Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Q&A Categories


Do you have Q&A pairs? Post them here

61904 Questions  View: All | Solved | Unsolved



Search Results...
  • Andika katika usemi taarifa. “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.(Solved)

    Andika katika usemi taarifa. “Tutawatembelea wazazi wetu leo jioni” Leo alimwambia Asha.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Andika katika ukubwa wingi. Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.(Solved)

    Andika katika ukubwa wingi. Kitoto kijeuri kikiletwa kitarejeshwa kwao.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi. Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia mbinu ya matawi. Mwanafunzi stadi amenunua kitabu kizuri.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Yakinisha sentensi hii. Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.(Solved)

    Yakinisha sentensi hii. Simba asiponguruma wanyama wote hawababaiki.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'(Solved)

    Taja sifa mbili bainifu za vokali 'U'

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.(Solved)

    Taja sauti mbili ambazo ni vikwamizo na hutamkiwa kwenye ufizi.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Wakaazi wengi wa maeneo ya kitajiri miji yetu hawajui wapo chini ya utawala wa machifu.Huenda wakasalia katika hali hii ya kutojua hadi wanapokosa kulipa ujira wa watumishi wao wa nyumbani halafu maskini mwajiriwa huyu anaripoti kwa chifu, kwa kuwa ni hali yake. Chifu ni uzi muhimu katika vazi Ia kijamii. Bila hawa maafisa, jamii kama tunavyoijua ingeporomoka. Wakati mwingine hawaungwi mkono. Mfano mzuri ni kukataliwa kwa katiba kielelezo cha Wako, Novembe 2005, wakati wa kura ya maoni. Kwa sababu jukumu la chifu au kibadala chake halikudhihirishwa wazi wazi katika kielelezo, wengi walikataa stakabadhi hiyo, wakihofia sasa hawataweza kufikia mtawala wao kushughulikia malalamishi yao. Nimeishi mtaa wa Nairobi West miaka mingi na kuhudhuria kamati nyingi za lokesheni, chini ya uwenye kiti wa chifu akisaidiwa na naibu na wazee. Mikutano, pia inahudhuriwa na madiwani, inspekta wa askari tawala na wawakilishi wengi na washia dau katika lokesheni. Takribani kila swali linalogusia maslahi ya jamii linajadiliwa na kuchunguzwa na maazimio kupitishwa. Mada muhimu wakati wa mikutano hii ni usalama, taa za barabarani, ulanguzi wa mihadarati hasa karibu na taasisi za elimu, kudumisha usafi wa vyoo vya umma, kudumisha usalama kupitia kwa raia na swala nyeti la vioski. Kazi ngumu ya chifu ni kuwazia kila kju. Kwa mfano, mwenye kioski ni sharti apate mkate wa kila siku na sehemu ya biashara yake iliyoko ni muhimu. Ikiwa kioski kitajengwa na kukiuka sheria za baraza la jiji au ikiwa wizi usiofahamika na utumizi wa dawa za kulevya unatokea kufuatia kukua kwa idadi ya vioski katika eneo, shinikizo zinaelekezwa kukuwa kwa wenye vioski. Chifu lazima azingatie shinikizo za umma hatari za kiusalama na hofu za wenye vioski kabla ya kufanya