msichana wa Andes yatatumbishwa

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina moja na neno: imani(Solved)

    Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina moja na neno: imani

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya sarufi - Kiima - Wakati - Kirejeleo - Kiswahili kitendwa - Kitenzi(Solved)

    Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya sarufi - Kiima - Wakati - Kirejeleo - Kiswahili kitendwa - Kitenzi

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Mahali palipohamwa panaitwa?(Solved)

    Mahali palipohamwa panaitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo (i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka (ii) Juma alifagia chakula (iii) Sisikii vizuri(Solved)

    Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo (i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka (ii) Juma alifagia chakula (iii) Sisikii vizuri

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha Riziki kama ajali huitambui ijapo(Solved)

    Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha Riziki kama ajali huitambui ijapo

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja Kuramba kisogo Kuzunguka mbuyu(Solved)

    Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja Kuramba kisogo Kuzunguka mbuyu

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli kifaacho (i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia (ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge (iii) Hamisi amekata nyasi vizuri...(Solved)

    Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli kifaacho (i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia (ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge (iii) Hamisi amekata nyasi vizuri (iv) Jiwe lile liliangukia matunda

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Sahihisha bila kubadilisha maana: (i) Usikuje hapa kwetu kwani sitakuwamo (ii) Basi la shule imeharibika moshi nyingi inatokea dirishani na maji inatiririka ovyo(Solved)

    Sahihisha bila kubadilisha maana: (i) Usikuje hapa kwetu kwani sitakuwamo (ii) Basi la shule imeharibika moshi nyingi inatokea dirishani na maji inatiririka ovyo

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika katika kauli ya kutendesha (i) Nataka upike chakula hiki vizuri (ii) Toa ushuru wa forodhani(Solved)

    Andika katika kauli ya kutendesha (i) Nataka upike chakula hiki vizuri (ii) Toa ushuru wa forodhani

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo (i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini (ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto(Solved)

    Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo (i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini (ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika katika msemo wa taarifa Mzazi: Kesho nataka ufike nyumbani mapema, unasikia? Mtoto: Nitajaribu, lakini mwalimu alisema tutafanya mtihani jioni(Solved)

    Andika katika msemo wa taarifa Mzazi: Kesho nataka ufike nyumbani mapema, unasikia? Mtoto: Nitajaribu, lakini mwalimu alisema tutafanya mtihani jioni

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Vijana wengi wake kwa waume, walikuwa ndio tu wakamilishe shughuli ya kusajiliwa chuoni. Walikuwa bado nadhari zao zimetekwa na ugeni, hawajapata starehe...(Solved)

    Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Vijana wengi wake kwa waume, walikuwa ndio tu wakamilishe shughuli ya kusajiliwa chuoni. Walikuwa bado nadhari zao zimetekwa na ugeni, hawajapata starehe akilini mwao wala kujisikia wamekaribia kama kwao nyumbani. Kwa hakika mazingira yale mapya yalikuwa yanawapa kiwewe kidogo au tuseme hata woga kiasi. Kusema kweli, kwa wakati ule walikuwa hawajui ni maisha ya namna gani yanayowasubiri mahali pale. Hawakuweza kukadiria kwa uyakinifu wowowtw iwapo makaazi yao pale ya miaka mine mizama kuanzia wakati ule, yangekuwa ya utulivu na raha au pengine yangeondokea kuwa ya roho juu juu na matatizo chungu mzima. Wamsubiri mkuu wa Chuo aingie wamsikize atakalosema, kisha ndipo waweze kubashiri vyema mkondo wa maisha yao utakavyokuwa. Lakini jinsi walivyosubiri Mkuu wa chuo aingie ukumbini ndivyo wayo wayo lao lilivyozidi kuwacheza shere. Waliwaza: Ugeni jamani kweli ni taabu. Mawazo mengi yaliwapitia bongoni mwao. Wakawa kinywa ukumbi mzima, kama kwamba wamekuja mazishini badala ya kuja kusoma. Waliwaza na kuwazua. Waliona au pengine walidhani kuwa hapa kila kitu ni tofauti. Wanafunzi hawa waliona tofauti nyingi kati ya mambo pale chuoni na yale waliyokuwa wameyazoea. Kwa mfano, mwalimu mkuu hapa hakuitwa ‘ headmaster’ kama kule katika shule za msingi na vile shule za upili aliitwa ‘ vice – chancellor’ Nyumba za kulala hazikuitwa ‘dormitory’ au ‘mabweni’, kama walivyozoea, bali ziliitwa ‘ halls’ kwa sababu sio kumbi za aina yoyote ile, bali ni nyumba hasa, zenye vyumba vya kulala, kama walivyozoea kita walipokiwa shule zao za upili huko, bali hapa wenyewe wenyeji waliita kwa majina mengine kabisa! Mara University, mara zutafindaki, mara Ndaki kwa ufupi, mara Jamahiri ya na kadhalika na kadhalika! Waliwaza: kweli mahali hapa wenyewe wenyeji waliita kwa majina mengine kabisa! Mara kumzubaisha mtu hadi kufikia kiwango cha kuonekana kama zuzu! Hata hivyo hawakuvunjika moyo, bali walipiga moyo konde wakanena kimoyomoyo: Potelea mbali! Ukiyavulia nguo, yaoge! Walikuwa wamo katika hali ya kurandaranda katika ulimwengu wa mawazo pale katika ulimwengu wao mpya, ulimwengu mwingine kabisa usioafanana hata chembe na ule waliouzoea, mkuu wa chuo alipoingia. Kuingia mkuu wa chuo wote walisimama kwa pamoja na kwa mijiko, wamekauka kama askari katika gwaride. Kuona hivyo, mkuu wa chuo akwaashiria wakae tu, bila kujisumbua. Kicheko kikawatoka bila kukosa adabu na heshima, kasha wakakaa kwa makini ndio mwanzo wakajisikia wamepoa. Kuona kuwa sasa wametulia na wamestarehe. Mkuu wa chuo akaanza kwa kuwaamkua kisha akawajulisha kwa wakuu wote wa vitivo mbali mbali na idara mbali mbali waliokuwa wamekaa pale jukwani alipo yeye upande huu na huu. Kufikia hapo, alaka ikawa imeungwa baina ya wenyeji na wageni wao. Kila mtu akaona mambo yamesibu tena; huo bila shaka ni mwanzo mwema, na kama ilivyosemwa na wenye busara, siku njema huonekana asubuhi. Hii, Kwa wote ndiyo asubuhi tu, bali ni asubuhi njema, si haba. (a) Ukirejelea aya ya kwanza na ya pili, eleza wasiwasi wanafunzi waliokuwa nao wakati wakisubiri (maneno 45- 55) (b) Ni mambo gani mageni wanafunzi hawakuyazoea yanayoelezwa katika kifungu (maneno 25 – 30) (c) Bila kubadilisha maana, fupisha aya tatu za mwisho kwa kutumia maneno yako mwenyewe. Tumia maneno 40 -45

    Date posted: June 27, 2019.  

  • UFAHAMU Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo tahadhari. Mathalani insiya amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na...(Solved)

