Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Andika katika msemo wa taarifa “Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona”, Kamau alimwambia shangazi yake(Solved)

    Andika katika msemo wa taarifa “Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona”, Kamau alimwambia shangazi yake

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika katika msemo halisi Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni(Solved)

    Andika katika msemo halisi Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina tunaweza kuunda vitenzi. Mfano Jina ...(Solved)

    Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina tunaweza kuunda vitenzi. Mfano Jina Kitendo Mwuzaji Uza Mauzo Uza Wimbo Imba Sasa kamilisha: Jina Kitenzi (i) Mnanda (ii) Kikomo (iii) Ruhusa (iv) ashiki (v) husudu

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu (i) Ngome (ii) Mitume (iii) Heshima (iv) Ng’ombe (v) Vilema(Solved)

    Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu (i) Ngome (ii) Mitume (iii) Heshima (iv) Ng’ombe (v) Vilema

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza kazi ifanywayo na (i) Mhariri (ii) Jasusi(Solved)

    Eleza kazi ifanywayo na (i) Mhariri (ii) Jasusi

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Akifisha kifungu kifuatacho Bwana mwenyekiti wetu wa leo wazazi wote na hata wanafunzi leo ni siku muhimu je mngependa niwafahamishe msaada tuliopokea kutoka kwa wizara ya elimu(Solved)

    Akifisha kifungu kifuatacho Bwana mwenyekiti wetu wa leo wazazi wote na hata wanafunzi leo ni siku muhimu je mngependa niwafahamishe msaada tuliopokea kutoka kwa wizara ya elimu

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi (i) Kula uyundo (ii) Kula uhondo(Solved)

    Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi (i) Kula uyundo (ii) Kula uhondo

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za Mlazo (i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba (ii) Huyu ni mtu mwenye busara (iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za Mlazo (i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba (ii) Huyu ni mtu mwenye busara (iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Eleza maana ya sentensi hizi (i) Mikono yao imeshikana (ii) Mikono yao imeshikamana(Solved)

    Eleza maana ya sentensi hizi (i) Mikono yao imeshikana (ii) Mikono yao imeshikamana

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo (i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi (ii) Weka mizigo kwa gari(Solved)

    Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo (i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi (ii) Weka mizigo kwa gari

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.” Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi...(Solved)

    Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.” Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi tukianza kuchunguza maisha ya vijana wa siku hizi katika jamii zote, hasa zile za Afrika. Kwa upande mmoja, maisha ya vijana hawa yanaonyesha cheche ya matumaini kwa maisha ya siku za usoni kwa sifa zao za mori na kupenda kujaribu na kushika mambo upesi kama sumaku. Lakini kwa upande wa pili, tunashuhudia upotevu wa kimawazo na hulka ambayo ndiyo kipingamizi cha kuendelea kwao kama raia wa kutegemewa. Kuwanyeshea vijana lawama na kashifa za kila aina hakufai wala hakufui dafu katika juhudi za kuwaongoza na kuwalea. Kwa hili hatuna budi kusadiki, “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Basi hivyo badala ya kuwashambulia vijana wenyewe. Tutafanya hivyo kwa imani kuwa “mwiba uchomeako ndiko utokeako.” Kiini cha matatizo ya vijana wa leo ni namna ya mwongozo na vielezo wanavyopokea kutoka kwa wazazi, waalimu, viongozi wa kijamii wakiwemo pia wale wa medhehebu tofauti na hasa kutokana na vyombo tofauti vya habari: vitabu majarida, filamu, magazeti na kadhalika. Jamii ina haki gani kuwashtumu vijana iwapo mzazi, tangu utotoni mwao amewahubiria maji na huku mwenyewe anakunywa mvinyo? Kama fasihi na maandishi mengine wanayoyabugia vijana yamejazwa amali, picha, jazanda na taswira zinazohimidi ugeni na kutweza Uafrika, tutashangazwa na nini pale vijana watakapoanza kupania zile zile amali za ugenini? Iwapo jamii na mazingira wanamokulia vijana yanatukuza kitu kuliko utu. Hatupaswi kupepesa macho na kukonyeza tunapowaona vijana wakihalifu sheria zote kwa tamaa ya kujinufaisha binafsi. Ni hoja isiyopingika kuwa kulea sio tu kulisha na kuvisha au kumpeleka mtoto shuleni sharti itambulike wazi wazi kuwa sehemu kubwa ya elimu na mwongozo unaoathiri mienendo ya jijana na watoto haitokani na yale waambiwayo bali hasa yote wanaoyashuhudia kwa macho na hisia zao. (a) Katika aya ya kwanza, maisha ya vijana wa kisasa yameelezwaje? (b) Kwa nini vijana hawapaswi kulaumiwa kulingana na mwandishi Maneno 30 – 35 (c) Eleza sifa za malezi bora (Maneno 20 – 25)

