Helpdesk: WhatsApp: 0736552548 Email: info@kenyaplex.com

Grade 7 Shughuli za Kiswahili na Novela for End Term 3 Assessment Test 2023

Institution: Junior Secondary

Course: Shughuli za Kiswahili na Novela

Content Category: Examinations

Posted By: swezlim98

Document Type: PDF

Number of Pages: 7

Price: KES 70
 
    

Views: 724     Downloads: 3

Summary

COMPETENCE BASED CURRICULUM JUNIOR SCHOOL
SCHOOL BASED ASSESSMENT 2023 GRADE 7
GREDI YA SABA KISWAHILI SEHEMU YA B
ZOEZI 3: UFAHAMU WA KUSOMA
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 4.
Zamani za kale, wanyama waliishi katika nchi ya Tegemeo. Simba ndiye aliyekuwa mfalme wao. Nchi hii
ilibarikiwa kwa rasilimali nyingi. Si misitu, si nyika, si bahari, si milima … Yakini nchi hii ilikuwa nchi
yenye fanaka.
Moja kati ya rasilimali kuu za nchi hii ilikuwa ziwa. Wenyewe waliliita Ziwa la Uhai. Humo mlipatikana
wanyama kama vile mamba na samaki wa aina mbalimbali. Wavuvi wengi walimiminika humo kujizumbulia
riziki.
Japo Ziwa hili lilistahili kuwafaidi wanyama wote, kuna baadhi ya wanyama waliotaka kufaidika zaidi
kuliko wengine. Miongoni mwao alikuwa Fisi. Daima kiumbe huyu hakuridhika. Aliwaonea wengine kijicho
hata kwa juhudi zao. Hakuacha kuwazuia wanyama wadogo kama vile Sungura na Kobe kuvua samaki na
kuchota maji humo. Wanyama wengine walimlilia hali Simba, naye Simba hakukawia kumshika sikio
kiumbe huyu. Alipoona hali imezidi, Simba alimtumia Fisi mjumbe, Mbweha. Mbweha alijaribu
kumkanya. Fisi alibadilika siku mbili tatu lakini akarudia tabia yake. Unajua tena tabia ni ngozi ya mwili.
Wanyama waliendelea kuungulika kutokana na tabia hii ya Fisi. Siku moja Kobe aliamua kumfunza
adabu Fisi. Alimwendea Simba na kumwelezea mpango wake. Simba aliridhia huku akimwonya dhidi ya
kufanya jambo ambalo ni kinyume cha haki.
‘‘Ndugu, Fisi, ninajua kwamba unalipenda na kulitunza ziwa letu kama mboni ya jicho. Sijui kama
umebahatika kusikia tetesi kwamba adui yetu amekuwa akilitumia ziwa, kulichafua na hata kutuzuia
sisi akina Kobe kulitumia. Ninaona ni heri tuukomeshe uovu huu.’’ Kobe alimwambia Fisi.
Bila kuwaza zaidi, Fisi alitimua mbio hadi ziwani kukabiliana na adui huyu. Kobe alimfuata unyounyo
huku akivunjika mbavu kwa kicheko cha ndani kwa ndani. Alisimama kando ya Fisi na kumwashiria kivuli
chake Fisi kilichotazamana ana kwa ana na Fisi mwenyewe. Fisi hakujua vipi, lakini alijipata akitapatapa
majini, amekirukia kivuli chake, ndicho adui! Maskini ! Fisi hakujua kuogelea. Isingekuwa Duma ambaye
alifika ziwani wakati huohuo, Fisi angekuwa hadithi ya kusimuliwa.
.................


Below is the document preview. Purchase to access the complete document.

  • Grade-7-Shughuli-za-Kiswahili-na-Novela-for-End-Term-3-Assessment-Test-2023_14924_0.jpg
  • Grade-7-Shughuli-za-Kiswahili-na-Novela-for-End-Term-3-Assessment-Test-2023_14924_1.jpg
........

This is the end of this document preview. Buy to download the complete document.


More Resources


More Content By swezlim98


View all resources