Helpdesk: WhatsApp: 0736552548 Email: info@kenyaplex.com

Sifa Za Nyimbo Za Bembelezi

Institution: Pwani university

Course: Bachelor of Education

Content Category: Articles

Posted By: Joe kinyua

Document Type: DOCX

Number of Pages: 5

Price: KES 50
 
    

Views: 19880     Downloads: 6

Summary

SIFA ZA NYIMBO ZA BEMBELEZI

Bembelezi kama nyimbo za kuimbia Watoto ndio watulie, waache kulia nawalale (Bakiza 2010). Huwa na baadhi ya sifa mbali mbali. Haji na wenzake (1992) wamefasili nyimbo za kuchombezea watoto kuwa ni nyimbo ambazo huimbiwa mtoto mchanga kwa ajili ya kumburudisha. Bali ni hayo Wamitila (2003) anasema bembelezi hukusudiwa kumlaza mtoto au kumuongoa aache kulia, huweza pia kutumiwa kupitisha ujumbe fulani. Wamitila anaendelea kusema kuwa bembelezi huweza kutumiwa kama njia ya kumpiga vijembe mzazi wake ikiwa anaehusika ni mlezi. Sifa hizi ni kama vile:
Huimbwa kwa maadhi ya chini na sauti nyororo.
Katika uimbaji wa nyimbo za bembelezi ni muhimu tufahamu kuwa mahadhi na mapigo yanafaa kushuka na kwa utaratibu . Akivaga na Odaga (1992) wanadai kuwa nyimbo bembelezi huimbwa kwa utaratibu na kwa sauti nyororo, uamilifu wa bembelezi, wanavyodai ni kudokeza au kubainisha jambo fulani kuhusu jamii husika. Sauti nyororo huchukua umakinifu wa mtoto katika hali yake ya kusikiza huwa pia anaburudika.Pia, sauti ya chini husababisha mazingira ya mtoto kuingia kwa ulimwengu wa usingizi.Nyimbo hizi huwa nzuri kwa jumla na Watoto wanaolia hujipata wametulia na wakati mwingine wao hulala.
.................


Below is the document preview. Purchase to access the complete document.

  • Sifa-Za-Nyimbo-Za-Bembelezi_14084_0.jpg
  • Sifa-Za-Nyimbo-Za-Bembelezi_14084_1.jpg
........

This is the end of this document preview. Buy to download the complete document.


More Resources



View all resources