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo Kisha Ujibu Maswali Zamani sana na hata hivi karibu watu wengi kote duniani walikuwa wakiamini kuwa kuna ardhi na mbingu tu basi. Imani hii...(Solved)

    Soma makala yafuatayo Kisha Ujibu Maswali Zamani sana na hata hivi karibu watu wengi kote duniani walikuwa wakiamini kuwa kuna ardhi na mbingu tu basi. Imani hii ilijikita katika mantiki inayosema kwamba ardhi au dunia ipo katikati ya maumbile yote na isitoshe, ni tambarare. Juu ya ardhi ni mbingu ambayo imejaa vimulimuli vidogovidogo sana viitwavyo nyota. Baina ya vimulimuli vipo viwili vikubwa viitwavyo mwezi na jua. Hivi viwili japo ni vikubwa kuliko vingine, bado ni vidogo kuliko ardhi. Hii ndiyo imani iliyoutawala ulimwengu kwa miaka na miaka, na ikawa imekita mizizi. Lakini jinsi wanajimu walivyozidi kuelimika, waligundua kwamba ukweli wa mambo umejitenga kando kabisa na imani hii Ukweli ni kwamba zima tulionalo la rangi ya samawati nusumviringo juu ya paa zetu za vichwa ni kubwa sana tena. Na si kubwa tu bali lazidi kupanuka. Katika bwaka hili lipanukalo kila uchao mna galaksi nyingi ajabu zisizokadirika. Ndani ya kila galaksi mna nyota mamilioni na mamilioni, malaki na kanui. Imejulikana kuwa nyota hizo japo huonekana kama vimulimuli vidogo sana usiku usiku ni kubwa ajabu. Kadiria mwenyewe! Jua letu ni nyota kubwa sana. Ukubwa wake umezidi wa dunia mara nyingi sana, zaidi ya elfu moja! Basi fikiria juu ya ukubwa wote huo. Imegunduliwa ya kwamba jua ni nyota ndogo sana ikilinganishwa na zingine zilizo katika galaksi yetu tu, licha ya galaksi nyinginezo zilizoko katika bwaka. Na haya sio maajabu peke yake. Wataalam wamevumbua mengi ya kushangaza zaidi. Mathalan, imekuja kufahamika kuwa jua letu ambalo ni nyota, lina sayari tisa zinazolizunguka. Baadhi ya sayari hizi ni Arthi yetu. Zaibaki, Zuhura, Mirihi, na mshitara baina ya tisa jumla. Baadhi ya sayari hizi zina visayari vidogo vinavyozizunguka. Visayari hivi ndivyo viitwavyo miezi. Ardhi yetu ina mwezi miwili ilhali Mshitara ina kumi na miwili! Sayari hizi zote na visayari vyao, au vitoto ukipenda, havitoi mwanga. Nuru ya mwezi na nuru ya hizo sayari zinazolizunguka jua letu inatokana na jua lenyewe. Kwa hakika ni mmeremeto tu unaotufikia sisi kupitia sayari hizi kutoka kwa nyota hii yetu iitwayo JUA. Kama wasemavyo washahili ya Mungu ni mengi. Taswira tuliyo nayo katika maelezo haya yaonyesha jinsi ambavyo mwanadamu licha ya kuwa na akili nyingi, bado hajawahi kuigusia siri kamili ya mungu. Lakini kwa ufupi twaweza kusema hivi. Ikiwa katika bwaka lote kuna galaksi nyingi, bila shaka kwa vile jua ni nyota basi zimo sayari nyingi ajabu zinazozunguka kila nyota au jua kama zipasavyo kuitwa. Kwa vile katika mfumo- jua imo sayari moja yenye viumbe vyenye uhai, binadamu wakiwemo, basi bila shaka katika mifumo- jua mingine katika galaksi yetu zipo sayari zinazofanana na ardhi hii yetu, ambazo sina viumbe vilivyo hai- penginepo watu pia! Wanona maajabu? Na katika magalaksi mengine je? Mambo pengine ni yayo hayo! Kwa hivyo huenda ikawa peke yetu katika bwaka hili; labda tuna viumbe wenzetu ambao hatutakutana nao katika uhai wetu kwa sababu uwezo wetu wa kimaumbile, na vile kisayansi ni hatifu. Lakini, kwa vile mwenye kupanga maajabu hayo yote, yaani Mwenyezi Mungu ni huyo mmoja basi huenda sote tukakutana Ahera. Mungu ni mkubwa (a) Kulingana na habari hii, taja mambo manne ambayo ni imani potovu (b) Kwa kusema “ ukweli wa mambo umejitenga kando” Mwandishi anamaanisha nini? (c) Taja sifa zozote nne za maumbile ya anga zinazopatikana katika habari hii (d) Taja vitu viwili vipatikanavyo katika galaksi (e) Taja sayari mbili ambazo ni kubwa kuliko ardhi (f) Ni ithibati gani iliyotolewa kuonyesha kuwa nyota sio vijataa vidogo? (g) Bainisha nuru aina mbili tuzionazo angani (h) (i) Ni neno gani lenye maana sawa na “anga” ama “upeo” katika habari hii? (ii) Andika neno moja ambalo lina maana sawa na paa kama lilivyotumiwa katika taarifa (i) Mwandishi anaposema kuwa katika magalaksi mengine “mambo pengine ni yayo hayo” anamaanisha nii?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu...(Solved)

    Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu “Tazama maandishi na anwani basi. Shule ya Msingi ya Barungani S.L.P 128 Vuga.”

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni la lazima na linawezekana kabisa, ingawa lina matatizo yake. Jambo linalotakiwa kufanya ni kuchukua wananchi wenye elimu ya juu wakatafsiri fikra za wazalendo katika Kiswahili. Kwa njia hiyo, lugha ya wanachuo itakuwa ndiyo lugha ile ile ya umma Ni jambo la kuepukwa kuwa na lugha mbili ambazo zinasaidia kuwatenga na umma. Wasomi wetu watakuwa wamekaribia umma kwa kutumia lugha iliyozoeleka na umma wenyewe. Jambo linalotutinga ni hili: mara nyingi wasomi wengine waliozoea kutakadamu lugha ya Kiingereza wanapojaribu kuwaeleza watu wengine jambo la kieleimu au kitaalamu, hushindwa kabisa. Wao huchanganya sana maneno ya Kiingereza na Kishwahili hata kufikia kiasi ambacho mtu wa kawaida haelewi chochote. Kwa kuwa wakoloni mamboleo wameelewa kwamba lugha ni kioo cha kuchujia utamaduni, miaka ya hivi karibuni wamejifunza kwa dhati kuliko wakati mwingine kupigania ufundishaji wa lugha zao, hususa, Kifaransi na Kiingereza. Wakati huo wao wanatoa porojo kuwa kugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya watumwa. Kwa mfano, utaona katika maandishi mngi kila wanapoorodhesha lugha kuu za dunia. Kiswahili hakionyeshwi katika hizo. Badala yake wanakiweka kwenye kiwango sawa na Kiganda, Kikikuyu, Kinyamwezi na lugha kadha wa kadha za kikabila. Hiyo ni harakati kubwa ya kudanganya umma na kukivua Kiswahili hadhi yake ilhali lugha hii inatumiwa na zaidi ya watu milioni mia moja wanaosambaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa kutumia hila hii, wao wanasadikisha watu wengi ili wachukulie Kiswahili kama lugha nyimgine ya kikabila. Ndiposa hawa wakoloni mamboleo wanawashawisha baadhi ya watumiaji wa Kiswahili wastawishe lugha za makabila mabalimbali na kuonyesha kwamba umaarufu wa lugha hizo ni sawa na Kiswahili. Hayo bila shaka ni mawazo. Ukweli ulioko ni kwamba mawazo kama haya yawezi keundeleza ukabila. Hata hivyo sharti kueleweka kwamba kusema hivyo si kudhalilisha umuhimu wa kukuza lugha za kikabila. Tusemacho ni kuwa ukuzaji wa lugha hizo ungekuwa na kusidi moja kuu ambalo ni kustawisha Kiswahili kufika ngazi za kimataifa. Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni hili: Wakoloni - mamboleo wanatuonaje tunapokazania Kiswahili? Je, wanaona ni faida kwao au kwetu? Jambo muhimu zaidi ni kutamba jinsi Kiswahili kinavyotuwezesha kuungana na kuwa kitu kimoja. Ni dhahiri kwamba wakoloni mamboleo hawafurahili wanapoona kishahili kikituunganisha. Machoni mwao Kiswahili ni ishara mojawapo ya kujikomboa kwetu kutokana na minyororo yao. Hivi si kusema kwamba hapupaswi kujifunza kiingereza, Kifaranza au Kijerumani, la hasha. Tunachosema ni kwamba tutumie Kiswahili ambacho ni kioo cha utamaduni wetu. (a) Mwandishi amesema nini kuhusu utengano kati ya umma wa wasomi? ( Maneno 30 – 40) (b) Eleza pingamizi zilizowekwa na wakoloni- mamboleo ili kudunisha Kiswahili (maneno 40 – 50) (c) Kulingana na mwandishi ni sababu gani zinazofanya wakoloni mamboleo kupinga maendeleo ya Kiswahili?

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo,...(Solved)

    Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo, mawazo tu bali pia katika kipengele kingine chochote utakachofikiria. Yote haya ni vielezo vya jinsi kizazi cha leo kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha ule wa vizazi vilivyotangulia. Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao basi, si ajabu katu kuwaona vijana wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana ajabu na kudhirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri. Hata hivyo, watu wengi wameonelea kwamba hali ya maisha ya vijana wa leo maasia yanayotokana na utundu na hata ukatili wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi hiki kisingepotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao ambamo wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama waminifu, heshima kwa wazee ama wakuu, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia kujitegemea. Yote haya yamesahaulika ama tuseme yamepuuzwa katika utamaduni wa kisasa.” Swali lilozuka sasa ni je tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au masharti gani? Tuwapige darubini kwa kutegemea hali ilivyo hivi leo duniani ama tuwapime kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini lisije likaegemea upande wowote. Mathalan, ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaothirika na hivyo kubadilika daima. Angalia kwa mfano jinsi maendeleo ya elimu, sayansi, mawasiliano na hata ufundi yalivyoyageuza maisha siku hizi. Yamkini vijana wa barani Afrika wakaona na hata kuzungumza wa wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani bila hata kunyanyuka hapa kwao nyumbani. Athari ya filamu, video, vitabu, magazeti, majarida n.k haikadiriki. Haya kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati wao. Isitoshe, mambo haya yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha kuwa yale wanayojifunza ni kweli. Matokeo yamekuwa ni wao kuudunisha utamaduni wao wa asili na kuupapia ule wa wageni waliowaathiri. Tusisahau kuwa ujana ni tembo la mnazi na rahisi kwao kubadili mawazo. Lakini hatuwezi kuwasamehe vijana wanaokosa akili razini kwa kupotoshwa na kuchacharika na yote, wanayoyapokea kutokea ugenini na hivyo kuanza kudhalilisha utamaduni wa Waafrika. Hata hivyo, badala ya kuwakashifu wanapopotea njia amakuwapongeza wanapotenda yale tunayoyategemea tu, ni wajibu mkubwa wa wazazi kuwaongoza na kuwasaidia vijana kuwa na uwezo mkubwa na kufanya uteuzi mwafaka katika maisha yao. Maswali (a) Kulingana na mwandishi, kundi linalodai kuwa maisha sio jiwe’ lina maoni gani? (b) Kulingana na taarifa uliyoisoma ni jinsi gani vijana wa kisasa wangeziepuka athari mbaya? (c) Kwa mujibu wa taarifa hii, utamaduni wa Kiafrika una manufaa. Yataje (d) Mwandishi anaposema mambo haya yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha vijana kuwa yale wanayojifunza ni kweli anamaanisha nini? (e) Mbali na wazazi, ni makundi gani mengine ya watu ambayo yanapaswa kutoa mawaidha kwa vijana? (f) Kwa maoni yako vijana wanapaswa kufanya uteuzi wa namna gani katika mvutano huu wa tamaduni? (g) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika makala (i) Maasia (ii) Razini (h) Andika methali moja ambayo inaafiki taarifa hii

