Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Questions and answers: Kiswahili

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

2287 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Muhtasari Sikukuu ya wafanyikazi huadhimishwa na wafanyikazi kote ulimwenguni kwa minajili ya kukumbushana na kutanabahishana umuhimu wa mshikamano na umoja katika kudai na kutetea maslahi na...(Solved)

    Muhtasari Sikukuu ya wafanyikazi huadhimishwa na wafanyikazi kote ulimwenguni kwa minajili ya kukumbushana na kutanabahishana umuhimu wa mshikamano na umoja katika kudai na kutetea maslahi na maendeleo yao. Kwa jumla wafanyakazi hukongamana kwa nia ya kutafakari kuhusu hali yao ya baadaye. Kwa sababu ya umuhimu wa wafanyakazi kuna kila nui ya sababu ya kuienzi sikuhii. Kwao ni siku yao ya kufanya tathmini ya jinsi wanavyotimiza wajibu wao wa kutoa kuzalisha mali pamoja na kutambua changamoto zinazowasakama kwa lengo la kubuni mbinu za kuzikabili. Aidha siku hii hutoa jukwaa kwa wafanyakazi na viongozi wao kuwapa tuzo wenzao waliobobea katika nyanja mbali mbali za kazi zao. Yaani, ni wakati wa methali, mcheza kwao hutuzwa au la, huangaliwa kwa muktadha wa matumizi. Hata hivyo, ukweli mmoja ni kuwa sio wote waliotamba huweza kutuzwa madhali ni muhali kumtuza kila mtu. Ama thamani na manufaa ya tuzo hupatikana katika uchache wake. Jambo muhimu na Ia kukumbukwa ni kwamba kila mfanyakazi ni mchapa kazi, atuzwe asituzwe! Jambo ambalo wafanyakazi hawapaswi kufunzwa, labda kukumbushwa tu, ni kuwa waendelee kufanya kazi kwa ari, umahiri na weledi wa hali ya juu. Mradi ni lazima watambue kuwa nafasi yao katika kuleta maendeleo ya kitaifa ni kubwa mno wala haimithilishwi na chochote. Ni kutokana na kuelewa umuhimu mkubwa wa wafanyakazi ambapo katiba za nchi nyingi kote duniani husabili sahifa nyingi kuangazia masuala ya wafanyakazi. Baadhi ya masuala yanayofafanuliwa ni wajibu wa wafanyakazi na waajiri pamoja na haki za kila kundi ambapo wajibu wa kundi moja ni haki za kundi lingine. Hata hivyo, haiwezekani katiba za nchi kushughuulikia masuala yote ya wafanyakazi. Kwa sababu hii, stakabadhi zingine kama sheria za nchi husika ni adhimu, huduma na mikakati yao hufafanua zaidi kuhusu masuala ya waajiri na waajiriwa. Nyaraka hizi zote huandaliwa katika misingi ya maazimio ya Shirika la Wafanyakazi Duniani yaani ILO. Haimhitaji mweledi kutambua kwamba wajibu mkubwa wa kila mwajiri ni kuhakikisha ya kuwa maslahi ya wafanyakazi yamepewa nafasi ya kwanza katika mipango yake yote. Miongoni mwa waajiri wote, serikali ndiyo mwajiri mkubwa. Hivyo basi, serikali inastahili kuwa kwenye msitari wa mbele katika kutunza na kutekeleza maslahi ya wafanyakazi wake. Jambo linalotamausha ni kushuhudia na kusikia kuhusu visa vingi vya migomo ya wafanyakazi kote duniani wakilalamikia mazingira duni ya kutenda kazi, mishahara midogo, marupurupu madogo na machache, ukosefu wa muda wa mapumziko na kadhalika. Na shani kubwa ni kwamba aghalabu mwajiri anayesusiwa huwa ni serikali. Hofu kubwa hapa ni kwamba serikali zikikosa kujali maslahi ya wafanyakazi wao, waajiri wengine katika sekta ya kibinafsi kama mashirika, taasisi na watu binafsi, hawataona haja ya kufanya hivyo. Na katika hali kama hii basi msemo kwamba kazi isiyo kipimo, mwishowe watu huteta huwa kitulizo kikubwa kwa waajiriwa. Wanapofikia na kufikishwa katika kiwango hiki, wafanyakazi hupandwa na jazba na kariha isiyoruhusu wala kusikiliza ama yoyote ya vitisho au ushauri ila tu utekelezaji wa matakwa yao! Maswali (a) Eleza umuhimu wa kuadhimishwa Sikukuu ya wafanyakazi unavyodhihirika katika aya tatu za kwanza. Maneno 45-50 Matayarisho Jibu (b) Kwa kurejelea aya zilizosalia, andika hoja kuu zinazozungumziwa. (Maneno 90— 100) Matayarisho Jibu

    Date posted: September 28, 2019.  

  • UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :- Utandawazi Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga...(Solved)

    UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :- Utandawazi Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga simu katika nchi jirani barani Afrika, ilimbidi kupitia kwa opareta katika nchi za Ulaya ndipo aunganishwe. Kupigia simu kutoka Gambia kwenda Senegali ilibidi kutumia opareta wa Kule London na wa Paris, Ufaransa, na wa Senegal. Leo hii kuna njia nyingi za mawasiliano zilizo bora, za kutegemewa na zinazofikisha ujumbe kwa kasi sana. Ujumbe ambao ungechukua muda mrefu kuufikisha, sasa unapelekwa kwa sekunde moja. Miongoni mwa njia hizi ni mdahilishi, simu tamba na tuama, faksi, setelaiti, mitandao ya wavuti, n.k. Hamna eneo sasa hivi hata liwe mbali vipi lisilofikika na aina hizi za mawasiliano. Maendeleo haya ya mawasiliano yamechangia pakubwa sana kuufanya ulimwengu kuwa kijiji kimoja. Sasa kuna uhusiano wa karibu sana miongoni mwa mataifa duniani katika Nyanja zote za maisha. Hall hii ndiyo inayoitwa utandawazi au utandaridhi. Utandawazi umeleta mabadiliko mengi maishani. Mojawapo ni utoaji na uzalishaji wa mali. Mabadiliko ya mawasiliano yameruhusu mashirika ya kimataifa kusambaza utoaji na uzalishaji wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali duniani. Hali hii imepunguza gharama za usafirishaji sana. Bidhaa zinazoundwa na kiwanda chenye hakimiliki kilichoko kule New York masafa ya mbali, zinaweza kuzalishwa na kiwanda kilicho hapa Nairobi. Bila shaka umesikia kuhusu madawa ya kurefusha maisha ya wahasiriwa wa UKIMWI ambayo yanazalishwa na baadhi ya viwanda vya kutengeneza madawa humu nchini. Kiwanda chenye hakimiliki kipo jijini London. Viwanda ambavyo vilikuwa katika mataifa tajiri kama vile Uingereza, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Japani sasa vimeweza kutandaza vitandabui vyake kote duniani. Utandazaji huu hufanywa kwa njia kadhaa. Kwanza, viwanda hivi huvinunua viwanda vilivyoko katika mataifa yanayostawi. Vinaweza kuingia katika ubia na viwanda vya mataifa wanakotaka kuhamia. Viwanda hivi vya mataifa yanayoendelea hupatana kuwa watasimamia utoaji na uzalishaji wa bidhaa fulani na kukubaliana namna ya kugawa mapato. Utandawazi katika sekta ya uzalishaji na utoaji bidhaa umeleta manufaa kadhaa katika nchi zinazoendelea. Mojawapo ya haya ni kupatikana kwa nafasi za kazi. Pili, bidhaa za nchi zinazoendelea ambazo hazingeshindana na zile za mataifa yalioendelea sasa zimepata nafasi ya kushindana. Halikadhalika, wateja wana nafasi ya kupata bidhaa watakayo bila kuvunjwa moyo. Iwapo bidhaa anazohitaji mteja hazipatikani katika nchi, zinaweza kuagizwa moja kwa moja kutoka kwa kiwanda kingine chenye uhusiano nacho. Uagizaji hauchukui muda kutokana na hali ya mawasiliano inayoweza kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza wakati. Fauka ya haya, wateja hupata uwanja mpana wa kuchagua wanachokihitaji. Utandawazi umehimiza kustawi kwa mazingira ya mashindano katika utoaji na uzalishaji mali viwandani. Sasa hivi hakuna nchi yenye uwezo Wa kufungia bidhaa za nchi nyingine katika mipaka yake. Kufanya hivi ni kujitia kitanzi kiuchumi. Lazima nchi zifüngue masoko yao. Navyo viwanda vya kimataifa huweza kuwania masoko haya. Matokeo yake ni wateja kufaidika kwa kupata uwanja mpana wa bidhaa za kuchagua. Wateja pia hupata bidhaa za hali ya juu na kwa bei isiyo ghali kutokana na mashindano haya. Mashindano ya kimataifa ni kama ya paka na panya na kiwanda kisichojifunga nira vizuri, huwa kinajihatarisha. Kinaweza kujipata kimetupwa nje ya soko na kuangamia.Manufaa mengine ya utandawazi ni kuwa watu sasa hivi wanaweza kuwasiliana kwa urahisi na wepesi. Kwa kutumia simu, au mdahilishi, mtu anaweza kuwasiliana na mwenzake popote alipo licha ya masafa. Zaidi ya haya, utandawazi umewawezesha watu kutoka asili mbalimbali kuingiliana na kutangamana. Utangamano huu umeweza kuleta umoja baina ya watu kwa kutoa hisia za ubaguzi. Hata hivyo utandawazi umetokeza kuwa na madhara. Kwanza, uchumi wa nchi nyingi umeibukia kutawaliwa na matukio ambayo hayazihusu nchi hizo moja kwa moja. Uvamizi wa kijambazi wa Septemba 11,2000 kule Marekani uliathiri uchumi wa nchi nyingi sana. Matukio ya vita katika Mashariki ya kati nayo yamechangia kuzorotesha uchumi wa nchi nyingi hasa zile maskini ambzo zinategemea mafuta kutoka huko ilhali vita hivyo haviwahusu sikio wala ndewe. Athari kubwa ya utandawazi yaonekana katika sekta ya kijamii. Tamaduni nyingi za jamii katika nchi maskini zinaendelea kuvurugwa na maadili kuporomoka kutokana na ustawi wa kimawasiliano. Vijana wanaiga kutoka mataifa ya kimagharibi bila kuchuja. Si ajabu kuwa vijana wetu wanavaa mavazi yasiyositiri uchi wao vizuri na yasiyostahiki kwa jina la ustaarabu. Wavulana nao huzidisha kwa kutoga masikio na kusuka nywele usiweze kuwatofautisha na dada zao. Maswali (a) Utandawazi ni nini? (b) Ni mambo yapi yanayosababisha kutokea kwa utandawazi? (c) Mashirika ya mataifa yaliyostawi yanatumia mikakati ipi kutandaza vitandabui vyao kote duniani? (d) Fafanua: (i) Manufaa matatu ya utandawazi. (ii) Hasara tatu za utandawazi. (e) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa. (i) Ubia (ii) Mashindano ya paka na panya. (iii) Kutoga (iv) Vitandabui