uamuzi ikiwa mijengo hiyo ibomolewe. Tatizo jingine ni watoto wa barabarani. Makao ya kuwakimu ni machache kama walivyo wahudumu wa kijamii, suluhu ni nini? Tuwatupe katika ukumbi wa kijamii, ambao watahepa pindi tu, wapatapo fürsa ndogo au wapelekwe huduma kwa vijana wa Taifa, ambapo wachache wanaweza kutunzwa kwa wakati mmoja. Ili kufaulu kwa wengine, sharti wawe katika vituo vya urekebishaji tabia za matumizi ya dawa za kulevya. Tuwakabidhi polisi kwa sababu wanaranda au tujaribu kuungana na vituo vya urekebishaji tabia kuhakikisha hawatarudi barabarani. Mazingira ya lokesheni pia huibuka katika ajenda. Hali ya barabara, juhudi za kusafisha mazingira, wizi wa maji na umeme, usafiri wa umma, uchafuzi wa mazingira, hewa na kelele, hii inatokea kupitia malalamishi ya watu wanaoishi karibu na mabaa na uzingativu wa saa ya biashara hujadiliwa kila mara. Chifu ni sharti afahamu sheria na kanuni zinazotawala hali hizo, halafu ajadili na wahusika kabla ya kutoa mwelekeo. Usawa na uwazi katika kugawa fedha za Hazina ya maendeleo ya maeneo Bunge, pia hujadiliwa. Katika maswala haya mengine, chifu ndiye aliye nyanjani. Anawajibikia jamii na wakubwa wake na hatarajii shukrani au kutambuliwa kwa kazi njema aliyofanya. Isipokuwa hukashifiwa anapofeli. Watu wengine wana taswira ya Chifu kama mtu kwenye jukwa, kofia yake. na kifimbo kinachompa mamlaka ya kuhutubia baraza, Kajubu tyji zaidi ya hivyo. Kwa mujibu wa kitabu cha mafunzo ya machifu na Naibu wao (Januari 2004), wajibu wa chifu ni kuwakilisha sera na mipango ya serikali kwa wananchi. Chifu ni ajenti wa “mabadiliko” mwenye wajibu Wa kuhamasisha watu katika maendeleo. Anajishughulisha na kujua ni nani maskini katika lokesheni, mkoa, mgonjwa asiyeweza kupata tiba na kupanga jinsi mhasiriwa atakavyopelekwa hospitali kama anavyoweza. Ni sharti ashughulikie ugomvi wa kinyumbani, uhalifu wa watoto, dhuluma za watoto, agawe chakula na mavazi kwa wahitaji na kuhukumu kesi ndogo za wizi na uharibifu. Chifu hutatua kesi za kisheria kwa wasioweza kumudu wakili. Wakati wananchi wanapohisi mbunge wao hafikiliki na hawana imani na polisi, chifu ndiye suluhisho. Lakini kuna machifu wachache ambao hawafanyi kazi yao vyema. Kwa ufupi, chifu ni mkusanyiko wa kushngaza; mfalme katika himaya yake, pasta, baba msikivu, wanasaikolojia, mtunga sheria na mdumisha sheria, balozi mchaguzi, mama, mlumbi na askari asiyechelewa. Ingawa halipwi vyema, anafanya kazi bila tarakilishi, na aghalabu hujilipia gharama ya kodi ya afisi yake kutoka mfuko wake. Kwa sababu ni mtumishi wa umma, tunataraji afanye kazi mufti. Hiyo haimaanishi tusishukuru kwa kazi njema aliyofanya. Serikali inaweza kufanya hivi kwa kuimarisha hali yake ya kazi, mazingira yake ya kikazi, na kuhakikisha yana tarakilishi, anapata mafunzo ya uongozi na usimamizi. Wananchi sharti washukuru watu hawa kwa kujitolea sabili. Maswali a) Fupisha aya nne za kwanza (Maneno 60) Matayarisho Jibu b) Kwa maneno kati ya 80-90 fupisha aya ya tano hadi mwisho. Matayarisho Jibu