    Date posted: June 27, 2019.  

  • Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani(Solved)

    Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani.

    Date posted: June 15, 2019.  

  • Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake(Solved)

    Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake.

    Date posted: June 9, 2019.  

  • Taja aina mbili za ala(Solved)

    Taja aina mbili za ala

    Date posted: June 9, 2019.  

  • Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.(Solved)

    Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.

    Date posted: May 14, 2019.  

  • Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo(Solved)

    Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo

    Date posted: May 14, 2019.  

  • Eleza dhima mbili ya kiimbo(Solved)

    Dhima ya kiimbo

    Date posted: May 14, 2019.  

  • Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata(Solved)

    Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata.

    Date posted: May 14, 2019.  

  • Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?(Solved)

    Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?

    Date posted: May 14, 2019.  

  • Taja na ueleze dhima tano ambazo sajili za lugha hutekeleza(Solved)

    Dhima ambazo sajili za lugha hutekeleza

    Date posted: May 14, 2019.  

  • UFAHAMU Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea...(Solved)

    UFAHAMU Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa yanayoendelea na yaliyoendelea inaendeiea kuongezeka kila siku. Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika tatizo hili. Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu, ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifu huu huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi. Mataifa yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayoendelea kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi husika. Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia wake kutoka kwenye dhiki hii.Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi,kuendeleza elimu inayolenga kutatua matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi kuwa waangalifu ili mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa yaliyoendelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya sera za kiuchumi sharti yauzlngatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya. (a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea. (b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea? (c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika kutatua tatizo la ufukara? (d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea? (e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (i)Turathi za kikoloni (ii) Kuatika (iii) Kuyaburai

    Date posted: May 7, 2019.  

  • MUHTASARI (alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima...(Solved)

    MUHTASARI (alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha. Nchi moja huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yotc hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake, matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake. Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema. Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake naya jamii yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake. Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi kuhasirika mradi taifa lake linufaike. Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa. (a) Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa. (b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70)

    Date posted: May 7, 2019.  

  • Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.(Solved)

    Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.

    Date posted: May 7, 2019.  

  • Tunga neno lenye muundo huu wa silabi: Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu(Solved)

    Tunga neno lenye muundo huu wa silabi: Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu

    Date posted: May 7, 2019.  

  • Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)(Solved)

    Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)

    Date posted: May 7, 2019.  

  • Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye(Solved)

    Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye

    Date posted: May 7, 2019.