Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • (1).Twamshukuru Mwenyezi. Kamwe wingi ukarimu Alo na kiti cha enzi, Mola wetu akramu Kutupa kitu azizi , lugha kutakalamu Lugha ni kitu kitamu, ujuwapo kutumia (2) Lugha mkuu mlezi...(Solved)

    (1).Twamshukuru Mwenyezi. Kamwe wingi ukarimu Alo na kiti cha enzi, Mola wetu akramu Kutupa kitu azizi , lugha kutakalamu Lugha ni kitu kitamu, ujuwapo kutumia (2) Lugha mkuu mlezi , aleaye binadamu Hata wanyama ja mbuzi, wema lugha wafahamu Hafuguwa simulizi, izaayo tabasamu Lugha huwa ni imamu, ujuwapo kutumia (3) Lugha hodari mkwezi, akweaye tata ngumu Huzifyeka pingamizi, zizushazo uhasama Ikazidisha mapenzi, wapendanao kudumu Lugha huyeyusha sumu, ujuwapo kutumia (4) Lugha ndiye mpagazi, mazito kuyahudumu Pia hupanga vizazi, pasi mbari kudhulumu Aidha hufanya kazi, ikawa mustakumu Lugha kwayo ni timamu, ujuwapo kutumia (5) Lugha ni mpelelezi, maovu kuwakasimu Huwatowa palo wazi, kashuhudia kaumu Yasifiwa na wajuzi, kuwa ni kitu adhimu Lugha mkuu hakimu, ujuwapo kutumia (6) Lugha huizuwa kazi, kutatiza mahakimu Huwaacha kanwa wazi, wakili kitakalamu Muhalifu na jambazi, wakaishinda hukumu Urongo huwa timamu, ujuwapo kutumia (7) Lugha iwe ni kiongozi, Kizungu au Kiamu Iwekapo waziwazi, silabi na tarakimu Huyakimu maongezi,yakasikizwa kwa hamu Lugha huwa ni muhimu, ujuwapo kutumia. (8) Lugha ni mapinduzi, wanyonge na wajukumu Kadhalika ni jahazi, ya nahodha muhitimu Kufa maji haiwezi, si vina si miizamu Lugha maji zam-zamu, ujuwapo kutumia (a) Eleza maudhui ya shairi hili (b) Eleza muundo wa shairi hili (c) Andika ubeti wa nne katika lugha ya nadhari/ nadharia (d) Taja huku ukitoa mifano, mbinu tatu za lugha alizotumia mshairi kuwasilisha ujumbe (e) Eleza maana ya msamiati kama ulivyotumika (i) Azizi (ii) Uhasimu (iii) Adimu.

    Date posted: October 9, 2019.  

  • Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani, Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani, Husuda wameikata, hata hawasengenyani, Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani, Wafanya bidii...(Solved)

    Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani, Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani, Husuda wameikata, hata hawasengenyani, Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja Mchwa nao nikaona, wamejenga masikani, Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani, Wao husaidiana, tena hawadanganyani, Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja Nalo jeshi la siafu, hutandawaa njiani, Laenda bila ya hofu, maana ajiamini, Silaha zao dhaifu, meno, tena hawaoni Wa kuwatadia nini ? Kwani wanao umoja. Nao chungu wachukuzi, nyama warima njiani, Masikini wapagazi, mizigo yao kichwani, Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini, Katu hawafarakani, wanadamu kwa umoja. Sisi ni wana Adamu, mbona hatusikizani, Tusitietie hamu, ukubwa kuutamani, Wachache wataalamu, tuwasadi kwa imani, Hii “Huyu awezani,” yatuvunjia umoja (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka. (b) Ni sifa zipi nne zinazopewa wanaozungumza. (c) Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wake katika shairi hili. (d) Eleza muundo wa shairi hili. (e) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (f) Taja mafunzo mawili unayopata kutokana na wahusika wanaozungumziwa. (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hilo. (i) Chungu (ii) Tuwasadi

    Date posted: October 9, 2019.  

  • Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia, Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia! Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia ! Huzunguka akilia kwa maana ya uketo Ndipo mamaye kawaza, pamwe na...(Solved)

    Alipokwenda kwao, mamaye alimwambia, Nipa fedha au nguo, nataka kwenda tumia! Nikosapo hivi leo, nipa kisu tajitia ! Huzunguka akilia kwa maana ya uketo Ndipo mamaye kawaza, pamwe na kuzingatia, Fedha zako umesoza, na leo zimekwisha, Kisu sikukukataza, twaa upate jitia! Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako! Ulipogeuka nondo, nguo ukazingilia, Kakaka kwa vishindo, usisaze hata moya, Leo wanuka uvundo, wambeja wakukimbia! Mbele zangu n’ondokea ! Wende na ukiwa wako! Ukijigeuza nyama, kama Simba ukilia, Watumwa ukawaegema, ukawla wote pia, Pasi kuona huruma, kutoa wahurumia, Mbona hukuzingatia? Wende na ukiwa wako! Si mimi naliokupa, ukata huo, sikia! Kwamba utakuja hapa, nipate kuondolea, Naapa thama, naapa, sina la kukutendea! Mbele zangu n’ondokea! Wende na ukiwa wako! Tamati, nalikomile, ni hayo nalokwambia, Hapahitaji kelele na kujirisha mabaya, Na kwamba yakutukie, sema yapate n’elea! Zidi radhi kuniwea ! Wende na ukiwa wako! (a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (b) Ni maudhui gani yanayojitokeza katika shairi hili (c) Taja na ueleze tabia za mnenewa katika shairi hili (d) Mshairi ametumia uhuru wa utunzi. Taja sehemu mbili alikotumia uhuru huo (e) Eleza umbo la shairi hili (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi :- (i) Uketo (ii) Ukata

    Date posted: October 9, 2019.  

  • KIACHE KINACHONG’AA Katu siwe na harara, wala moyo kukupapa, Usichukue hasira, na moyo kutapa-tapa, Utaharibu na sura, mwishowe uende kapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Mbeleye kina madhara, kile kinachokukukwepa, Mbele...(Solved)

    KIACHE KINACHONG’AA Katu siwe na harara, wala moyo kukupapa, Usichukue hasira, na moyo kutapa-tapa, Utaharibu na sura, mwishowe uende kapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Mbeleye kina madhara, kile kinachokukukwepa, Mbele yake ni hasara, si chema kitakutupa, Hutaipata ijara, kuchuma ama kukopa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Hicho jangwa la Sahara, si mnofu ni mfupa, Hakina njema ishara, humtupa mwenye pupa, Kibovu kama tambara, hupasuka kama chupa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Kitaleta ufukura, si huko wala si hapa, Kina mengi mazingira, na mbele kitakuchapa, Sijitie usogora, ukavimbisha mishipa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Si kazi yenye ujira, mshahara kukulipa, Ya cheo chenye kinara, na heshima wakikupa, Mbele haina imara, japo leo wajitapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Japo kazi ya biashara, kutwa wauza makopa, Uwe mtu na kipara, Mwananchi ama Yuripa, Bora uwe na busara, fedha tajaza mapipa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Usione kinang’ara, huku chapiga marapa, Ukimbilie kupora, moyo wako kukuzipa, Kitakugeuza chura, mbele yake utaapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Usitupe sarara, nyuma kisogo kuipa, Ukaenda kwa papara, kiumbe mbele kitanepa, Kwanza tumia fikira, uchague njema chapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Na sisemi masihara, hakika kweli nawapa Mlio pwani na bara, wa Mufindi na wa lupa Maneno haya kitara, muarifu na Wachepa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara Tamati niliyochora, ya shikeni si kuepa Kisha muwe na basira, na Mola kumuogopa, Kinachokwepa si nyara, ufunge ndani ya kwapa, Kiache kinachokwepa, mbeleye kina madhara (a) Eleza hii ni bahari gani ya shairi (b) Eleza dhamira ya mshairi (c) Fafanua hasara nne zinazoletwa na tamaa - vile ving’aavyo (d) Taja na ueleze mbinu mbili za kifasihi zilizotumika katika shairi (e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi (i) Kuchuma (ii) Kisogo kuipa

    Date posted: October 9, 2019.  