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo halafu ujibu maswali Kama kuna jambo ambalo limeiparaganya akili yamahuluki ni kuielewa dhana ya demokrasia. Kiumbe huyu heshi kuuliza mkururo wa maswali. Demokrasia ni nini hasa? Tunaweza kula demokrasia? Ni dude gani hili lina kichwa au mkia pekee yake? Je demokrasia inazuia njaa? Demokrasia ni himaya ya wasomi tu au vilevile ni haki ya mafalahi? Kwa muda mrefu kumekuwa na kinyang‟anyiro kikubwa katika jamii ambacho azma na. matokeo yake yamekuwa ya kutatanisha. Baadhi ya watu wamejitokeza kama mchuzi wa ugali na kuzusha zahama ambazo si za kuyumkinika. Vichwa vya adinasi vikafyekwa kwa miundo na maparange na matumbo yakapasuliwa na kuapakaza utumbo na vijusi kila mahali. Shingo zikapigiwa vigingi na kukomewa ardhini. Demokrasia si mchezo wa lelemama. Ni sharti tujifunge vibwebwe tumwage damu na tufe ili tupate demokrasia ya kweli!” Mmoja wa mibabe wa demokrasia alinguruma kadamnasi ya umati huku ngoma za vita zikirindima.” Hata Marekani na ulaya walimwaga damu. Mamilioni ya watu walipukutishwa na kimbunga cha demokrasia. Chini walilaliana kama Vimatu na tunutu. Hawa manafiki wanafikiri hatuwajui. Katu hatutakubali porojo zao. Wanatupikia majungu kisha wakatoweka. Kuna demokrasia ya Afrika na ile ya Ulaya „ mkereketwa wa Uafrika akachanganua. Demokrasia ya Afrika basi imefuata mkondo huu wa umwagikaji damu. Kila kukijiri uchaguzi zahama hutawala. Walio madarakani hawataki kubanduka. Hutaruta visababu vya kukwepa wimbi la ushinde. Demokrasia ni mchezo wa mizengwe tu ati. Hali hil imesababisha maafa makubwa, uharibifu mkubwa wa mali, majeraha, ukimbizi wa raia ndani na nje ya mataifa husika, dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake, kuzagaa kwa magonjwa ainati, uhasama wa kikabila. Jambo la kusikitisha ni kwamba raia na viongozi hawaelekei kujifundisha chochote kutokana na hali. Huku mataifa mengi Ulayani na Asia yakikwea daraja moja baada ya nyingine kimaendeleo, Afrika imedumaa tu. Imesalia kuimba ule wimbo wake wa kutokea azali„ Tutaendelea vipi na tunadhulimiwa na kaka wakubwa”. Siasa ya demokrasia katika bara la Afrika ina tija kubwa hususan kwa wale wachache wanaofanikiwa kudhibiti nyenzo za kutia tonge kinywani. Ulitima wa umma husalia miradi hewa ya tabaka la viongozi ambayo hutumiwa kujinadi zamu nyingine ifikapo tena. Demokrasia ya kweli imo mikononi mwa umma pale utakapojikomboa kimawazo na kwa ujasiri kudai huduma bora, uajibikaji na kuheshimiwa kwa mkataba wa kijamii uliosisiwa na Jean Jacques Rousseau. Maswali a) Binadamu amechanganyika kwa njia ipi? b) Ni vipi Demokrasia ya kweli inaweza kufikiwa c) Kwa nini inasemekana kuwa „Demokrasia ni mchezo wa mizengwe? d) Ni athari gani hutokana na kinyang‟anyiro cha Demokrasia? e) “Dhiki za raia zimesalia kuwa mradi-hewa wa wanasiasa” Eleza. f) Fafanua maana ya maneno na mafungu yafuatayo jinsi yalivyotumika katika taarifa. i) Mafahali ii) Wanatupikia majungu iii) Ukarabati

