Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

61904 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.(Solved)

    Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.(Solved)

    Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    “Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)

    Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea...(Solved)

    “Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea kiweo hakikatwi.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa dondoo. (b) Tambua tamathali ya lugha iliyotumika katika dondoo. (c) Ni maudhui yapi yanayojitokeza katika dondoo hili? (d) Fafanua sifa mbili za mzungumzaji wa kauli ya kwanza.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali....(Solved)

    “Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali. Nimechoka kuongolewa kwa wimbo wa performance contract.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa nukuu hii. (b) Thibitisha tamathali mbili za usemi zinazodhihirika katika dondoo hili. (c) Maudhui gani yanayowasilishwa katika dondoo hili? (d) Kwa mujibu wa riwaya, ni mambo yapi yanayomchosha mzungumzaji wa kauli hii.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la...(Solved)

    “Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili. (c) Taja mbinu ya sanaa iliyotumika katika dondoo hili. (d) Jadili hulka moja ya msemaji wa dondoo hili kwa kurejelea dondoo. (e) Eleza kinyume cha kauli ya nafsineni kwa kurejelea hoja tano kutoka kwenye riwaya.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri) (a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu. (b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama...(Solved)

    “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri) (a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu. (b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama msemaji maishani.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa...(Solved)

    “Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa fimbo!” (a) Weka maneno haya katika muktadha wake. (b) Fafanua masuala mengine saba aliyowasilisha mzungumzaji. (c) Kwa kurejelea sehemu nyinginezo za riwaya, jadili sifa zozote nne za mzungumzaji wa dondoo hili.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa...(Solved)

    “Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza masaibu yaliyomkumba baba anayerejelewa maishani mwake.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii. (c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji...(Solved)

    “Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii. (c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji na wakimbizi wengine katika kambi ya wakimbizi.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.(Solved)

    Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.(Solved)

    Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala...(Solved)

    “Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala katika dondoo hili? (c) Fafanua kilichokuwa kimetukia kabla ya dondoo hili. d) Taja sifa mbili za mamake Umulkheri. (Naomi)

    Date posted: February 6, 2023.  

  • “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)(a) Weka dondoo hili katika muktadha...(Solved)

    1. “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri) (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake faafu. (b) Eleza mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (c) Eleza jinsi mrejelewa alivyomsaidia nafsineni.

    Date posted: February 6, 2023.  

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. WASAKATONGE 1. Wasakatonge na juakali Wabeba zege ya maroshani, Ni msukuma mikokoteni, Pia makuli bandarini, Ni wachimbaji wa migodini, Lakini...(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. WASAKATONGE 1. Wasakatonge na juakali Wabeba zege ya maroshani, Ni msukuma mikokoteni, Pia makuli bandarini, Ni wachimbaji wa migodini, Lakini maisha yao chini 2. Juakali na wasakatonge Wao ni manamba mashambani, Ni wachapa kazi viwandani, Mayaya na madobi wa nyumbani, Ni matopasi wa majaani, Lakini bado ni masikini. 3. Wasakatonge na juakali Wao huweka serikalini, Wanasiasa madarakani, Dola ikawa mikononi, Wachaguliwa na ikuluni, Lakini wachaguaji duni 4. Juakali na wasakatonge Wao ni wengi ulimwenguni, Tabaka lisilo ahueni. Siku zote wako matesoni, Ziada ya pato hawaoni, Lakini watakomboka lini? (Mohammed Seif Khatib) (a) “Shairi hili ni la kukatisha tamaa”. Fafanua rai hii kwa kutoa mifano minne. (b) Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na uonyeshe mifano miwili ya jinsi iiivyotumika. (c) Eleza umbo la shairi hili. (d) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari. (e) Onyesha mifano miwili ya maadiii yanayojitokeza katika shairi hili. (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi. (i) Manamba (ii) Tabaka lisilo ahueni

