Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Tanzu za lugha katika mawasiliano
Date Posted:
10/8/2017 1:12:18 AM
Posted By: SAW Membership Level: Silver Total Points: 122
pia kujirekebisha unapokosea.
Dosari/udhaifu ya maongezi
Hayana hifadhi ya kudumu kuhusu yale yaliyozungumzwa kwa hivyo mzungumzaji anaweza kukana aliyoyasema.
Ni vigumu kudhibiti makundi makuu ya watu.
Kuna uwezekano wa kukatizana na kukosa mweleko wa kimazungumzo.
Maranyingi washiriki huathiriana kwani huonana uso kwa uso.
Ubishi huweza kuzuliwa hasa washiriki wanapokosa kuelewana kuhusu mada Fulani.
Kadri muda,mazingira na wahusika wanavyo badilika ndivyo kiini cha ujumbe kinaweza kupotea na kubadilika kabisa.
(2)maandishi
Maranyingi hutumiwa katika mawasiliano yenye urasmi ambapo hati maalum ya lugha hutumiwa kupitisha ujumbe.huweza kutumiwa katika ripoti,barua,kumbukumbu,taarifa na Makala mengineyo ya kifasihi.
Manufaa ya maandishi
Maandishiyana rekodi ya kudumu ya ujumbe unaowasilishwa na huweza kurejelewa baadaye.
Isipokuwa katika uchapisho mpya wa ujumbe na maandishi hubaki ule ule.
Msomaji huwa na muda wa kutosha kusoma,kuchambua na kutafsiri maandishi kadri ilivyokusudiwa na mwandishi.
Kuna ushahidi wa kutumia na kupokea ujumbe
Maandishi huweza kutolewa katika Makala mengine na kusambazwa kwa watu wengi ilikupata ujumbe huo huo kwa wakati mmoja.
Maandishi ni nyenzo rahisi na pia yenye uwazi wa kupitisha maswali nyeti.
Udhaifu wa maandishi
Ni vigumu kudhibitisha iwapo ujumbe uliotuma kimaanishi imesomwa na kueleweka kwa mpokezi.
Majibu na maitikio ya ujumbe hayawezi kufikia mwasilishwaji moja kwa moja
Maandishi yakiwa na kasoro ni vigumu sana kurekebisha hivyo basi kasoro hiyo inakuwa moja wapo ya ujumbe, hayawezi kufikia mwasilishwaji moja kwa moja.
Maandishi hayana nafasi ya mjadala au mashauriano kati ya mwandishi na mpokezi.
(3)Ishara
Ni zile alama na miondoko inayotumiwa kuwasilisha ujumbe pasipona kutumia lugha.hujumlisha ishara ishara uso,macho,kichwa,mikono,na viungo vinginevyo kupasha ujumbe.
Matumizi ya ishara hutegemea muktadha pamoja na kaida ya jamii.
Sperber anasema kwamba chochote unachokionyesha ama katika kukimya ni ishara ya mawasiliano.picha za hizi ishara sauti za kuarifu hujumlishwa katika mawasiliano ishara.
Udhaifu wa ishara
Isipokuwa ishara maalum ishara nyingi huhitaji maarifa kuhusu jamii husika ilikupata kuwasiliana
Ishara huweza kutafsiriwa visivyo hivyo kusababisha ugomvi.
Ishara zinazo tumiwa katika mawasiliano na watu wenye upungufu ya kuongea huhitaji ufunzaji iliueleweke.
Huhusika na muktadha pekee ya mazungumzo.
Next: Making our country self-sufficient food supply
Previous: Limitations of income per capita in measuring the standards of living in different countries