    Date posted: September 28, 2019.  

  • Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.(Solved)

    Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.

    Date posted: September 26, 2019.  

  • Kanusha sentensi hii Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.(Solved)

    Kanusha sentensi hii Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.

    Date posted: September 26, 2019.  

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. i) twaa (kutendeka) ii) Kosa (Kutendesha) iii) Cha (Kutendwa)(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. i) twaa (kutendeka) ii) Kosa (Kutendesha) iii) Cha (Kutendwa)

    Date posted: September 26, 2019.  

  • Maneno haya yamo katika ngeli gani? i) Fagio ii) Nyigu(Solved)

    Maneno haya yamo katika ngeli gani? i) Fagio ii) Nyigu

    Date posted: September 26, 2019.  

  • Ngeli ni nini?(Solved)

    Ngeli ni nini?

    Date posted: September 26, 2019.  

  • Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii...(Solved)

    Soma taarifa ifuatavo kisha uiibu maswali Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii imetambuliwa kama mojawapo ya lugha za mawasiliano katika muungano wa Afrika. Magwiji wa Kiswahili wamechaguliwa kuunda msamiati mwafaka kutegemea mabadiliko ulimwenguni na kuingiza katika matumizi kupitia tarakilishi. Mpango huu utakapo faulu, mtu ataweza kutumia tarakilishi akiwasiliana kwa Kiswahili. Juhudi hizi heri zizidi kupongezwa na nyingine kuimarishwa Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili barani ni mojawapo wa hatua za kufanikisha juhudi hizi. Taasisi kama hiyo itatafiti historia ya lugha, mabadiliko yake na maenezi, msamiati wake na kuleta usawa wa mazungumzo kwa Kiswahili miongoni mwa mambo mengine.Kuweka lugha hii katika maandishi ni jambo litakalochangia kuimarisha lugha ya Kiswahili. Vitabu ,magazeti, na majarida yatakayolenga kiwango cha wasomaji yaandikwe na bei yake isiwe ghali mno ili wengi waweze kugharamia. Tanzu zote za lugha zizingatiwe.Lugha hii ifunzwe na kutahiniwa katika daraja zote za elimu. Lifanyapo hili, bila shaka lugha ya Kiswahili itaimarika.Uajiri wa wafanyikazi ukitambua ujuzi katika lugha hii hadhi yake itaimarika.Tafsiri ya kazi zilizoandikwa katika lugha mbalimbali zikifanywa katika Kiswahili, lugha hii itakua na kukitamizizi kwingi ulimwenguni.Watu wengi watapata hamu ya kusoma kazi asilia na ile ya tafsiri yake.Redio na magazeti ni vyombo muhimu katika kuwasiliana na kundi kubwa la watu kote duniani. Vyombo hivi vya mawasiliano kwa umma vikihimiza matumizi ya Kiswahili, bila shaka mchango mkubwa utaonekana katika kustawisha lugha hii. Vipindi maalumu matangazo na burudani vizingatie matumizi ya Kiswahili.Mashindano kati ya shule na shule,nchi na nchi ya kianzishwa na kuzingatiwa yanaweza kuimarisha Kiswahili pakubwa. Mashairi, mijadala, matokeo ya utafiti fulani, nyimbo, ngano na hadithi za kufunza umma ni njia za kuwezesha kufanyiwa mashindano kama hayo.Mikakati hii na mingine ikizingatiwa itakuwa mbolea nzuri ya kukuza lugha ya Kiswahili. Maswali i) Bila kubadilisha maana iliyokusudiwa ,fupisha aya mbili za mwanzo. (maneno 35 - 40) ii) Andika kwa muhtasari juhudi zinazofaa katika uimarishaji wa lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa Makala haya. (maneno 70 -80)

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo.(Solved)