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata: Kila Mchimba Kisima Musa Mzenga 1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima, Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia, Kalmia yenye upendo, kufurahisha...(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata: Kila Mchimba Kisima Musa Mzenga 1. Tenda utendapo tendo, tenda tendo kwa hekima, Lindamane mwenendo, sawa na yakio kalmia, Kalmia yenye upendo, kufurahisha mtima, Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe. 2. Utendapo la faraja, tendo ni yako salama, Ya kukupa kila tija, na ushindi wa daima, Upate njema daraja, duniani na kiyama, Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe. 3. Utendapo la miuja, tendo ni yako nakama Ya kukutia harija, hasara kukuandama, Usione afuwaja, mwanza ajue heshima, Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe 4. Nakwambia uelewe, pulika ninayosema, Si ari ya mwenginewe, kumuonya kwa lazima, Mtu hufunza mwanawe, Kwanza ajue heshima, Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe. 5. Nisipokwambia wewe, kukufunza kila jema, Kusudi nikuongowe, uepukwe na tujuma, Matusi ndimi nipawe, ila na kila lawama, Kila mchimba kisima, bundi hungia mwenyewe 6. Hii si heri ujuwe, matusi kuigandama, Hadhi usiniuzuwe, hamithilishwa na nyama, Fikiri moyo utuwe, nikupapo taaluma Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe. 7. shika tena utambuwe, wasia huu ni mwema Matendo usipunguwe, mazuri kutenda hima, Yatende ubarikiwe, upawe na taadhima Kila mchimba kisima, budi hungia mwenyewe. 8. Yakupasa uchunguwe, kila jambo kulipima Upime ufafanuwe, mambo yote kwa alama La kuwaka ulijuwe, pia lipi la kuzima, Kila mchimba kisima hungia mwenyewe. a) Eleza maudhui ya shairi hili. b) Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili una hadhira lengwa tatu. Zitaje na utoe mifano. c) Eleza umuhimu wa kipokeo kinachotumiwa katika shairi hili

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata: KIBARUWA: Abdilatif Abdalla Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa! Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa...(Solved)

    Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata: KIBARUWA: Abdilatif Abdalla Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa! Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa Ndipo mte ukatipuza! Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-. Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza? Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza? Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza? Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotoshelezaIsipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza? Viulize: Ni nani huyo ni nani! Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya? Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya? Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya? Viulize: Ni nani huyo nani1 Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao “Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!” a) Eleza dhamira ya shairi hili. b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya kimuundo mshairi d) Huku ukitoa mifano, eleza kwa kifupi mwelekeo wa mshairi kuhusu vibarua. e) Andika ubeti wa tano katika lugha ya nathari f) Onyesha utata wa maana katika matumizi ya Kibaruwa Manamba

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. Dhamiri yangu Dhamiri imenifunga shingoni. Nami kama mbuzi nimefungwa Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi Na nimekwishachora duara. Majani niwezayo kufikia yote nimekula. Ninaona...(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. Dhamiri yangu Dhamiri imenifunga shingoni. Nami kama mbuzi nimefungwa Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi Na nimekwishachora duara. Majani niwezayo kufikia yote nimekula. Ninaona majani mengi mbele yangu Lakini siwezi kuyafikia: kamba, kamba. Oh! Nimefungwa kama mbwa. Nami kwa mbaya bahati, katika Uhuru kupigania, sahani ya mbingu Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena Kuifikia na hapa nilipofungwa Nimekwishapachafua na kuhama siwezi. Kamba isiyoonekana haikatiki. Nami sasa sitaki ikatike, maana, Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba Aliharibu na mbwa aliuma watu. Ninamshukuru aliyenifunga hapa Lakini lazima nitamke kwa nguvu “Hapa nilipo sina uhuru!” (E. Kezilahabi) (a) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia. (b) Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru? (c) Eleza rnaana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. “Kamba isiyoonekana haikatiki.” (d) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hili. (e) Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza katika shairi hili. (f) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • HAKI 1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu, Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu, Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu, Tutokwe na utu! 2. Hatutakufanya, mwana kwa...(Solved)

    HAKI 1. Haki watutisha, tusikuandame, kwa matendo yetu, Watukorofisha, tusikuandame, kila penye kitu, Mbona watugwisha, miba ituchome kwenye huu mwitu, Tutokwe na utu! 2. Hatutakufanya, mwana kwa mvyele; aliyemzaa, Haki watunyima, machumi ya mbele, na nyingi hadaa, Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa, Haki twashangaa! 3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu, Tunakutazama, kwa kuulizia, kuweza thubutu, Na kwenye milima, ilotueka, kupandia watu, Usifanyekatu! 4. Sio hao mabwana, waloteuliwa, kupata mwangaza, Haki wakubana, lilotarajiwa, kwenye hichi kiza, Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza, Kambi yatuviza! 5. Haki buna njia, kizuizi mali, ndio njia panda, Tukiifatia, hatufiki mbali, wengi tunaganda, Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda, Haki yatuponza! 6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kwisha haribika, Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itavyopatika, Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika, Kwetu nimashaka! 7. Haki hufanyiki, papitapo mambo, na vikubwa visa, Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa, Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa, Nandio ya sasa! 8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa, Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa, Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa, Haki wauliwa! 9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae, Hatuna ashiki,kuvutalahaja,haki ituvae, Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae, Haki tamati! (Suleiman A. Ali) Malenga Wapya (a) Eleza dhamira ya shairi hili. (b) Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (c) Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (d) Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi katika shairi hili. (e) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (f) Mshairi ana maana gani kwa kusema: (i) Kambi yatuviza (ii) Kuweza tukisi.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Capture.JPG (a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (b) Shairi hili ni la aina gani? Toa...(Solved)