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Laleni!(Solved)

    Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Laleni!

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? i. Nyasi ii. Furaha(Solved)

    Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? i. Nyasi ii. Furaha

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano. -baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)(Solved)

    Tunga sentensi mbili ukitumia mzizi uliopewa ili kuonyesha mwingiliano wa maneno katika mabano. -baya (kivumishi kuwa kiwakilishi)

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. i. Ningeenda leo ningefika mapema. ii. Ningalienda ningalifika mapema.(Solved)

    Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo. i. Ningeenda leo ningefika mapema. ii. Ningalienda ningalifika mapema.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Andika maana mbili za sentensi ifuatayo. Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.(Solved)

    Andika maana mbili za sentensi ifuatayo. Wanafunzi walipigia wazazi wao simu.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tunga sentensi uliyopewa upya bila matumizi ya ‘amba’ Ndoo ambayo ilinunuliwa ilivunjwa jana.(Solved)

    Tunga sentensi uliyopewa upya bila matumizi ya ‘amba’ Ndoo ambayo ilinunuliwa ilivunjwa jana.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Onyesha Nomino na ueleze aina katika sentensi ifuatayo: Warembo walijifukiza manukato na kuvalia mavazi ya kupendeza.(Solved)

    Onyesha Nomino na ueleze aina katika sentensi ifuatayo: Warembo walijifukiza manukato na kuvalia mavazi ya kupendeza.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Sahihisha sentensi zifuatazo. i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa. ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo. i. Hao mandugu wamekosana juu ya pesa. ii. Mtu mwenye anakula mkate ametumana aletewe chai.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Geuza kwa wingi. i. Njia hii huenda Kisumu ii. Wembe huu utafaa.(Solved)

    Geuza kwa wingi. i. Njia hii huenda Kisumu ii. Wembe huu utafaa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Kanusha sentensi ifuatayo: Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo: Ningalifuzu katika mtihani wangu ningalituzwa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Sahihisha sentensi ifutayo. Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.(Solved)

    Sahihisha sentensi ifutayo. Sukari zilizowekwa mfukoni zimenyeshewa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani. i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa. ii. Hamisi ni daktari wa meno.(Solved)

    Onyesha vitenzi kisha uvieleze ni vya aina gani. i. Kakangu amewahi kutembelea makavazi ya kitaifa. ii. Hamisi ni daktari wa meno.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Ainisha sentensi hii: Kilichopikwa(Solved)

    Ainisha sentensi hii: Kilichopikwa

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo: i. Silabi za irabu pekee ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu iii. Silabi za konsonanti pekee(Solved)

    Andika maneno yaliyo na aina za silabi zifuatazo: i. Silabi za irabu pekee ii. Silabi za konsonanti, nusu irabu na irabu iii. Silabi za konsonanti pekee

    Date posted: November 25, 2022.  

  • SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI. Malezi mema Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza Atafikia kilele, mzazi atampuza(Solved)

    SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI. Malezi mema Malezi bora si yale, mtoto kumdekeza Atafikia kilele, mzazi atampuza Utapiga makelele, wala hatasikiza. Daima usikubali, kuridhi kumpendeza Lazima uwe mkali, mengine kumkataza Na wala usikubali, maneno kuyaigiza. Mtoto ukimuita, hana budi kuginiza Sio mdomo kufyata, mamboye kuendeleza Ama dakika zapita,aje ikimpendeza. Mzazi usithubutu,mwanao kumteteza Uambiwapo na watu, mwanao alifanyiza Kuwa na hali ya utu, Kadhia kuchunguza. Iwapo amekusudi, makossa kuyatimiza Kumrudi huna budi,jukumu kutekekeza Lau usipomrudi, kosa taliendeleza. Maswali a) Eleza malezi mema jinsi yanavyosimuliwa na mshairi. b) Taja mambo matano wanayoshauriwa wazazi kutoyatenda c) Je, mzazi asipochukua jukumu lake, kuna athari gani kwa mtoto d) Toa methali moja inayoambatana na ujumbe wa Shairi hili e) Shairi hili lina mishororo ngapi f) eleza vina,vipande na mizani vya Shairi hili g) eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika Shairi. i. kumdekeza ii. kuginiza iii. mdomo kufyata iv. alofanyiza v. lau usipomrudi

    Date posted: November 25, 2022.  

  • “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko" i. tambua kipera hiki ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla(Solved)

    “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko" i. tambua kipera hiki ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele(Solved)

    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele Naomba la uhakika, jawabu enyi wavyele Wa kuume tangu lini, kuukata wakushoto! Tangu dahari miaka, mikono ina upole Meungana pasi shaka, ni miwili vile vile Mmoja ukisumbuka, mwingine hujaa ndwele Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto! MASWALI a. Shairi hili ni la arudhi. Dhibitisha kwa kutoa sababu tatu b. Nakili kibwagizo cha shairi hili c. Eleza ujumbe mmoja unaojitokeza kwenye shairi

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.(Solved)

    Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.(Solved)

    Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.(Solved)

    Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.(Solved)

    Bainisha kivumishi katika sentensi hii. Matunda mawili yaliuzwa.

    Date posted: November 25, 2022.  

  • Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari. Walituchezea(Solved)

    Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari. Walituchezea

    Date posted: November 25, 2022.