  • 1. Namwona yu shambani, Na jembe mkononi, Analima, Mwanamama,(Solved)

    MWANAMKE 1. Namwona yu shambani, Na jembe mkononi, Analima, Mwanamama, Mavuno si yake, Ni ya mume wake. 2. Namwona viwandani, Pia maofisini, Yu kazini, Hamkani, Anabaguliwa, Na anaonewa. 3. Namwona yu nyumbnai, Mpishi wa jikoni, Yaya yeye, Dobi yeye, Hakuna malipo, Likizo haipo. 4. Namwona kitandani, Yu uchi maungoni. Ni mrembo Kama chombo, Chenye ushawishi, Mzima utashi. 5. Namwona mkekani, Yuwamo uzazini, Apumua, Augua, Kilio cha kite, Cha mpiga pute. 6. Kwa nini mwanamke, Ni yeye peke yake, Heshimaye, Haki anakosa, Kwa kweli ni kosa (Muhammed Seif Khatib) (a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua dai hili kwa kutoa mifano minne (b) Eleza umbo la shairi hili (c) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari (d) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima utoe mifano miwili ya jinsi ilivyotumika (e) Onyesha mifano miwili ya ubabedume inayojitokeza katika shairi hili (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika shairi: (i) mzima utashi (ii) maungoni

    Date posted: October 9, 2019.  

  • KIPI NIKITENDE? Tayari ni sarakani, niambie yote johara,Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira,Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara,Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama?Miezi tisa...(Solved)

    KIPI NIKITENDE? Tayari ni sarakani, niambie yote johara, Mosi nimpe shukrani, kanizaa bira zira, Wapo haiko hisani, ningefaa kwa uparara, Kipi takachokitenda, ni nene heko kwa mama? Miezi tisa tumboni, yote nina kajinyima, Kanikopa uchunguni, safari ndefu kazima’ Kama kinda kiotani, kiniasa huyu mama’ Kipi takachokitenda, ninene heko mama ? Baba siku jana madadi, kawa vingaito mambo, Kaolewa na asadi, kachalazwa kwa wimbombo, Kaona – bali jadili, kuchao puani bombo, Kipi takachokitenda, ninene heko mama? Kila kuchao zarani, kupalilia kondeni, Kachanika mpinini, chungu povuka motoni, Kaviyariya fingani, kinijali jikoni, Kipi tukachokitenda , ninene heko mama? Wa siku hizi vijana, wakahujuru nyumbani, Wengine wao jagina, kawa lofa mutaani, Hali ukashiba nina, afikapo tu, “kongoni!” Kipi takachokitenda, ninene heko mama? Nawe bwana siwe maya, vita hasha kiwa kombo, Tena simfanye yaya, ya kikoa ndio mambo, Simtende ya hizaya, siwe mwao kila jambo, Kipi takachokitenda, ninene heko mama? Sasa jamvi nakuja, kisa nimesakarika, Naomba niliyotaja, tatia manani kaka, Nenayo yasiwe ngoja, ili nipokee baraka, Mema nitamtendea, apate futahi pia. (a) Eleza umbo la shairi hili (b) Kwa nini msanii amshukuru mamaye ? (c) Ni kina nani wanaokashifiwa na msanii ? Kwa nini ? (d) Onyesha tofauti katika ujumbe iliyoko katika beti nne za kwanza na mbili zinazofuata (e) Toa majina mengine yenye maana sawa na haya yaliyotumiwa katika shairi hili : (i) Mama (ii) Dawati (iii) Imara/thabiti (f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika kaika shairi: (i) Kawa vangaito mambo (ii) Wimbombo (iii) Kongoni

    Date posted: October 9, 2019.  