    Capture.JPG (a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (b) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja. (c) Eleza mambo matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili kujitegemea. (d) Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake. (e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (f) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi: (i) Ghaibu (ii) Tukamshabihi.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali 1. Huno wakati mufti, vijana nawausia, Msije juta laity, mkamba sikuwambia, Si hayatti si mamati, vijana hino dunia, Uonapo vyang’aria,...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali 1. Huno wakati mufti, vijana nawausia, Msije juta laity, mkamba sikuwambia, Si hayatti si mamati, vijana hino dunia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 2. Japo aula kushufu, na machoni vyavutia, Dunia wana dhaifu, waugua nisikia, Vijana nawasarifu, falau mkisikia, Ukiona vyang’aria, tahadhari vitakula. 3. Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria, Msije andama baa, makaa kujipalia, Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 4. Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia, Wajimwaie uturin na mapoda kumichia, Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 5. Wawapi leo madume, anasa walopapia? Wamepita ja umeme, leo yao sitoria, Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 6. Nambie faida gani, nambie ipi fidi? Upatayo hatimani, waja wakikufukia, Ilakufa kama nyani, kasoroyako mkia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 7. Kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia, Ujifanye kama kwamba, u jiwe huna hisia, Wakwambe watalokwamba, kwa lolote vumilia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 8. Vyatiririka tiriri, vina vyanikubalia, Alo bora mshairi,pa tamu humalizia, Nahitimisha shairi, dua ninawapigia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. 9. Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia, Wakinge wanarika, na anasa za dunia, Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia, Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula. (Mwalaa M.Nyanje) (a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (b) Fafanua kwa kutoa mifano, mbinu nne alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (c) Nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili inasema na pande mbili. Zieleze pande hizo. (d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. (e) Bainisha toni ya shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana, Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana, Kiwa ni riziki yangu,...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana, Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana, Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona, Ni wakati utanena. Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipazao nao, Wapitao wakiimba, eti mimi, ningapenda hali zao, Haupandiki mgomba, wana nyemi, fisadi wa hadhi zao, Eti ni kwa raha zao. Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa, Ni mtu kuwa hawara, wa vitimbi, ama alozawa tasa? Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa, Waama sina makosa Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo, Muwaite watribu, kina Siti, watuzwa ilimu hiyo, Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo, Kwalo sichafuki moyo Hidhuru yote ni bure, sio kitu, kudhiki asodhikika, Siwi nikaona ghere, lailatu, nyota njema itafika, Kwa shangwe na njerejere, kila mtu, mdomo utafumuka, Akiri amejibika. (Mwalaa M. Nyanje) (a) Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa. (b) Fafanua mambo matano ambayo mzungumzaji (nafsineni) anapinga katika shairi hili. (c) Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili. (d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (e) Eleza muundo wa shairi hili. (f) Bainisha matumizi mawili ya tafsida katika shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Watafuta Riziki 1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni Vyakula washakiki, visipungue vinyuani. 2. Watafuta riziki, wahaingaikao...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Watafuta Riziki 1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni Vyakula washakiki, visipungue vinyuani. 2. Watafuta riziki, wahaingaikao mijini Kutwa kile na hiki, kama watanga na mipini Japo hawasikii, hawakosi kujiamini 3. Watafuta riziki, wazalendo wa nchi hii Kamwe hawajidhiki, tama za moyo kutii Bali huafiki, kupingana na ulaghai 4. Watafuta riziki, pato ambalo la halali Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali (a) Fafanua sifa tano za watu wanaozungumziwa katika shairi hili. (b) Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (c) Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (i) idadi ya mishororo katika beti. (ii) mpangilio wa vina (iii) mpangilio wa maneno

    Date posted: February 1, 2023.