Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

61904 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza 1 Ngakua na mato, ya kuonea Ngalisana kito,cha kuchezea Kilicho kizito, cha kuelea Kikamuenea,...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza 1 Ngakua na mato, ya kuonea Ngalisana kito,cha kuchezea Kilicho kizito, cha kuelea Kikamuenea, akivae. 2 Makusudi yangu,ngaliandaa Ngafinyanga chungu, cha mduwaa Ngatia vitangu,vinavong’aa Ili ziwe taa, kwa apikae. 3 Mkungu wa tano, wa mduwara Ulo bora mno, kisha imara Ulo na maono, kuwa ni dira Kwenye barabara, itindiae. 4 Ngaomba Baraka, kwake Rabana Punje za nafaka, kila aina Chunguni kuweka, kwa kulingana Hajaangu suna, yule alae. 5 Ngafanya bidii, kwenda mwituni Sio kutalii, kukata kuni Ya miti mitii, huko jikoni Isio na kani,ni iwakae. 6 Kwa yangu mabega, nikathubutu Ngabeba mafiga, yalo matatu Bila hata woga, kwenye misitu Simba tembo chatu, sinitishie. 7 Miti yenye pindi,na jema umbo Ngajenga ulindi, mwema wimbombo Fundi aso fundi, penye kiwambo Moyo wenye tambo, apekechae. 8 Singaajiri, ngachimba mimi Kisima kizuri, cha chemchemi Maji ya fahari, ya uzizimi Jua la ukami, siyaishae 9 Tamati nafunga, kwa kuishia Mato ndo malenga, kanikimbia Nahofu kutunga, mabeti mia Asije chukia, ayasomae. (a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (b) Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi aliotumia mshairi. (c) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (d) Eleza toni ya shairi hili. (e) Fafanua aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (f) Bainisha nafsi neni katika shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Mwili Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili. Vitisho kamwe...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Mwili Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili. Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili. Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili. Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili. Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili. a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili. c) Eleza toni ya shairi hili. d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili? e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande. f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa hamu Kushika mpini na kutokwa jasho Ili kujikimu kupata malisho. Anapotembea anasikiliza Videge vya anga vinavyotumbuiza Utadhani huwa vimemngojea Kwa usiku kucha kuja kumwimbia; Pia pepo baridi kumpepea Rihi za maua zikimletea Nao umande kumbusu miguu; Na miti yote hujipinda migongo kumpapasa,kumtoa matongo; Na yeye kuendelea kwa furaha kuliko yeyote ninayemjua Akichekelea ha ha ha ha ha ha … Na mimi kubaki kujiuliza Kuna siri gani inayomliwaza? Au ni kujua au kutojua? Furaha ya mtu ni furaha gani katika dunia inayomhini? Ukali wa jua wamnyima zao Soko la dunia lamkaba koo; Dini za kudhani zamsonga roho Ayalimia matumbo ya waroho; Kuna jambo gani linamridhisha? Kama si kujua ni kutokujua Laiti angalijua, laiti angalijua! (T. Arege) Maswali a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili. c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili. d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili: i. tashhisi ii. kinaya iii. tashbihi f) Eleza toni ya shairi hili. g) Bainisha nafsineni katika shairi hili. h) Changanua muundo wa shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona unyoofu wake Unyoofu ambao unatisha zaidi Punde natumbukia katika shimo Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena Ghafla nakumbuka ilivyosema Ile sauti zamani kidogo “Kuwa tayari kupanda na kushuka.” Ingawa nimechoka Jambo moja li dhahiri Lazima nifuate barabara Ingawa machweo yaingia Nizame na kuibuka Nipande na kushuka Jambo moja nakukumbukia: Mungu Je, nimwombe tena? Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu Nashangaa tena! Kitu kimoja nakiamini Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu Nikinaswa na kujinasua Yumkini nitafika mwisho wake Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla. (a) Eleza toni ya shairi hili. (b) Tambua nafsineni katika shairi hili. (c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu? (d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka. (e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (f) Eleza maana ya: (i) kuruba (ii) barabara yenye ukungu

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami...(Solved)

    Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami imani, wala kupanga siasa Mwasema sayansini, siku ningalitosa Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia. Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza. Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia? Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa. Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote Msamiati huwa, ni wa Afrika yote Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika. Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia. Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana Kukua imeridhia, msamiati kufana Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia. Maswali (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu (b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha. (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (d) Eleza toni ya shairi hili. (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu. (f) Bainisha nafsineni katika shairi. (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. i. nasongwa ii. kuriaria iii. adinasi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)

    Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti, Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti, Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati, Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti, Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti Maisha ya kupishana, yule ende yule keti, Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti, Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti, Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti, Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati, Sote tungeambatana, kama ukosi na shati, Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati, Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Peleleza utaona, hayataki utafiti, Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati, Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti, Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti, Yote tuloelezana, katenda bila senti, Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? (Abdalla Said Kizere) Maswali a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili. b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi. d) Eleza umbo la shairi hili. e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano. f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi. g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)

    Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)

    Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)

    Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)

    Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)

    Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi(Solved)

    Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi(Solved)

    Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi(Solved)

    Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo: a) Sakarani b) Ngonjera c) Malumbano d) Masivina e) Taabili f) Mandhuma g) Kisarambe h) Mavue i) Sabilia j) Togoo k) Kumbukizi(Solved)

    Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo: a) Sakarani b) Ngonjera c) Malumbano d) Masivina e) Taabili f) Mandhuma g) Kisarambe h) Mavue i) Sabilia j) Togoo k) Kumbukizi

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani(Solved)

    Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno(Solved)

    Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Eleza aina za mashairi kulingana na vina(Solved)

    Eleza aina za mashairi kulingana na vina

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo(Solved)

    Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti (Solved)

    Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.(Solved)

    Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Nini maana ya bahari za mashairi?(Solved)

    Nini maana ya bahari za mashairi?

    Date posted: February 1, 2023.  

  • Taja visawe vya mashairi huru(Solved)

    Taja visawe vya mashairi huru

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Taja visawe vya mashairi ya jadi(Solved)

    Taja visawe vya mashairi ya jadi

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini Naja kwingine kuwapi,...(Solved)

    Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo? Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo? Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando? Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini Naja nije rudi papo, panigedeme mgando Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini (Limenukuliwa) Tunaainisha shairi hili kama la jadi kwa sababu:

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Taja sifa za mashairi huru(Solved)

    Taja sifa za mashairi huru

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Nimeyaandika maneno haya kwa niaba ya, Mamilioni wasio malazi Wazungukao barabarani bila mavazi Wabebao vifurushi vilivyo wazi, … milki yao ya maisha. Kwa niaba ya: Maelfu wanaovuma bila haki Wiki baada ya wiki Leo...(Solved)

    Nimeyaandika maneno haya kwa niaba ya, Mamilioni wasio malazi Wazungukao barabarani bila mavazi Wabebao vifurushi vilivyo wazi, … milki yao ya maisha. Kwa niaba ya: Maelfu wanaovuma bila haki Wiki baada ya wiki Leo sumu au spaki Leo kamba au bunduki Na kwa wale wanasubiri kunyongwa Kwa niaba ya Vijana walio mtaani Wale mayatima na maskini Wazungukao mapipani Kila pembe mjini Kuokota sumu kutia tumboni Kujua bila kujua ’ili kupata kuishi. Kwa niaba ya: Wakongwe wasiojiweza Walao chakula kilichooza Wachukuao choo wakijipakaza Pole pole wakijiangamiza Katika vyumba vyao Baridi na giza Kwa saba hawan watazama Wala wauguza Eleza sababu za kuliita shairi hili huru

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Fafanua migao/kategoria mbili kuu za mashairi(Solved)

    Fafanua migao/kategoria mbili kuu za mashairi

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Eleza maana za istilahi zifuatazo za ushairi; i. Bahari ii. Diwani(Solved)

    Eleza maana za istilahi zifuatazo za ushairi; i. Bahari ii. Diwani

    Date posted: January 30, 2023.  

  • Malenga ni nani?(Solved)

    Malenga ni nani?

    Date posted: January 30, 2023.