  • 1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti Amefanya nini, la kutetea umati Kipimo ni kipi? 2. Yupi wa maani, asosita katikati Alo na maoni, yasojua...(Solved)

    1. Nitampa nani, sauti yangu ya dhati Kwa kipimo gani, ingawa kiwakatiti Amefanya nini, la kutetea umati Kipimo ni kipi? 2. Yupi wa maani, asosita katikati Alo na maoni, yasojua gatigati Atazame chini, kwa kile ule wakati Kipimo ni kipi? 3. Alo mzalendo, atambuaye shuruti Asiye mafundo, asojua mangiriti Anoshika pendo, hata katika mauti Kipimo ni kipi? 4. Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti Utu uko wapi, ni wapi unapoketi Nje kwa mkwapi, au ndani kwa buheti Kipimo ni kipi? a) Eleza umbo la shairi hili b) Taja na ueleze jinsi mwandishi alivyotumia uhuru wa ushairi c) Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari e) Taja bahari tatu zinazojitokeza katika shairi na utoe sababu f) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi hili i) Katiti ii) Gatigati iii) Mangiriti

    Date posted: October 9, 2019.  

  • 1. Mke wangu wameshanipoka Ndugu zangu, wamedai ububu Wazazi kuzoea kunigombeza(Solved)

    HATIMA YANGU 1. Mke wangu wameshanipoka Ndugu zangu, wamedai ububu Wazazi kuzoea kunigombeza 2. Juzi mali lilimbikiza Furaha lilitanda Makanwa yalijaziwa Hoi hoi ikawa desturi 3. Kilabu tulikwenda Nyama tulichoma Mahali tulizuru Tuliteremsha! 4. Leo mambo yamenigeuka Wao masahibu siwaoni Matumbo yakaninguruma Kama radi ya mvua 5. Nyumbani nimebaki pweke Mke amenitoroka Watoto wameparara Skuli kugharamia Imegeuka balaa belua 6. Ndipo nimeamua Afadhali kitanzi badala ya balaa Kumbe kupanga ndiyo maana Maisha na waasia (a) Eleza mambo muhimu yanayoelezwa katika shairi hili (b) Fafanua sifa mbili za anayezungumza katika shairi (c) Dondoa na ufafanue mbinu zozote mbili za lugha katika shairi hili (d) Eleza maana ya:- (i) Ndugu zangu wamedai ububu (ii) Kumbe kupanga ndiyo maana

    Date posted: October 9, 2019.  

  • WAFULA KABILIANA NA KISU Ee mpwa wangu, Kwetu hakuna muoga, Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo, Fahali tulichinja ili uwe mwanamme, Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu ! Iwapo utatingiza...(Solved)

    WAFULA KABILIANA NA KISU Ee mpwa wangu, Kwetu hakuna muoga, Uoga ukikufikia, huenda ni wa akina mamayo, Fahali tulichinja ili uwe mwanamme, Eewe mpwa wangu, kisu kikali ajabu ! Iwapo utatingiza kichwa, Uhamie kwa wasiotahiri. Wanaume wa mbari yetu, Si waoga wa kisu, Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo, Wewe ndiye wa kwanza, Iwapo utashindwa, Wasichana wote, Watakucheka, Ubaki msununu, Simama jiwe liwe juu, Ndege zote ziangamie. Simu nimeipokea, Ngariba alilala jikoni, Visu ametia makali, Wewe ndiye wangojewa, Hadharani utasimama, Macho yote yawe kwako, Iwapo haustahimili kisu, Jiuzulu sasa mpwa wangu, Hakika sasa mpwa wangu, Hakika tutakusamehe, mwaka kesho unakuja. Asubuhi ndio hii, Mama mtoto aamushwe, Upweke ni uvundo, Iwapo utatikisa kichwa, Iwapo wewe ni mme, Kabiliana na kisu kikali, Hakika ni kikali! Kweli ni kikali! Wengi wasema ni kikali! Fika huko uone ukali! Mbuzi utapata, Na hata shamba la mahindi, Simama imara, Usiende kwa wasiotahiri (a) Hili ni shairi la aina gani ? Thibitisha (b) Ni nani anayeimba shairi hili na analiimba kwa nani ? (c) Toa ithibati kwenye shairi hili kuthibitisha kuwa msimulizi ana taasubi za kiume (d) Taja kwa kutolea mifano mbinu zozote nne za uandishi katika shairi hili (e) Taja shughuli zozote mbili za kiuchumi za jamii inayorejelewa katika shairi hili (f) Eleza kwa mifano, uhuru wa kishairi katika shairi hili (g) Msamiati ufuatao umetumika kwa maana gani katika shairi hili ? (i) Mbari (ii) Msununu (iii) Ngariba (iv) Uvundo

    Date posted: October 9, 2019.  

  • Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani.Afya yangu dhahili, mno nataka amaniNawe umenikabili, nenende sipitaliniSisi tokea azali, twende zetu mizumuniNifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?Mababu hawakujali, wajihisipo...(Solved)

    Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwandani. Afya yangu dhahili, mno nataka amani Nawe umenikabili, nenende sipitalini Sisi tokea azali, twende zetu mizumuni Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani? Mababu hawakujali, wajihisipo tabani Tuna dawa za asili, hupati sipitalini Kwa nguvu za kirijali, Mkuyati uamini Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele fulani Nifuateni sipitali, na dawa ziko nyumbani? Mtu akiwa hali, tumbo lina walakini, Dawa yake ni subili, au zongo huanoni Zabadili pia sahali, kwa maradhi yalo ndani Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani? Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini Daktari k’ona mwili, tanena kensa tumboni Visu visitiwe makali, tayari kwa pirisheni Ukatwe kama fagili, tumbo nyangwe na maini Nifuateni sipitalini, na dawa ziko nyumbani? Japo maradhi dhalili, kutenguliwa tegoni Yakifika sipitali, huwa hayana kifani Wambiwa damu kaliti, ndugu msaidieni Watu wakitaamali, kumbe ndiyo bunani Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani? Mizimu wakupa kweli, Wakueleze undani. Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani Utete huku wawili, wa manjano na kijani Matunda pia asali, vitu vyae shamoni Nifuateni sipati, na dawa zi langoni? (a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka (b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili (c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitalini (d) Eleza umbo la shairi hili (e) Kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi ? (f) Andika maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa kwenye shairi :- (i) Dhalili – (ii) Azali- (iii)Sahali-

    Date posted: October 9, 2019.  

  • Umekata mti mtima Umeangukia nyumba yako Umeziba mto hasira ...................(Solved)

    SHAIRI ‘A’. Umekata mti mtima Umeangukia nyumba yako Umeziba mto hasira Nyumba yako sasa mafurikoni Na utahama Watoto Wakukimbia Mbuzi kumkaribia chui Alijigeuza Panya Akalia kulikuwa na pala Kichwani Mchawi kutaka sana kutisha Alijigeuza Simba Akalia na risasi kichwani Jongoo kutaka sana kukimbia Aliomba miguu elfu Akaachwa na nyoka Hadija wapi sasa yatakwenda Bwanako kumpa sumu ? Hadija umeshika nyoka kwa mkia Hadija umepitia nyuma ya punda SHAIRI ‘B’ Piteni jamani, Piteni haraka Nendeni, nendeni huko mwendako Mimi haraka, haraka sina Mzigo wangu, mzigo mzito mno Na chini sitaki kuweka Vijana kwa nini hampiti ? Kwa nini mwanicheka kisogo ? Mzigo niliobeba haupo. Lakini umenipinda ngongo na Nendako Haya piteni ! Piteni haraka ! Heei ! Mwafikiri mwaniacha nyuma ! Njia ya maisha ni moja tu. Huko mwendako ndiko nilikotoka Na nilipofikia wengi wenu Hawatafika. Kula nimekula na sasa mwasema Niko nyuma ya wakati Lakini kama mungepita mbele Na uso wangu kutazama Ningewambia siri miaka Mingi. (a) Haya ni mashairi ya aina gani ? Toa saabu (b) Washairi hawa wawili wanalalamika. Yafafanue malalamishi yao (c) Onyesha jinsi kinaya kinavyojitokeza katika tungo hizi mbili (d) Ni vipi Hadija :- (i) Amekata mti mtima ? (ii) Amepita nyuma ya Punda (e) Toa mifano 2 ya uhuru wa mashairi kwa kurejelea mashairi haya (f) Kwa kurejelea shairi ‘B’ eleza maana ya:- (i) Mzigo (ii) Siri (iii) Kula nimekula (iv) Niko nyuma ya wakati

    Date posted: October 9, 2019.  

  • Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo! Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu. Mzee Oluoch : Na wangu...(Solved)

    Mzee Oluoch :....................................................................ni kweli hayo! Mzee Mwenda : Ndio. Huyu mtoto wangu nimemsomesha mpaka akahitimu chuo kikuu na anafanya kazi ya uhasibu. Mzee Oluoch : Na wangu amehitimu na sasa ana shahada ya uzamili. Yeye ni mhandisi mkuu. Chukua tu mbuzi hamsini na utukubalie kujenga uhusiano wa ukwe. Mzee Mwenda : Je, mbuzi hao ni wa ‘mfuko’ au ni .......? (a) Mazungumzo ya aina hii hutokea katika muktadha wa aina gani? (b) Eleza sifa nane za lugha inayotumika katika wa aina hii Mzee Oluoch : Kuna wa mfuko ......thelathini na hao wengine ishirini. Mzee Mwenda : Basi lete hao ulio nao. Wengine hamsini watabaki deni. Utakuwa ukinilipa polepole. Idhini yangu nimetoa ili mipango iendelee.

    Date posted: October 9, 2019.  

  • AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways! SHIKU : Namba nane ngapi? AZIZ : Mbao ingia, blue. SHIKU : Nina hashuu. AZIZ...(Solved)

    AZIZ : Ingia 46! Adams mbao Kenyatta, railways beba! 46 Adams mbao kenyatta, railways! SHIKU : Namba nane ngapi? AZIZ : Mbao ingia, blue. SHIKU : Nina hashuu. AZIZ : Blue Auntie. SHIKU : Sina. AZIZ : Ingia. 46 Adams mbao, kenyatta railways gari bebabeba. AHENDERA : Mimi sinako shirini. Chukuako tu kumi. AZIZ : Dinga inakunywanga petrol mzee. AHENDERA: Kumi mingi. AZIZ : Haaya ingia twende. Driver imeshon twende. (i) Eleza muktadha wa mazungumzo haya (ii) Taja sifa sita za lugha iliyotumika katika mazungumzo haya

    Date posted: October 9, 2019.  

  • Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili(Solved)

    Eleza juhudi tano zinazotumika kukiendeleza Kiswahili

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya.... (a) Hii ni sajili gani? (b) Eleza...(Solved)

    Bw. Mosuka : Mheshimiwa spika, naichukua fursa hii kuipinga hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Mahira, mheshimiwa Kochaberi kuhusu suala la kuavya.... (a) Hii ni sajili gani? (b) Eleza sifa za mazungumzo ya sajili hii

    Date posted: October 8, 2019.  

  • A : Ohh, dada NaomiB : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe!A: Asifiwe sanaB: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuonaA: dada wee...Nilitumwa huko kusini...(Solved)

    Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali : A : Ohh, dada Naomi B : Dada Ruth (anamsogea kwa bashasha wanakumbatiana). Ahh Mungu asifiwe! A: Asifiwe sana B: Ehh dadangu, miezi ...mingi...sijakuona A: dada wee...Nilitumwa huko kusini ...Kuwahubiria watu injili (mtuo mdogo)singeweza kukata... B: Ehh, usiwe kama Yona A: Habari ya siku nyingi? B; Nzuri Mungu bado ameendelea kunibariki A: Amen! B: Nimeendelea kuiona neema yake A: Amen! Asifiwe Bwana B: Halleluya A: Ni Mungu wa miujiza! B : Amen. Hata nami nimeona neema yake Bado niko imara katika wokovu katika siku hizi za mwisho A : Amen ! B : Ni Mungu wa ajabu kweli ! A : Nilikumbana na matatizo lakini nikategemea sala Kama Paulo na sila… Na nikashinda (anatua). Sikuweza kumpa shetani nafasi…maana ameshindwa B : Ameshindwa kabisa (i) Hii ni sajili ya wapi ? Fafanua (ii) Taja na ueleze sifa za sajili hii (iii) Taja na ueleze mambo mawili muhimu yaliyosaidia katika maenezi ya Kiswahili Afrika mashariki na kati