    Soma nakala yafuatayo kishaujibu maswali Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoukabili mataifa yanayoendelea. Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yaloyaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao. Vyanzo vya umaskini huu ni anuwai ; mathalan, ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabirika,idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalo husika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu na adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili. Jamii ya xxxxxxx mpaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi fulani unaathari pana sana.Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuwa msingi ambako matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina. Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwamuhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea. Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora yakupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umasikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima ya zingatie uhalisi wa maisha ya raia wa mataifa hayo. a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea? b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea? c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini? d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga? e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya: i) Kulitadarukia ii) Kuatika iii) Kuyaburai madeni

    Date posted: September 25, 2019.  

  • "Asanteni sana kwa kuja, sisi. . . hukabiliana na mengi."(Solved)

    Damu Nyeusi na Hadithi nyingine : Ken Walibora na Said A. Mohamed "Asanteni sana kwa kuja, sisi. . . hukabiliana na mengi." i) Eleza muktadha wa dondoo hili. ii) Fafanua matukio yaliyosababisha mkutano huu. (alama 4) iii) Jadili changamoto sita zinazokumba jinsia ya kike katika hadithi hii.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Matatizo yanayowakumba wanacheneo ni kielelzo cha matatizo yanayowakumba wananchi wa mataifa mengi ya ulimwengu wa tatu. Thibitisha ukerejelea "Mstahiki Meya".(Solved)

    Matatizo yanayowakumba wanacheneo ni kielelzo cha matatizo yanayowakumba wananchi wa mataifa mengi ya ulimwengu wa tatu. Thibitisha ukerejelea "Mstahiki Meya".

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Mstahiki Meva : Timothy M. Arege "Nilikusahau lini. . , ? Mtu haukati mkono unaomlisha.(Solved)

    Mstahiki Meva : Timothy M. Arege "Nilikusahau lini. . , ? Mtu haukati mkono unaomlisha. a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. b) Taja na ueleze mbinu ya kifasihi iliyotumika katika dondoo hili. c) Eleza sifa nne za msemewa. d) Kwa kutoa mifano mitano thibithisha jinsi viongozi wa cheneo walivyoukata mkono uliokuwa ukiwalisha.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Huku ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea thibitisha kwamba vijana wana suluhu tosha kwa matatizo yanayoikumba jamii wanamoishi.(Solved)

    Huku ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea thibitisha kwamba vijana wana suluhu tosha kwa matatizo yanayoikumba jamii wanamoishi.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Kidagaa kimemwozea ; Ken Walibora . .. alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima na kutetemeka kama waliopigwa na dhoruba ya theluji."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea ; Ken Walibora . .. alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima na kutetemeka kama waliopigwa na dhoruba ya theluji." a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Bainisha hulka ya mrejelewa. c) Huku ukitoa mifano mwafaka jadili mchango wa wanawake katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Andika kinyume. Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.(Solved)

    Andika kinyume. Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi ifuatayo; Ule wangu niliopalilia unakua vizuri.(Solved)

    Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi ifuatayo; Ule wangu niliopalilia unakua vizuri.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.(Solved)

    Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Andika visawe vya maneno haya; i) Wajihi ii) Laazizi(Solved)

    Andika visawe vya maneno haya; i) Wajihi ii) Laazizi

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea. Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.(Solved)

    Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea. Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo. Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.(Solved)

    Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo. Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa. Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.(Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa. Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari, Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumai kujengea nyua.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari, Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumia kujengea nyua.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Kanusha Ukiona vyaelea vimeundwa.(Solved)

    Kanusha Ukiona vyaelea vimeundwa.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Andika kifungu kifuatacho katika msemo wa taarifa; Amani alilia, "Marafiki zangu, majambazi wamenipiga na kunipora pesa zangu zote. Mali yangu sasa hali yangu nimbaya(Solved)

    Andika kifungu kifuatacho katika msemo wa taarifa; Amani alilia, "Marafiki zangu, majambazi wamenipiga na kunipora pesa zangu zote. Mali yangu sasa hali yangu nimbaya."

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha maana ya neno 'ilimradi'(Solved)

    Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha maana ya neno 'ilimradi'

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Ainisha vielezi katika sentensi hii. Mwalimu wetu anayefundisha kistadi hutembea kwa maringo.(Solved)

    Ainisha vielezi katika sentensi hii. Mwalimu wetu anayefundisha kistadi hutembea kwa maringo.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Tunga sentensi moja yenye viungo vya sarufi vifuatavyo;(Solved)

    Tunga sentensi moja yenye viungo vya sarufi vifuatavyo; i) Kikanushi ii) Kiima katika nafsi ya pili wingi. iii) Kiwakilishi cha wakati uliopita. iv) Mtendewa katika nafsi ya tatu wingi. v) Mzizi wa kitenzi cha silabi moja. vi) Mnyambuliko wa kitenzi kauli ya kutendea.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Taja sifa mbili bainifu za vokali /i/(Solved)

    Taja sifa mbili bainifu za vokali /i/

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Eleza maana ya sauti.(Solved)

    Eleza maana ya sauti.

    Date posted: September 25, 2019.  

  • Ubinafsishaji wa mashirika ya umma ni nguzo kuu katika ulimwengu wa leo.(Solved)

    Soma kifungu kisha uiibu maswali Ubinafsishaji wa mashirika ya umma ni nguzo kuu katika ulimwengu wa leo. Kimsingi, ubinafsishaji ni hatua na harakati zinazochukuliwa kupunguza kushiriki kwa serikali katika uendeshaji wa mashirika na kuhimiza kupanuka kwa sekla ya kibinafsi.Serikali huweza kuhimiza, kutokana na uuzaji, uhawilishaji wa mali kutoka umiliki wa umma hadi kwenye umilikaji wa sekta ya kibinafsi. Aidha, serikali inaweza kuuza hisa zake kwenye mashirika ya umma. Njia nyingine ni kuchochea ugavi wa zabuni kupitia kwa mikataba ambayo inashindaniwa na mashirika au kampuni tofauti. Lengo kuu la ubinafsishaji ni kuigatuanafasi ya serikali katika utendakazi na uendeshaji wa mashirika.Uuzaji wamashirika ya kiserikali au hisa huwa chanzo cha mapato yanayoweza kutumiwa kuendesha miradi mingine, Hii ni njia ya kupunguza harija ya serikali inayotokana na uendeshaji wa mashirika yasiyoleta faida. Ubinafsishaji huzuia uwezekano wa kuingiliwa kwa mashirika na wanasiasa, huimarisha utamaduni mpya wa muundo wa mashirika na huvunja uhodhi wa kiserikali. Ubinafsishaji huweza kuatika mbegu za ujasiriamali wa raia kutamani kuanzisha amali tofauti. Ubinafsishaji huweza kuyaruhusu mashirika ya kimataifa kutwaa mashirika muhimu nchini, kufutwa kazi kwa wafanyikazi na kuongezeka kwa umaskini. Ubinafsishaji wa sekta zinazohusiana na elimu na afya huweza kuathiri vibaya wenye mapato ya chini. Ubinafsishaji haumaanishi ufanisi wa utendakazi wa makampuni na mashirika. Aidha, ikiwa haupo utaratibu mzuri wa kutathmini au kupima thamani za hisa pana uwezekano wa hisa zinazouzwa kupewa thamani ya juu au ya chini. Maswali a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu, andika muhtasari wa aya ya kwanza na ya pili. (Maneno 35 - 40). b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya tatu na ya nne. (Maneno 45 - 50)

    Date posted: September 25, 2019.