    UFAHAMU Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo tahadhari. Mathalani insiya amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na hata kuchafua mito kutokana na maji machafu kutoka viwanda hivyo. Takataka zinazotupwa ovyo ovyo zinarundikana kila mahali. Isitoshe miti inakatwa vivyo hivyo bila simile. Matokeo ya haya yote ni kwa mfano tunapata mvua ya asidi ambayo huhasiri mimea. Aidha nao ukanda wa ozoni unaotukinga dhidi ya miali hatari kutoka kwa jua umeharibiwa tayari na hivyo kuongeza joto duniani. Sehemu nyingi zimeanza kugeuka na kuwa jangwa huku sehemu zingine zikifurika kwa maji ya mito na mvua. Maji haya yameanza kumeza visiwa vingi vilivyo baharini. Kutokana na madhara haya, binadamu sasa anatapatapa ili kutafuta makao kwingine kwenye salama. Ndiposa siku hizi nadhari za binadamu zimeelekezwa katika mawanda mengine nje kabisa ya kisayari hiki kidogo kiitwacho dunia. Kwa miaka mingi sasa binadamu amekuwa akitafakari uwekano wa kuishi katika sayari nyingine. Hii ndiyo sababu mwaka wa 1969 waamerika walimkanyagisha binadamu wa kwanza kabisa mwezini. Lengo lilikuwa ni kutalii na kuchunguza uwekano wa binadamu kuishi huko ili wale watakaoweza wahamie huko, hata mimea. Mwezini ni vumbi tupu lisiloota chochote. Kipatikanacho kwa wingi sana ni madini tu ambayo hayawezi kufaidi binadamu kwa lolote. Sayari nyingine alizozitalii binadamu ni Zuhura, Mirihi, Mushtara na tuseme karibu zote zinazolizunguka jua. Kilichogunduliwa ni kuwa upo uwezekano wa sayari kama Zuhura na pengine Mirihi kuwa na mvua, lakini nyingi mno isiyoweza kuruhusus mimea kukua. Sit u, zuhuria inasemekna kuwa joto sana wakati wa mchana ilhali Mirihi ni baridi sana siku zote; baridi kiasi cha kuuwa binadamu na wanyama hawawezi kuishi huko. Mushtara yasemekana kuwa joto ajabu, ambapo hizo sayari nyingine zina joto sana au zina baridi sana. Habari hii imemfunga binadamu katika jela ya kijisayari chake kiki hiki kiitwacho dunia anachokichafua uchao. Je, binadamu amekata tama? Hata kidogo! Ndio mwanzo anajaribu sana kuzikata pingu alizofunzwa na maumbile. Vipi? Amejaribu kuchunguza uwezekano wa kuihama ardhi na kuishi baharini, kwa sababu bahari inazidi ardhi mara tatu kwa ukubwa. Na ni vipi binadamu anadhani anaweza kuishi baharini mahali ambapo hakuumbwa aishi humo kama samaki? Jawabu ni kuwa angefanya hivyo kwa kutumia maarifa yake. Binadamu anaamini kabisa kuwa ana uwezo wa kujenga miji mikubwa mikubwa humo humo baharini… mikubwa zaidi yah ii tuliyo nayo ardhini. Anaamini ya kuwa anaweza kuitawala bahari kiasi alichitawala ardhi, na hivyo basi kufanya bahari impe makao na kumlisha bila ya kuyabadilisha maumbile yake. Na iwapo hili halitawezekana basi, ikiwajibika, abadilishe maumbile yake kwa kujiunda mashavu kwa mfano, ili avute pumzi ndani ya maji Njia ya pili ya kuepukana na pingu za maumbile ni kuishi angani. Hii ina maana ya kujenga miji iliyoelea angani, kama madungu vile. Na kwa vile anga haina kikomo, binadamu atakuwa amejipatia visayari vyake visivyo idadi ingani! Njia ya tatu ni kubadilisha umbo lake ili asihasirike na joto wala baridi. Binadamu wa kisasa anaamini kuwa inawezekana kumuunda upya mtu katika maabara badala ya katika mamba. Mtu huyu wa maabra, aitwaye ‘cyborg’ kwa lugha ya Kiingereza, anaweza kuwa na chuma ndani badala ya mifupa, na mwili wa kawaida wa udongo na maji nje. Kiunde huyu atakuwa hadhuriki ovyo ovyo kama binadamu wa sasa aliyeumbwa kwa chumvi, maji na protini. Au bora zaidi, binadamu mpya wa maabarani aundwe kwa zebaki. Binadamu huyu wa zebaki hafi wala hakatikikatiki. Na iwapo atakatika vipande vipande, basi kama zebaki hivyo vitaundika tena upya na kumrudishia umbo la awali kamili. Njia nyingine ya kuepukana na uangamizi ni kutumia viunde vyake vya electroniki kama vile tarakilishi yaani kompyuta, na mitambo mingine kama iyo. Binadamu anaamini kwamba uwezo wa vyombo hivi utakapokamilishwa, basi vitamsaidia kwa lolote lile. (a) Inasemekana kwamba binadamu anakichafua hiki kisayari chake kila uchao. Kwa kutumia mifano mitatu, eleza vile binadamu amechafua mazingira yake. (b) Kwa nini ongezeko la joto limeleta jangwa duniani wa wakati huo huo likaleta mafuriko? (c) Eleza sababu mbili zinazomfanya binadamu kuhangaika na kutafuta makao kwingine (d) Ni mambo gani yanayomfunga binadamu katika ardhi. Taja mawili (e) Unadhani ni kwa nini madini mengi yaliyoko mwezini hayaletwi duniani. Taja na ufafanue sababu mbili (f) Kulingana na aya mbili za mwisho, eleza jambo ambalo binadamu anajaribu kukwepa (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu (i) Mashavu (ii) Madungu (iii) Asihasirike (iv) Kiunde

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha (i) Ali hapo (la) (ii) Ali hapo (fa) (iii) Ali hapo...(Solved)

    Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha (i) Ali hapo (la) (ii) Ali hapo (fa) (iii) Ali hapo (oa)

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama(Solved)

    Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama

    Date posted: June 27, 2019.