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo, mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:- Niaje wasee! Ma-holiday ndizo hizo tena. Najua ma-mission ni mingi! Lakini jo, mambo imebadilika ! Ni kubaya maze. Usifikirie kila kitu unaona ni reality, ukadhani ni gold ! Hiyo siyo real life maze ! Round hii maze ni ‘‘Ku-chill!’’ Usipige ma-stunts zingine zitakuacha uki-regret later! NI POA KU- CHILL au aje maze? a) Bainisha rejista ya mazungumzo haya b) Kwa kurejelea kifungu andika sifa za rejista hii. c) Kwa nini watu hutumia lugha zaidi ya moja. d) Orodhesha hatua tatu zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha matatizo yanayokumba Kiswahili nchini.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili(Solved)

    Fafanua changamoto tano zinazozuia maenezi ya haraka ya lugha ya Kiswahili

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya(Solved)

    Fafanua mikakati mitano inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa kiswahili nchini Kenya

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kuwa anasumbuliwa na uto mwingi mwilini. Uto unaweza kudondoshwa kwa kufanya mazoezi, kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na hata protini. Protini iwapo nyingi mwilini hugeuzwa kuwa glukosi ambayo huhifadhiwa mwilini. Hii huwa msingi wa unene pia ambao unahatarisha afya. Jamaa yake aliyeaga dunia alikuwa mgonjwa wa bolisukari ambayo inaweza kurithishwa. Kimsingi, lazima awe na welewa bora kabisa wa lishe. Mwenzake naye aliathiriwa na aflatoxins zilikuwa kwenye chakula alichokula. (a) Sajili hii inapatikana wapi? Kwa nini? (b) Taja sifa zinazohusishwa na sajili yenyewe

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.(Solved)

    Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Saidi : Hallo............Hallo....Huyo ni Bw. Mohamed?Mohamed : Ndio...uko wapi...Saidi : Shuleni...sasa...ulinifikishia ujumbe?Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwaSaidi : Sina credit. Nipigie tafadhali.Mohamed : Sina...(Solved)

    Isimu Jamii Saidi : Hallo............Hallo....Huyo ni Bw. Mohamed? Mohamed : Ndio...uko wapi... Saidi : Shuleni...sasa...ulinifikishia ujumbe? Mohamed : La. Parade ilikuwa imehitimishwa Saidi : Sina credit. Nipigie tafadhali. Mohamed : Sina pia, nitatuma sms Saidi : Iwe saa hii eh? Mohamed : Baada ya dakika tano Saidi : Good day Mohamed : Welcome (a) Taja na uthibitishe sifa zinazojitokeza katika mazungumzo haya (b) Eleza sababu za wazungumzaji kutumia mbinu zifuatazo katika mazungumzo yao (i) Mdokezo (ii) Lugha mseto

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Nomino zifuatazo ni za ngeli gani? i) Nzi ii) Soksi(Solved)

    Nomino zifuatazo ni za ngeli gani? i) Nzi ii) Soksi

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo Soroveya atapimia wanunuzi viwanja.(Solved)

    Bainisha aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo Soroveya atapimia wanunuzi viwanja.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu. Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa(Solved)

    Changanua sentensi ifuaatayo kwa kielelezo visandu. Mwanafunzi aliyeleta kitabu chake amepongezwa

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Eleza na udhibitishe kwa mfano, matumizi mawili ya tu.(Solved)

    Eleza na udhibitishe kwa mfano, matumizi mawili ya tu.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Kanusha sentensi hii;- Ukionana naye mwambie aje anione.(Solved)

    Kanusha sentensi hii;- Ukionana naye mwambie aje anione.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Andika sentensi ifuatayo katika wingi wa udogo.Mtu mchoyo hamfai mwingine kwa vyovyote vile.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika wingi wa udogo. Mtu mchoyo hamfai mwingine kwa vyovyote vile.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. Juma ameinjika chungu mekoni.(Solved)

    Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. Juma ameinjika chungu mekoni.

    Date posted: October 8, 2019.  

  • Tumia viunganishi mwafaka kuunganisha sentensi hizi ziwe sentensi moja. Alikimbia kwa nguvu zake zote. Alishindwa, kulikuwa na mtu mwenye mbio kumliko.(Solved)

    Tumia viunganishi mwafaka kuunganisha sentensi hizi ziwe sentensi moja. Alikimbia kwa nguvu zake zote. Alishindwa, kulikuwa na mtu mwenye mbio kumliko.

    Date posted: October 8, 2019.